Okay asante ntafanyia kazi na maswali mengi ya kuuliza i have to go.Watu binafsi wanapokea ndio na kima cha chini inategemeana na mnada wa hisa zao kwa wakti huo. Ila hata 500k unaweza kuweka ingawa return itakuwa ndogo sana labda uwe unafanya kama uwekezaji wa muda mrefu sana.
Kila ijumaa wanatoa seminar kwa wanaohitaji kufahamu mambo ya uwekezaji kwenye hati fungani zao,kawasikilize mkuu.
Hio 10M umeiweka kwa muda gani?Nimeweka UTT tokea mwaka Jana mwezi wa 9. Nakula elfu 88 kila mwezi kwa niliyoweka 10m.
Hapana NMB ni wahuni walichoweka kwenye fixed calculator yao na uhalisia ni vitu viwili tofautiNMB fixed deposit intest 9.5% , una swali jingine?
Calculator yao ipoje mkuu tupate maarifa.Hapana NMB ni wahuni walichoweka kwenye fixed calculator yao na uhalisia ni vitu viwili tofauti
Hakuna mtu anakataa weka ushahidi watu wanatafuta profit sio ubishaninilicho gundua humu ndani kuna watu wako nyuma sana kwenye masuala haya ya Fixed deposit account/fixed deposit reserve (fdr)
kuna kampuni zinapewa rates za 10% mpaka 11% ama 11.5 % tena kwa miezi mitatu tuu (3)
sasa kuna mshamba mmoja ata toka uko na povu kukataa hili!..
Ukicheki calculator yao riba inasoma 9.5 ila ukienda kuweka unaletewa risiti inasoma 5 au 6 percent… ukilalamika wanakupa semina ooh hii imekosewa mara hii sio riba ya fixed kuna sijui uwekezaji wa maisha , kimsingi maelezo yao hayaelewekiCalculator yao ipoje mkuu tupate maarifa.
Kimsingi hizi rates wanazotoa bank zote siyo kwamba hiyo pesa unaipata kama ilivyo; NO.
Kwa mfano CRDB watakwambia utapata 9% kwa mfano, lakini kama mwezi unaishia tarehe 28, au 30 au 31 pesa utakayopata ni tofauti sana. Tatizo kwenye ile 10% ya kodi watakata ya 9%.
Nitakupatieni mifano hapa: Mimi nilimwekea kijana wangu wa kwanza 100M, kwa rate ya 9% kwa miaka 3, ambapo ilibidi kila mwezi nipate 750,000/= lakini sasa baadhi ya miezi inaingia 739,000/= wakati mwingine 750,000/= wakati mwingine 755,000/= lakini kwenye makato wanataka 76,000/= kila pesa inapoingia.
Kwa hiyo kuna wakati unajikuta unapata 670,000/= kama faida ya mwezi hapa wakianza tena makato yao unabakia na 665,000/=
Kwa hiyo uwekezaji wa bank ni security tu siyo business; this goes to UTT-Amis as well.
Ila jamani tupo tofauti mtu milioni kumi uweke bank upewe riba hata haizid laki kwa mwezi....Mimi huyu na bangi zang za chuga kabisa hata nipewe laki kwa milioni mbili sikubali abadani
Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
Hio 10M umeiweka kwa muda gani?
Aiseee[emoji28][emoji28][emoji28][emoji28] Mil 10 mtaji unapata Elfu 88 maana akee ni 3000 kwa sikuu.. kwa mtaji wa mil 10???? Ilaa hata kama ni Uogaa huu umezidii mkuuu... Tokaa kwenye hicho kifungo cha kuogopa kupotezaa helaaaaa...Nimeweka UTT tokea mwaka Jana mwezi wa 9. Nakula elfu 88 kila mwezi kwa niliyoweka 10m.
Hamna mtaji wala hela inayoongezeka ni ufinyu tu wa maarifa yako ya maswala ya fedha ndio inakufanya uone hivyo,Uki weka hiyo 100M kwa malipo ya 750K kila mwezi-hiyo unayolipwa ni thamani ya kiasi ambacho hela yako inapoteza thamani kila siku ikiwepo huko.Kwa hela hiyo UTT ungepata 883,390/= kila mwezi bila makato plus mtaji wako unaongezeka taratiibu. Kupanga ni kuchagua[emoji2957]
SahihiKama lengo ni riba nzuri weka UTT.
Utawekezaje sehemu ambayo mtaji wako unapoteza thamani mara 3 unachokipata kwa mwezi? Au una maanisha akishakuwa bilioneya hatajali mtaji wake kushuka thamani?Inflation rate ya Tanzania kwa mwezi ni wastani ni 4.0% huku hiyo riba ni 0.5-1% kwa mwezi,so obviously kila siku hela yako inashuka thamani zaidi.kwa lugha nyingine uwekezaji wako unapoteza thamani mara 3 zaidi ya unachokipata katika mwezi.
Kwa kijana ambaye unaweza kutumia hicho kiasi ukahangaika ni mara 100, ufanye hivyo kisha ukipata fedha nyingi kama faida katika biashara ndio uwekeze huko.
Huku inachezwa bei ya vipande Mf leo kianauzwa say 250 baada ya wiki mbili ni 252 hivyo thamani ya hela yako inabadilika kutokana na bei ya hiki kipande.Hivyo fix riba sio rahisi ila labda mwisho wa siku ina range kati ya 10 - 12 au zaidi kidogo kwa uzoefu wangu wa miaka kadhaa na hawa utt(liquid).UTT riba ni 10% kwa mwaka fixed ,kwa mtu wa 10M kwa mwez gawio linacheza kati ya 83,000/- hapo cash kwa mwaka ni 1M gawio
Aiseee[emoji28][emoji28][emoji28][emoji28] Mil 10 mtaji unapata Elfu 88 maana akee ni 3000 kwa sikuu.. kwa mtaji wa mil 10???? Ilaa hata kama ni Uogaa huu umezidii mkuuu... Tokaa kwenye hicho kifungo cha kuogopa kupotezaa helaaaaa...