Nikiwa kama MwanaCHADEMA Kanda ya Pwani. Nitapiga kampeni Halima Mdee arejeshwe. Tuanze na Kura humu mtandaoni

Nikiwa kama MwanaCHADEMA Kanda ya Pwani. Nitapiga kampeni Halima Mdee arejeshwe. Tuanze na Kura humu mtandaoni

Je Halima Mdee Arudi au asirudi Chadema?


  • Total voters
    42
  • Poll closed .
Arudi haraka sana, pia mnyika kwenye nafasi ya ukatibu amepwaya, ni wakati muafaka sasa chadema iiajiri katibu mwanamke, naye si mwingine bali ni Halima Mdee!!
Mnataka kumaliza chama kumpa msaliti Mdee chama bora mayeba sio mdee msaliti ni msaliti tu Huyo team Mbowe lia lia alikua manzi ya Mbowe
 
Hehee! Kumekucha na Makucha yake.

Halima Mdee ndani ya nyumba. Twajua afanya makosa lakini kosa moja lafutaje jasho na damu zake peke zake.

Nitapiga nakupiga kampeni. Erythrocyte tunajua ugomvi wako na Halima Mdee haujaanza juzi wala Jana. Umekwama. Na bado
ahadhari tu.
Kura yako ni haki yako lakini isiwe ni njia ya kupitisha hata wasiostahili.
Itabidi ujieleze kwanza; kama mimi nitakavyojieleza kukataa kata kata kwa kinyago kama Yericko kuwa sehemu ya chama hicho.

Natumaini umenielewa ninachojaribu kutahadhalisha kisiwe kama mazoea tu ndani ya chama.
Mazoea yalishatuonyesha huko CCM sifa ya "uwenzetu" ni turufu tosha kabisa ya kuwa mwanachama mwenye matumaini makubwa ndani ya chama hicho.
Hili lisiruhusiwe kuingia ndani ya CHADEMA.

Unatuhimiza tuanze na kura humu, wakati hujatueleza lolote juu ya ushawishi wako kuhusu Halima?
 
Sikuwahi kujua kama ww kiongozi hii ndio id yako. Akina Halima kumbuka walienda hadi mahakamani kulinda ubunge wa kihuni. Ninachojua ni kuwa Mdee sio mfia chama bali ni mfia cheo. Mtu wa aina yake ndio hao watatumika kutoa Siri za chama. Arudi abaki bila cheo kama alivyo Dr. Slaa.
Bila shaka yoyote; haya ndiyo mambo mazito sana yanayohitaji kupimwa kwenye mizani ya yeye kufikiriwa kurudi ndani ya CHADEMA.
Bila ya kuyapuuza haya, ni muhimu pia kuchambua kwa kina na kujuwa nguvu iliyokuwa ikiyapa msukumo.

Hili ulilosema hapa ni doa lisiloweza kusafishwa kiurahisi; lakini pia inafaa kumpa nafasi ya kujieleza juu yake.

Kabla ya mkasa huu, ilikuwa ni rahisi kwa mtu kumtaja Halima kuwa mmoja kati ya nguzo imara sana ndani ya chama hicho; na mchango wake katika kuongoza kundi la wenzake kukiasi chama kama ilivyofanyika, ni miongoni mwa mambo muhimu yanayohitaji ufafanuzi.

Kukaa kwake kimya hadi wakati huu, wakati wenzake wote wakionyesha ubovu wao juu ya imani yao juu ya chama, nalo ni jambo muhimu linalompambanua yeye na kundi hilo.
 
Halima Mdee hatakiwi na alishafukuzwa Chadema. Cha ajabu hajawahi kutoka hadharani na kusema nini kilitokea. Kurejeshwa Chadema itatuvunja moyo. Halima kama anarejeshwa apewe masharti maalum na moja liwe kueleza hadharani nini kilitokea mpaka akafikiri yeye no mkubwa kuliko chama
Tuache nongwa arejeshwe mpiganaji. Iwapo Lowassa aliwahi kurudishwa CCM na Bulaya vilevile sembuse HALIMA Mdee kutenda kosa kwa mara moja si tatizo,shida ni kurudia kosa ni...? huo ndio ubinadamu.
 
ahadhari tu.
Kura yako ni haki yako lakini isiwe ni njia ya kupitisha hata wasiostahili.
Itabidi ujieleze kwanza; kama mimi nitakavyojieleza kukataa kata kata kwa kinyago kama Yericko kuwa sehemu ya chama hicho.

Natumaini umenielewa ninachojaribu kutahadhalisha kisiwe kama mazoea tu ndani ya chama.
Mazoea yalishatuonyesha huko CCM sifa ya "uwenzetu" ni turufu tosha kabisa ya kuwa mwanachama mwenye matumaini makubwa ndani ya chama hicho.
Hili lisiruhusiwe kuingia ndani ya CHADEMA.

Unatuhimiza tuanze na kura humu, wakati hujatueleza lolote juu ya ushawishi wako kuhusu Halima?

Nitahakikisha hilo linatokea
 
Tuache nongwa arejeshwe mpiganaji. Iwapo Lowassa aliwahi kurudishwa CCM na Bulaya vilevile sembuse HALIMA Mdee kutenda kosa kwa mara moja si tatizo,shida ni kurudia kosa ni...? huo ndio ubinadamu.
Uko serious, yaani mtu arejeshwe cdm kwa kuwaiga ccm? Fahamu cdm ni chama cha siasa, wakati ccm sio chama cha siasa bali dola. Cdm hawaigi upuuzi wowote wa ccm boss.
 
Uko serious, yaani mtu arejeshwe cdm kwa kuwaiga ccm? Fahamu cdm ni chama cha siasa, wakati ccm sio chama cha siasa bali dola. Cdm hawaigi upuuzi wowote wa ccm boss.

Na bado
 
Back
Top Bottom