Nikiwa Rais ntaanzaisha mradi wa kuactivate nyota ambazo haziko active (blackholes)

Nikiwa Rais ntaanzaisha mradi wa kuactivate nyota ambazo haziko active (blackholes)

Huwezi kuwa Rais ikiwa ndoto yako ni ku deal na blackholes, watu wanahitaji kukombolewa na ujinga maradhi na umasikini wewe unakuja na hoja za blackholes???

Hata raia wa nchi kama America hawawezi kuwa interested na idea kama hii.

Hizi ni idea ambazo zinakuwa pursued na private companies kama kina Elon Musk wanavyofanya na ikitokea ikawa successful basi ndo serikali wanatoa support fulani ndogo ila hawawezi kugharamia project kama hii mwanzo mwisho
 
Kumbe Jupiter na Saturn ni nyota? Na zinazalisha mwanga wake kama lilivyo jua letu? 😳

Black holes zinatokana na nyota kubwa (giant stars) zilizoishiwa Hydrogen (na Helium); na hivyo kusinyaa (collapse) ndani kwa ndani mumo kwa mumo. Hizi ni kwa zile ambazo nguvu ya uvutano inayovutia ndani huishinda nguvu inayosukuma kwa nje. Nguvu inayosukuma kwa nje ikiishinda nguvu inayovuta kwa ndani nyota hizi zinazokaribia mwisho wa uhai wake huweza kuripuka kama supanova. Hili limeshathibitishwa na telescopes za Hubble na James Webb. Kama jua letu lingekuwa ni kubwa sana (giant star), huu ndiyo ungekuwa ndiyo mwisho wake baada ya miaka kama bilioni 4 hivi ijayo - ama lingeripuka kama supanova au lingesinyaa mumo kwa mumo na kuwa blackhole. Kulingana na saizi yake kuwa ndogo, jua letu hili litakapoishiwa na Hydrogen basi "litanenepeana futufutu" na kuwa kubwa halafu jekunduu (red giant); na hatimaye litakufa kabisa na kuwa dead star!

Sasa wewe unaposema kuwa utayafufua manyota makubwa yaliyokufa na kuwa black holes, utatoa wapi matrilioni na matrilioni ya tani za Hydrogen (na Helium)? Na utawezaje kuingia na kutoka katika black holes ambako tunaambiwa kuwa nguvu za uvutano ni kubwa mno kiasi kwamba hakuna kinachoweza kutoka kikiingia isipokuwa tu labda mabaki kidogo ya nguvu za mnunurisho wa mwanga (Hawking Radiation)?

Na utafikaje kwenye hiyo black hole wakati black hole iliyo karibu zaidi kwetu ni Gaia ambayo kuifikia ni safari ya miaka 1,500 kwa roketi inayosafiri kwa spidi ya mwanga? Natumaini unajua kwamba kulingana na makalikyulesheni ya Albert Einstein katika nadharia yake ya Relativity, haiwezekani kwa kitu chenye mass (hata kama ni punje ya mchele) kusafiri kwa spidi ya mwanga maana itahitajika nishati kubwa/nyingi isiyo na kikomo. Sijui wewe utatumia njia gani kuifikia Gaia kama safari yenyewe tu inachukua miaka 1,500 kwa spidi ya mwanga 😳

Akina Profesa Michio Kaku wanasema kwamba kwa vile kwenye black holes hakuna muda, siku moja wanasayansi wangeweza kupata njia ya kuweza kwenda kuishi humo ndani basi wangeweza kuishi milele. Na hata kuna dhana kwamba huenda mbinguni ni ndani ya black hole ndiyo maana kuna kuishi milele na milele huko (yaani hakuna muda!)

Wanasayansi wenyewe wanakiri kwamba hawajui hasa kinachoendelea katika black holes maana kanuni za kawaida za Fizikia huko hazifanyi kazi; hata muda haupo. Kwenye black holes ni sawa na kilichokuwepo kabla ya Big Bang - wanasayansi hawajui na Fizikia ya sasa haiwezi kutupa majibu. Labda wewe ndiyo utakuwa mtu wa kwanza kutueleza kwa kinagaubaga kilichokuwa kinaendelea kabla ya Big Bang na kinachoendelea ndani ya black holes. Na nakuhakikishia. Utakuwa maarufu kuliko hata Albert Einstein na Stephen Hawking maana utaleta mvuvumko mpya katika Fizikia na pengine hata kuweka mazingira rafiki ambapo nadharia za Relativity na Quantum Mechanics zinaweza kuunganishwa na au kuwa compatible (jambo ambalo Albert Einstein mwenyewe alitumia zaidi ya miaka 30 ya maisha yake bila mafanikio)

Na bila shaka unajua lugha inayotumika - ni mafomyula na makalikyulesheni. Siyo tu blah blah za mtu aliyeshiba makande yake huko Upareni na kuanza kupayuka. Weka makalikyulesheni yako yanayoonyesha jinsi utakavyosafiri mpaka kufika huko kwenye black hole ya karibu, mahali utakakopata gazilioni na gazilioni za tani za Helium na Hydrogen, jinsi utakavyoziwasha hizo nyota tena ili zianze kusaga hiyo Hydrogen (wakati huo wewe sijui utakuwa umesimama wapi!) na mengineyo mengi ambayo hata kinadharia tu hayawezekani kwa sasa!
 
Kumbe Jupiter ni nyota? Na inazalisha mwanga wake kama lilivyo jua letu?

Black holes zinatokana na nyota zilizoishiwa Helium na Hydrogen na hivyo kusinyaa (collapse) ndani kwa ndani. Hizi ni kwa zile ambazo nguvu inayovuta ndani huishinda nguvu inayosukuma kwa nje. Nguvu inayosukuma kwa nje ikiishinda nguvu inayovuta kwa ndani nyota hizi zinazokaribia mwisho wa uhai wake huweza kuripuka kama supanova. Hili limeshathibitishwa na telescopes za Hubble na James Webb.

Sasa wewe unaposema kuwa utazifufua nyota ambazo zimeshakufa na kuwa black holes, utatoa wapi matrilioni na matrilioni ya tani za Helium na Hydrogen? Na utawezaje kuingia na kutoka katika black holes ambako tunaambiwa nguvu za uvutano ni kubwa mno kiasi kwamba hakuna kinachoweza kutoka kikiingia isipokuwa tu labda mabaki kidogo ya nguvu za mnunurisho wa mwanga (Hawking Radiation)? Wanasayansi wenyewe wanakiri kwamba hawajui hasa kinachoendelea katika black holes maana kanuni za kawaida za Fizikia huko hazifanyi kazi; hata muda haupo.

Na utafikaje kwenye hiyo black hole wakati black hole iliyo karibu kwetu inaaminika ni ile iliyo katikati ya Galaxy yetu ya Milky Way na kufika huko sijui ni miaka milioni ngapi ya mwanga (light years).

Akina Profesa Michio Kaku wanasema kwamba kwa vile kwenye black holes hakuna muda, siku moja wanasayansi wangeweza kupata njia ya kuweza kwenda kuishi humo ndani basi wangeweza kuishi milele. Na hata kuna dhana kwamba huenda mbinguni ni ndani ya black hole ndiyo maana kuna kuishi milele na milele huko (yaani hakuna muda!)
Ww umeelezea vizur na kueleweka zaid ya mleta mada..

Na bado hauutak Uraisi.
 
Kumbe Jupiter ni nyota? Na inazalisha mwanga wake kama lilivyo jua letu?

Black holes zinatokana na nyota zilizoishiwa Helium na Hydrogen na hivyo kusinyaa (collapse) ndani kwa ndani. Hizi ni kwa zile ambazo nguvu inayovuta ndani huishinda nguvu inayosukuma kwa nje. Nguvu inayosukuma kwa nje ikiishinda nguvu inayovuta kwa ndani nyota hizi zinazokaribia mwisho wa uhai wake huweza kuripuka kama supanova. Hili limeshathibitishwa na telescopes za Hubble na James Webb. Na huu ndiyo utakuwa mwisho wa nyota yetu (jua) baada ya miaka bilioni kama 4 hivi ijayo - ama itaripuka kama supanova au itasinyaa mumo kwa mumo na kuwa blackhole japo pia kuna scenarios zingine.

Sasa wewe unaposema kuwa utazifufua nyota ambazo zimeshakufa na kuwa black holes, utatoa wapi matrilioni na matrilioni ya tani za Helium na Hydrogen? Na utawezaje kuingia na kutoka katika black holes ambako tunaambiwa nguvu za uvutano ni kubwa mno kiasi kwamba hakuna kinachoweza kutoka kikiingia isipokuwa tu labda mabaki kidogo ya nguvu za mnunurisho wa mwanga (Hawking Radiation)?

Na utafikaje kwenye hiyo black hole wakati black hole iliyo karibu kwetu inaaminika ni ile iliyo katikati ya Galaxy yetu ya Milky Way na kufika huko sijui ni miaka milioni ngapi ya mwanga (light years).

Akina Profesa Michio Kaku wanasema kwamba kwa vile kwenye black holes hakuna muda, siku moja wanasayansi wangeweza kupata njia ya kuweza kwenda kuishi humo ndani basi wangeweza kuishi milele. Na hata kuna dhana kwamba huenda mbinguni ni ndani ya black hole ndiyo maana kuna kuishi milele na milele huko (yaani hakuna muda!)

Wanasayansi wenyewe wanakiri kwamba hawajui hasa kinachoendelea katika black holes maana kanuni za kawaida za Fizikia huko hazifanyi kazi; hata muda haupo. Kwenye black holes ni sawa na kilichokuwepo kabla ya Big Bang - wanasayansi hawajui na Fizikia ya sasa haiwezi kutupa majibu. Labda wewe ndiyo utakuwa mtu wa kwanza kutueleza kwa kinagaubaga kilichokuwa kinaendelea kabla ya Big Bang na kinachoendelea katika black holes. Na nakuhakikishia. Utakuwa maarufu kuliko hata Albert Einstein na Stephen Hawking maana utaleta mvuvumko mpya katika Fizikia na pengine hata kuweka mazingira rafiki ambapo nadharia za Relativity na Quantum Mechanics zinaweza kuunganishwa na au kuwa compatible (jambo ambalo Albert Einstein mwenyewe alitumia zaidi ya miaka 30 ya maisha yake bila mafanikio)

Na bila shaka unajua lugha inayotumika - ni mafomyula na makalikyulesheni. Siyo tu blah blah za mtu aliyeshiba makande na kuanza kupayuka. Weka makalikyulesheni yako yanayoonyesha jinsi utakavyosafiri mpaka kufika huko kwenye black hole ya karibu, mahali utakakopata gazilioni na gazilioni za tani za Helium na Hydrogen, jinsi utakavyoziwasha hizo nyota tena ili zianze kusaga hiyo Hydrogen (wakati huo wewe sijui utakuwa umesimama wapi!) na mengineyo mengi.
Kuna namna ya kuactivate blackholes izalishe hydrogen na Helium sio kweli kwamba zimeishiwa
 
Tatizo lako unaamini mwafrika hawezi fikiria mambo makubwa
Mimi ntaondoa hiyo kasumba na sisi tuwe na uhuru wa kufikiria mambo makubwa
Don't play victim, ila ushauri wangu ni kwamba rudi shule utakuwa hujaelewa jambo huwezi kusema kwenye sayari ya Jupiter kuna Black hole halafu tukuache tu upite salama, hichi sio kijiwe cha kahawa hii JF lazima tutakupiga maswali
 
Don't play victim, ila ushauri wangu ni kwamba rudi shule utakuwa hujaelewa jambo huwezi kusema kwenye sayari ya Jupiter kuna Black hole halafu tukuache tu upite salama hichi sio kijiwe cha kahawa hii JF lazima tutakupiga maswali
Jupiter na Saturn composition yake ni Hydrogen na Helium sawa na jua

Wazungu wamewadanganya kwamba Jupiter na Saturn ni sayari zile sio sayari bali nyota
 
Back
Top Bottom