Niko njia panda msaada

Niko njia panda msaada

Pole mkuu Ila ninachokiona unampenda sana mkeo kiasi kwamba hata akikuosea huwa unatafuta point za kuhalalisha makosa yake.

Ila itabidi ukubali kuwa mkeo hakuoni jinsi unavyomuona na pengine alikuwa na mpango wa kuachana na wewe ndio maana alibeba ujauzito huku card za clinic zikiwa na jina la mwenye ujauzito wake kwa sababu anampa haki hiyo kwenye manisha yake pasipo kufikiria atakuumiza au kukufedhehesha kiasi gani.

Kwenye ndoa nishawahi kuona matukio mabaya zaidi ya hilo na watu hawakuachana. Kwa hiyo naamini ni wewe wa kaamna, kulitesekea penzi kwa kuwa wa ziada kwa mkeo au ujiweke huru... Uamuzi ni wako
 
Hivi kweli,ikiwa ni wewe. Namba 4 hapo. Unaweza? Hiyo ni zaidi ya dhalau. Bora achepuke tu utasamehe,japo kauli kupenda,haipo. Huko ni kujitia uzuzu bure tu. Mpaka anamzalia mtu,ni ile unaambiwa,nipo kwake kimwili tu. Sasa,huyo wa nini?

Hii simpo. Mpaka anajifungua,bado siku chache sana. Hizo zivumilie. Kikubwa tunza hiyo namba.
Kwao,ikifika siku,mpeleke tu. Nauli toa,lakini usimuache na chochote. Na hapo hapo,kama wazazi wapo,ongea nao,na ushahidi uliopo wape. Akizaa poa. Akijifungua,sawa. Kadi ya kliniki haipo mbali,ukitaka ipige kopi,uende nayo ukweni. Mwambie atoe origino. Akigoma,toa kopi.
Mahakama ina uwezo wa kuziomba kampuni za mitandao kutoa mawasiliano ya mtu na mtu. Wambie hilo wasiwe na wasiwasi,utaghalamia. Ye mwenyewe ataamua.

Akikataa,thibitisha. Akikubali,achana nae. Ukute ulikuwa unaogea taulo alilojifutia mwenzio.
Katika kumshauri mtu usipende kumwambia jinsi unavyotaka kufanya wewe, mpambanulie na mwachie aamue mwenyewe. Ndivyo nilivyojifunza kwenye counselling. Actually, mtu anapoomba ushauri hataki umwambie aamue vipi, uamuzi anao mwenyewe. Anachotaka ni kupambanuliwa (kama kuweka kalata mezani) ili aweze kuchagua afanye nini.
 
Katika kumshauri mtu usipende kumwambia jinsi unavyotaka kufanya wewe, mpambanulie na mwachie aamue mwenyewe. Ndivyo nilivyojifunza kwenye counselling. Actually, mtu anapoomba ushauri hataki umwambie aamue vipi, uamuzi anao mwenyewe. Anachotaka ni kupambanuliwa (kama kuweka kalata mezani) ili aweze kuchagua afanye nini.



Absolute

Ushauri huwa unalenga kumpa maana ya ndani ili mshauriwa afanye maamuzi ya busara zaidi.

Ndo maana huwa nasema sio kila MTU anaweza kutoa ushauri .

Mimi comment yangu nimeifuta baada ya mtoa mada kusema this is fiction story from Facebook.
 
1. Mimi ningeshauri kwa sasa ungekaa kimya na umpeleke kwao kama anavyodai.
2. Baada ya kujifungua, akishapata nguvu, ongea naye na onyesha kwamba una mashaka na uhusiano wenu, hasa kwamba una hakika anachepuka na mtu unayemfahamu.
3. Ona mwenyewe kama unaweza kuvumilia hali hiyo (mtu mwingine asikuingizie mawazo yake).
4. Kama unampenda, samehe na endelea kuishi naye kama mkeo.
5. Katika masuala kama haya, kama hatua ya kwanza, usimhusishe mtu mwingine/ndugu/wazazi - kufanya vikao etc - jadilini mkiwa wawili tu.
5. Pole sana kwa yote.
Kuanzia hapo no 4 na 5 umepuyanga aisee,hivi unaanzaje kuishi na mwanamke wa hivyo?,hata kama unampenda
 
Pole sana kiongozi, hakika Una busara na hekima ya Hali ya juu. Tafuta ushahidi wa kutosha. Mpeleke akajifungue, baada ya wiki nenda kwao na ushahidi wote Kisha mchakato wa talaka uanze. Huyu huwezi kuishi nae kama mke tena kwenye ulimwengu huu.
Ingekua ni mimi mpaka huyo first born ningemkana aisee,ningesema hata huyu siamini kama ni wa kwangu
 
Mmh! Pole sana, huu ni wakati wako wa kuonyesha umekomaa kiakili na una msimamo,
Hata kuandika hivi umejitahidi sana, Mungu akutie nguvu kulimaliza hili katu usikubali kujimaliza.
 
Kuanzia hapo no 4 na 5 umepuyanga aisee,hivi unaanzaje kuishi na mwanamke wa hivyo?,hata kama unampenda
Nimetoa ushauri. Wewe ungetaka nimwambie ambavyo ningeamua. Kushauri ni tofauti na kumwambia mtu uamuzi wako kwa suala ambalo si lako. Mimi nimefuata principles za counselling, wewe unasema from the point of view of a layperson. Hivyo, lazima uone kwamba nimepunyanga maana siyo area yako hii.
 
Boss:

1 Unaweza ukamsamehe ukaendelea kuishi naye lakini Kila ukikumbuka alimvulia mwanaume mwenzako nguo na kupewa mimba juu na kuzaa kabisa.Na mbaya zaidi watoto unawaona hawa hapa.Utazidiwa na hisia na mwisho utajenga chuki ambayo itakutesa Kila siku ya maisha yako na hapo shetani anaweza chukua point kukushauri ujiue au ufanye jambo lolote baya.Kwa hiyo ni suala jema kuvunja ndoa na kufocus na mambo mengine.

2 Msubirie azae BIla kumwonesha reaction YEYOTE Ili watoto wasije wakapata shida tumboni. akishazaa ibua aliyokuwa anayafanya pindi yupo Kwa wazazi wake na kuachana naye.

3 Yesu(Mungu) mwenyewe anakataa talaka ila kwenye ishu kama hii alitoa ruhusa.

Mathayo 19:8-10

8 Yesu akajibu, “Musa aliwaruhusu kuwataliki wake zenu kwa sababu mlikataa kupokea mafundisho ya Mungu. Lakini talaka haikuruhusiwa hapo mwanzo. 9 Ninawaambia kuwa, kila anayemtaliki mke wake, isipokuwa kutokana na uzinzi, na akamwoa mwanamke mwingine, anazini.”
 
Una utulivu sana Hadi umeweza kuandika vizuri!, ninachokushauri chukua huo ushahidi ulioupata then kwakuwa ni mjamzito na alisema anataka kwenda kwao basi muache aende, baada ya yeye kwenda kaa Kwa kutulia jipe utulivu wa akili na ujiulize maswali wewe mwenyewe kama unaweza kuendelea nae?, utapata jibu la kiume humo.

Maamuzi yako sasa yatategemea, yeye asirudi kwako na abakie huko huko au arudi...ukiamua asirudi basi asirudi kweli au ukiamua kurudi pia it's okay.
 
Back
Top Bottom