Nikiweka fixed deposit 10M naweza kulipwa kiasi gani na bank kila mwezi?

biashara mtandao
 
Hesabu za matikiti hizi [emoji3]
 
Mkuu unaweza kufafanua vyema hizo biashara wengine tunataman kuzifanya hizo mishe
Asante
 
Nenda utt weka kwenye mfuko wa liquidy fund unaweza pata kuanzia 70000 mpaka laki na usheee kwa mwezi na hela unaweza kutoa wakati wowote unaotaka ndani ya siku tatu hela inakuwa kwenye akaunti yako, achana na fixed deposity za benk mkui
Hii UTT ni nini wakuu?
Tupeane elimu kidogo hapa

Sent from my TECNO PR651H using JamiiForums mobile app
 
Nenda utt weka kwenye mfuko wa liquidy fund unaweza pata kuanzia 70000 mpaka laki na usheee kwa mwezi na hela unaweza kutoa wakati wowote unaotaka ndani ya siku tatu hela inakuwa kwenye akaunti yako, achana na fixed deposity za benk mkui
Ushauri mzuri sana utt pesa yako haipotei na kila siku wanakuwekea faida yako Wana mobile app yao. Muda wowote unatoa siku 3 tu unachukuwa mzigo wako wote. Ni sehemu sahihi kuliko bank especially mfuko wa liquid
 
Mzee wa punyeto
 
Wataalamu wa bank je naweza kuweka deposit kiasi cha hela kama 10m halafu kila mwezi bank inanilipa riba? Na je watanilipa kiasi gani kila mwezi? Wakati huo hela yangu ipo tu bank ?
Kwanini uweke kiasi kingi hivyo cha hela Bank? Huko utapata faida kama ya 1% kila mwezi au 10% kwa mwaka, ambayo naamini kama ukiwekeza hiyo hela kwenye uwekezezaji wowote mzuri unaweza kupata hela zaidi ya hiyo. Nenda hata maeneo mapya ambayo yameshakuwa ya uswahili kutokana na population ya watu kuongezeka, nunua kiwanja hata kwa 1M kisha jenga vyumba viwili, sebule, jiko na choo ndani kisha pangisha huwezi kukosa 200,000 au zaidi kwa mwezi na bado utakuwa na nyumba. Biashara zipo nyingi za kufanya kukuingizia kipato kikubwa hadi 1M kwa mwezi kwa hela hiyo. Wekeza, wekeza, wekeza na sio kuweka akiba!!
 
una wazo zuri sana
...boda moja ni wastani wa 2.6m hadi 3.15m kwa 125cc na 150cc boxer na Tvs ambazo ndo ziko kwenye chati,so anapata boda 3 za uhakika na inayobaki anatia kwenye viepe.
Shida ni kutokuwa tayar kupambana na changamoto za marejesho kwa vijana i.e kukosa muda wa kufatilia na umakini katika mahesabu(madeni n.k)
Kiujumla..ukipata vijana waaminifu na wenye kujitambua ni biashara inayolipa sana,binafsi naifanya mwaka wa nne sasa.

Sent from my SM-N975U using JamiiForums mobile app
 
UTT tu ndo wana riba nzuri kuliko mabank kwa wanaotaka kuweka hela zao tu na hawana mpango na biashara….
Na ukitaka hela yako ni 3working days unapata chap, mim naprefer zaidi UTT kuliko fixed account za bank
 
Mkuu biashara ya boda boda anae pata faida ni dereva. Twende taratibu utanielewa. Tufanye umenunua piki piki hadi inaingia barabarani umetumia 2.5m ,hesabu kwa siku elfu 10 kwa mwezi laki tatu kwa mwaka hadi mkataba unaisha utakua umeingiza 3.6m .sasa toa gharama uliyo nunulia hiyo piki piki una baki na 1.1m , Gawanya hiyo pesa kwa miez 12 uone kwa mwezi unapata kiasi gani na ukipata kwa mwezi gawa kwa siku 30 uone kwa siku moja unapata kiasi gani. Hapo utajua wewe uliye wekeza 2.5m na dada anae saidia mama ntilie na kulipwa buku 3 mpo sawa
 
Wataalamu wa bank je naweza kuweka deposit kiasi cha hela kama 10m halafu kila mwezi bank inanilipa riba? Na je watanilipa kiasi gani kila mwezi? Wakati huo hela yangu ipo tu bank ?
Bunge la Tulia litakupa majibu.
 
Biashara Sio kwa ajili ya Kila mtu.
Biashara uendana na nyota
Nyie ndio ambao hufungua biashara na kuweka vibahasha vya kiganga au stika za manabii.

Kanuni za biashara brother ni rahisi sana wala sio za business school.
Amini nilikuwa kama wewe huu mwaka wa nne toka nijiingize kwenye mabiashara tofauti tofauti hadi natamani kuacha kazi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…