Kimsingi hizi rates wanazotoa bank zote siyo kwamba hiyo pesa unaipata kama ilivyo; NO.
Kwa mfano CRDB watakwambia utapata 9% kwa mfano, lakini kama mwezi unaishia tarehe 28, au 30 au 31 pesa utakayopata ni tofauti sana. Tatizo kwenye ile 10% ya kodi watakata ya 9%.
Nitakupatieni mifano hapa: Mimi nilimwekea kijana wangu wa kwanza 100M, kwa rate ya 9% kwa miaka 3, ambapo ilibidi kila mwezi nipate 750,000/= lakini sasa baadhi ya miezi inaingia 739,000/= wakati mwingine 750,000/= wakati mwingine 755,000/= lakini kwenye makato wanataka 76,000/= kila pesa inapoingia.
Kwa hiyo kuna wakati unajikuta unapata 670,000/= kama faida ya mwezi hapa wakianza tena makato yao unabakia na 665,000/=
Kwa hiyo uwekezaji wa bank ni security tu siyo business; this goes to UTT-Amis as well.