mdukuzi
JF-Expert Member
- Jan 4, 2014
- 20,925
- 51,688
Sikumbuki mwaka ila nakumbuka nilikuwa mdogo ,tulitoka na mzee wangu mitaa ya kariakoo tukaelekea mitaa ya Magomeni Mapipa mtaa sikumbuki ila ni karibu na Shibam.
Kufika pale kulikuwa na vijana watoto wamjini hakuna aliyezidi miaka 50,walikuwawakicheza draft,bao,zumna na kunywa kahawa
Vijana wa makamo wawili walikuwa wakicheza draft mmoja akamfunga mwenzake,akamtania kuwa hajui kitu bora acheze na mimi,hapo nikaachiwa nicheze na yule mwingine,yule mwenzake akaenda kusikiliza ushabuki wa mpira,walikuwa wamemzunguka mtu mmoja mnene mfupi ba sauti ya kukwaruza.
Miaka michache baadae nikagundua kumbe yule mtu niliyecheza nae draft ni Mh Waziri wa fedha Jakaya Mrisho Kikwete.
Na yule mtu mfupi mwenye sautiya kukwaruza alikuwa Jamhuri Kihwelu Tantalila,mchezaji wa zamani wa Simba.
Nilikuja tena kuonana na Mh Kikwete akiwa kwenye foleni ya ATM,CRDB Bank Holland House,Ohio Street,kipindi hicho akiwa waziri wa mambo ya nje miaka zaidi ya kumi tangu tukio la Magomeni.
Baada ya hapo niliishia kimuona kwenye luninga na magazetini
Kama mtakumbuka kipindi akiwa Rais alikuwa akitokea mara kadhaa kwenye media akishiriki mazishi ya watu ambao hata hawajulikani nchini,watu hao ni marafiki zake wa hali ya chini kabisa wakiwemo wa magomeni na Saigon Club na Hugo House Kinondoni alikokuwa akienda kunywa Supu
Kuna Mheshimiwa mmoja ajifanya kuigiza kuwa ni mtu wa matabaka yote ila technolojia ikamuumbua,muuza kahawa ni afisa wa TISS,mwingine akamuuzia muhindi wa kuchoma na bastola kiunoni kumbe ni maigizo tu .uungwana hauji kwa maigizo bali huzaliwa nao.
Kwa viongozi wa sasa sidhani kama kuna wazori wa fedha anayeweza kukaa kijiweni jioni,au waziri wa mambo ya nje anayeweza kukaa kwenye foleni ya ATM
Viongozi mmekuwa miungu watu mpaka mnatwambia tukimbilie Burundi.
Jifunzeni kujishusha kama Mh.Jakaya Kikwete nanyi mtakwezwa