Nikiwaambia msioe muwe mnasikia; kwa miezi 4 mwamba kaishi maisha magumu bila mshahara kumbe mkewe ana laki 8 ndani, na usaliti juu kaambulia

Nikiwaambia msioe muwe mnasikia; kwa miezi 4 mwamba kaishi maisha magumu bila mshahara kumbe mkewe ana laki 8 ndani, na usaliti juu kaambulia

Tatizo mnamshamburia mtoa maada badala ya kuoppose kwa point...why do you think he is wrong?
 
MY CHILDS ARE ENOUGH NDO NINI[emoji706][emoji706][emoji706]
Halaf acha kujifananamisha na matajiri kujifariji. Nyie ndo mukiumwa hamna anayeeleweka katika kuwauguza

Sent from my SM-G960U using JamiiForums mobile app
Mmmh mbona ni wengi walikua na ndoa zao ila wapo wanajiuguza wenyewe kwakuwa wenza wao wamewakimbia?

#YNWA
 
Sijao SIHITAJJ KUOA KABISAAA

ila Nina watoto wawili.

Mmoja naishi nae (5 Yrs) na mama ake kaolewa ana maisha yake.

Ila mwengine/wa pili mama ake kagoma kunipa kwasababu ana mwaka na miezi 10 (Dec/2019).

Ila wiki hii nimeongea nae naona kama analegeza vile.

Maana kaniahidi mwezi wa 12 atamtuma home aje kunisalimia.

Nilichomuomba nae akiolewa anipe Mimi mtoto yeye akatafute wengine na huyo mume wake atakaye mpata.

SITAKI KUOA MY CHILDS ARE ENOUGH.

Siamini kama kupinga kuoa ni "Arrogant boy" maana hata huyo Tajiri wa India Rajan alishawahi sema "mahusiano hupunguza akili"

Kwahiyo kwa kauli hii ya Tajiri wa India nikisema nilinganishe mafanikio na akili basi ina maana miss pablo HUNA AKILI maana yeye hana mahusiano NI TAJIRI..!!!

Lakini pia hata Bill gate na Bezos walishawahi nukuliwa "Nimeachana na ndoa kwasababu inanibana sanaa"

Wali maanisha NDOA zinafanya wasi concentrate na Mali zao.

Kwa staili hiyo..

Nikisema nii oppose hoja yako na opinion zao basi miss pablo NDOA INAKUCHELEWESHA SANAA.

Matajiri wakina Dangote, Bill gate, na Benzos walishtuka kwa kuchelewa na kuachana na ndoa.

Ni hayo Tu.

#YNWA

#YNWA

My childs are enough kwel mkuu???

Inaonesha hujalelewa na wazazi wote ndo mana unaona childs are enough ila ngoja tukuache na mtazamo wako Mr Childs are enough!!!!
 
Umeandika kitu kikubwa mnoo , I gree with you [emoji109]
 
We mbwa joka jeusi njoo unaitwa na john michael na mr liverkrussen au liverpool
 
He is very arrogant mkuu. Yaan ukiangalia kwa makini unaona uvulana mwingi ndani yake. Tumpe pole

Sent from my SM-G960U using JamiiForums mobile app
Usimwone jamaa mpumbavu

Heshimu msimamo wake

Binafsi nimeshuhudia visa vingi sana vya kutisha kwenye hizi ndoa za siku hizi .

Ndoa ni moja ya Taasisi inayoongoza kwa unafiki uliopitiliza (hapa huwezi nipinga Nina uhakika umeyashuhudia).nimeshuhudia kwa macho yangu tena watu wangu wa karibu kabisa.

Watu wako wako tu ili mradi ajulikane ni mke wa mtu fudenge fulani au mme wa mtu ila hakuna maana yoyote ya ndoa.

Ukianza kukejeli msimamo wa mtu na kumwona mpumbavu vipi yeye unadhani anakuonaje wewe kwenye akili yake? [emoji1]

Tujifunze kuheshimu mawazo ya watu na kama anavyosema "just agree to disagree and peace out"[emoji3577]

NB: Sijaweka msimamo wangu kwenye hili la ndoa maana Mimi mwenyewe sijafanya maamuzi niinge huko unafikini au ni komae kivyangu japo umri sahihi nimefika .
 
Eeeh bwana ehh ni Mimi Mr. Liverpool Tena.

Weekend hii tumempiga Manure na nyundo Kali sanaa mpaka kapoteana.!!
Sasa jiulize ile ilikua Old Traford, je wakija Anfield..!!!

Turudi kwenye mada ....

HIVI KWANINI HAMSIKII NIKIWAAMBIA MSIOE ??😳😳😳

Sasa Kuna mwenzenu yamemkuta huku ......

Nimemsikitikia sanaaa "Hiii BAGOSHAAAA" (in jiwe's voice)

Mr. Liverpool ni mfanyakazi na mkuu wa idara fulani katika moja ya Halmashauri nchini.

Ana rafiki yake nae ni mkuu wa Idara (kaimu) nyengine (tumuite John).

John kuna jambo alizingua mwezi wa 2 akapigwa SP (Due to Absentees - alisepa kazini wiki bila ruhusa Wala taarifa na aliondoka kiboya hasaa).

John aliishia miezi 4 bila mshahara (akipambana na nisamehe na kumbembeleza HR mpaka wakafungua mshahara, waliufungua mwezi wa 6).

Jana nikaona nipige na John story; "Alitoboa vipi maisha miezi 4 bila MSHAHARA" Tuliongea mambo mengii ila Kuna jambo kanisikitisha sanaaa.

Anasema ........

Kipindi hana mshahara ndio aliijua rangi halisi ya mkewe..!!
Kaishi na mkewe miaka 5 ila hakujua huyu mkewe yuko hivi..!!

Mwezi wa 4 ndio ulikua mwezi mgumu. Hali ilikua ngumu japo kwa nje hakuonyesha.

Alivyoona mambo magumu hasa ilibidi amshirikishe mkewe. Alimueleza kila kitu mkewe japo mkewe ana duka la mahitaji ya nyumbani ambalo alifunguliwa na John ila alimjibu hana kitu.

(John alioa mama wa nyumbani ila aliamua kumfungulia duka ili asiwe wa nyumbani kabisa..!!!)

Ikabidi John anyamaze tu "mtu gani kwenye biashara miaka miwili apati faidi ye kila siku anatangaza hasara?"
John alijiuliza mengi akaona anyamaze alale.

Maisha yalikua taiti, John alikosa hela ya bia na ya manhood (kulinda wallet).
Ye alikua ana hakikisha tu mwanae mmoja wa ndoa anakula na kufurahi.

Kumbe bana John alikua anapitia mengi kwa siri sanaa na hata kula alikua anakula mgahawa wa mbali ili tusimuone yule mzoea makuku ana kula maharage..!!!

Aliogopa aibu na maneno ya walimwengu.

Kuna siku hali ya ugumu ndio ilizidi alirudi home empty (kazini hakupata dili wala kaposho cha kikao).
Kukopa hataki (atalipa nini na hana mshahara?).

Kufika home akamshirikisha mkewe, mkewe akatoa jibu lile lile SINA HELA..!!!

Asubuhi ya siku ifuatayo ilifika aliwazaa akaona leo haendi kazini. Alimwacha mkewe aende dukani, John aliamua kufanya searching nyumba nzima.

Alikuta vifuatavyo:-

1. Kwenye begi la nguo lilikua limechanwa chini.
Alijiuliza begi jipya kuchanika..!! akakuta mule kwenye mchano Kuna vidonge vya uzazi na laki 3 kamili..!!!

2. Akainua godoro, kwa mwisho kwenye kono ya godoro akakuta kuna laki 5.

Akafanya searching kubwaa sanaa kwenye chumba chao cha kulala. Anakwambia alivyovigundua vilimfanya apate hasira hasaa.

Alitoka kwa hasira mpaka dukani kwa mkewe. Akamkuta mkewe anahudumia mteja, kuangalia simu akakuta haijajifunga (mkewe alikua akiangalia kitu YouTube)

John alizuga pale dukani akaiba ile simu akaenda kujificha ili aifanyie upekuzi.

Alivyoviona ........

1. Kumbe mkewe ana bwana ambae alikuaga mwanafunzi mwenzake chuo.

2. Na kwa kusoma sms, inaonyesha huyo jamaa ni X wa mke, na jamaa kapata Kazi mkoa huu huu tuliopo.

3. Mke wa John alimlipia jamaa kodi ya kuanzia maisha kazini na godoro alimnunulia.

3. Mke wa John anavyosemaga anaenda mjini kujumua vitu vya dukani huwa anashukia kwa mwamba ambacho ni chumba cha mke wa John na X..!!

4. Kwenye chatting ya WhatsApp inaonyesha X alimshauri mke wa John waache kutumia P2 ila mke awe anakula vidonge vya majira..!!!

Yaani John Ali screenshot kila chatting akajitumia WhatsApp.
Kwa kuonyesha ukatili hakufuta zile picha ili mkewe ajue kwamba John amejua.

Sasa haya yametokea Kati ya mwezi wa 4 mpaka wa 6.
John anasema anahitaji kuvunja ndoa.

Mke kuona John haitaki tena ndoa kakimbilia kanisani.
Mchungaji alimuita John, John alijibu "Mumewe huyo ni Michael (X)"

Mke akakimbilia kwa wazazi aombewe msamaha.
Wazazi wa mume na mke wamekaa, ila John anasema aliomba ili aelewe cha mtu basi yafanyike mazungumzo mengine na kwenye hayo mazungumzo Michael (X) awepo.

Ila Michael aligoma kabisaa kutimba kwenye usuluhishi na kwa taarifa ya mke pale alipokua anaishi Michael kahama na hajui kahamia wapi na namba za simu hazipatikani tena...!!!

John aligoma kumsikiliza yoyotee kwahiyo wazazi walisepa bila maelewano.

Nilichoshangaa sasa, anasema... Hajawahi kuongea na mtu juu ya hili ila Mimi kumuuliza mambo ya ku survive bila mshahara ndio kumemfanya animwagie yotee kama kushusha mzigo wa fikra..!!!

John haitaki tena ndoa na mpaka tunavyoongea hapa kasha file kesi ya talaka.

Kwake hajafika tokea mwezi wa 6 na nyumba haitaki tena.

John huenda kumchukua mwanae shule akitoka siku za Ijumaa huenda nae gheto lake jipya huku akimtaarifu mkewe "mtoto yupo kwangu".

Mshahara ulivyofunguliwa John kumbe kapanga chumba karibu kabisa na kwangu..!!

Kanunua vitu vichache vya kuanzia maisha.
Kaamua kumuachia mkewe nyumba tu aishi na mwanae.

Ye kaondoka na Shamba la Eka 10 na kiwanja chenye pagala..!! Hati ya nyumba kaacha kwa mkewe ye kaondoka na documents za kiwanja cha pagala na Shamba.

Kabla mahakama haijaamua John kashagawa mali na maisha yanasonga...!!!

Nilichofanya nilienda kupajua kwake alikopanga maana sasa Mimi ndio nimekua jirani yake..!!

Kwenye pagala lake anataka ajitahidi amalizie hata vyumba viwili ahamie maana maisha ya kupanga alishayasahau kabisaa.

TURUDI KWENU WANAUME WABISHI ......!!!!

Na hizi ndio ndoa zenu mnazokimbilia.

Mwamba alijifanya kupenda akamfungulia mpaka biashara kumbe POLE YAKE.

NIKIWAAMBIA MSIOE MUWE MNASIKIA.

Nani kakwambia kuwa wanakupenda?

Braza They love your wallet..!!

Huyu alimpenda John au alipenda pesa za John za kufungulia biashara??

Just hook with them halafu pita hivi kabla wallet haijaisha.

Ila man usisahau kuwezekeza kwenye Mali na akili (financial knowledge).

SECURE YOUR FINANCIAL FUTURE.

When You have ASSETS and FINANCIAL KNOWLEDGE, Then it's ENOUGH..!!!

PESA NDIO KILA KITU, Huoni ZILIVYOMUOKOA RAFIKI YANGU JOHN.

#YNWA
Kama hakuwa mmachame basi huyu jamaa ni wa kuhurumia. Kimsingi, hakuwa na mke bali mlaji. Maana hizo shinda ndizo zingewakomaza katika ndoa. Hata hivyo, huyo mama atalipa siku si nyingi.
 
My childs are enough kwel mkuu???

Inaonesha hujalelewa na wazazi wote ndo mana unaona childs are enough ila ngoja tukuache na mtazamo wako Mr Childs are enough!!!!
Yess they are real shit enough.

Kwa dunia ya sasa BINADAMU NI WAONGO SANA....

1. Wenye ndoa Wana nyumba ndogo Tena wengine zaidi ya moja.
Ana kula/liwa na huyu halafu usiku uleule uchi anampelekea mkewe/mumewe.

2. Hata wewe nikikwambia unaletee ndoa zenye matatizo, utaniletea nyingii za mtaani kwenu na kwa wanaokuzunguka.

3. Raia Hawana amani kabisa ndani ya ndoa. Wanandoa wanaishi kama misukule kabisaa ndani ya ndoa.
Utasikia, ndoa sitaki ila nalea wanangu tu..!!!

4. Kazini wenye ndoa wanaliwa na kula vya watu, mtaani kila siku kufumaniwa.
Ila dip down kwasababu nyumbani/ndoani wamekosa kitu Bora wavitafute nje.

Aisee ndoa zimejaaa Majanga tu siku hizi.

Unajua ndoa nyingi sanaa zinatalaka japo hazijasajiliwa mahakamani?
Wenza kulala vyumba tofauti, sio talaka hii?

Mwanaume analea watoto sio wake..!!

Na akiona gumu utasikia "Kitanda hakizai haramu"

Je ni kweli KITANDA HAKIZAI HARAMU..!!!

#YNWA
 
Matajiri duniani wapo single ila abdallah wa MWANANYAMALA anaongeza mke mwengine.

HIVI NI KWANINI?

#YNWA

Unaargue kwa kigezo cha matajiri
Ongelea kwnye jamii inayokuzunguka achana na wakina Jeff mkuu

Kwanini Abdullah asiongeze mke kama ndo kitu kinachompa furaha
Embu acha watu waowane na kuolewa usitusumbue tafadhali
 
Yess they are real shit enough.

Kwa dunia ya sasa BINADAMU NI WAONGO SANA....

1. Wenye ndoa Wana nyumba ndogo Tena wengine zaidi ya moja.
Ana kula/liwa na huyu halafu usiku uleule uchi anampelekea mkewe/mumewe.

2. Hata wewe nikikwambia unaletee ndoa zenye matatizo, utaniletea nyingii za mtaani kwenu na kwa wanaokuzunguka.

3. Raia Hawana amani kabisa ndani ya ndoa. Wanandoa wanaishi kama misukule kabisaa ndani ya ndoa.
Utasikia, ndoa sitaki ila nalea wanangu tu..!!!

4. Kazini wenye ndoa wanaliwa na kula vya watu, mtaani kila siku kufumaniwa.
Ila dip down kwasababu nyumbani/ndoani wamekosa kitu Bora wavitafute nje.

Aisee ndoa zimejaaa Majanga tu siku hizi.

Unajua ndoa nyingi sanaa zinatalaka japo hazijasajiliwa mahakamani?
Wenza kulala vyumba tofauti, sio talaka hii?

Mwanaume analea watoto sio wake..!!

Na akiona gumu utasikia "Kitanda hakizai haramu"

Je ni kweli KITANDA HAKIZAI HARAMU..!!!

#YNWA

Una negative perspectives nyingi kuliko positive.
Kila kitu kwenye maisha kina negatives zake.
Hata urais una negative effects nyingi mno.
Lakini nchi haiwez kukosa rais eti kisa kuna rushwa na upigwaji mwingi.
Tatizo unatafuta mtu perfect ukizani wapogo duniani.
Subiri tufe mkuu ukaoe malaika huko.
 
Tatizo wanawake ni watu wachoyo sana, walafi mno, wana tamaa sana, roho mbaya, wana chuki, wabinafsi, watu wenye mashindano, wasiotulia, wachawi, wasiowafikiria wengine Na ndoa ni biashara kwao
Kama wewe ni mwanaume kweli, I mean rijali basi kuna nati imechomoka[emoji848]
 
Back
Top Bottom