Niko njia panda msaada

Niko njia panda msaada

Duh! Wewe mvumilivu sana shehe, Kutokana na hilo nashauri uendelee nae tu maana wewe ndo unamfaa huku street saahii angekuwa Mloga na tumbo lake

Bila kusahau toka hapo njiapanda.
 
Piga picha message zote Kwa ushahidi asifute, mpekele kwako hata kesho usimuache hapo
 
Kama ni kweli pole sana; kwa sasa usimwambie chochote bali pambana arudi kwao akajifungue.
Baada ya kujifungua mueleze yeye na wazazi wake ukweli, kisha vunja ndoa tafuta mwanamke mwingine.
 
Kama Hadi dakika hii unaongea hujafanya mauaji au kujeruhi blaza unastahili PhD ya uvumilivu...mi nahis ningeshampiga Hadi atapike hao watoto
 
Peleka huyo Mwanamke kujifungua kwao.
Peleka Mtoto kupima DNA...!

Kwa Ushahidi ulionao sijui hata ulikua na sababu ya kuomba Ushauri...!

Wanawake ni Wabinafsi hafu ni Washenzi Mkuu, pia hawana huruma, wanatumia Hisia kufikiri, Akili wanatumia tu wakitaka kuvukia Barabara ama wanapokua SHULE...!

Kama ni kweli... Huyo sio Mke wako.... !
 
FB_IMG_1719557793598.jpg
 
Pole... Kusanya ushahid wa ktosha, peleka kwao Kam anavotaka, akjfngua akikaa saw kla ktu ktaishia hko kwao. Hyo yupo hapo Kwako kwa masilah yake tu.
 
Haya maisha haya!halafu utashangaa mchungaji sijui padri anakuambia kilichounganishwa na Mungu binadamu asikitenganishe!!

Man pole sana man!

Mpeleke kwao Kwa amani!ukifika waambie wazazi wake ukweli wote na useme naogopa nisije nikamuua Kwa hasira ndio maana nimemrudisha Kwa amani tu!
 
Kusanya ushahidi wa kutosha halafu baada ya hapo mpe mkono wa kwakheri 🤔😡
 
Kama ni kweli basi kuna watu wanajua kupiga dhambi za masafa marefu daah
 
Maisha ni mtihani,wewe ni jasiri piga moyo konde. Jipe muda kwa sasa ona hayo maumivu unastahili. Ukihisi sasa umepona kaa mzungumze ila kwa sasa usifanye maamuzi yoyote.
 
NJIAPANDA: Mke wangu alileta mchepuko wake kwangu wiki mbili wakitafuta mtoto, sasa anakaribia kujifungua!

Sina kawaida ya kushika simu ya mke wangu kwani nilikuwa namuamini kiasi kwamba sijawahi hata kufikiria kama atakuja kunisaliti. Nimeoa na ndoa yangu ina miaka 3 sasa, na Mungu ametujalia mtoto mmoja. Sasa hivi mke wangu ni mjamzito na ana mapacha wawili tumboni.

Wiki mbili zilizopita niliona kama mke wangu amebadilika. Alikuwa hana raha na kila nikitaka kuongea naye, anakuwa mkali, na hata kunifokea hadi kunitukana mbele za watu. Mimi nilijua ni ujauzito kwani ana mimba ya miezi nane, hivyo nilijishusha na kukaa kimya.

Lakini kuna kitu kilinichanganya, alikuwa karibu sana na simu yake. Alikuwa bize nayo kiasi kwamba hata chakula alikuwa hali. Ilionekana kama kuna mtu anachati naye. Kilichonishtua zaidi ni kwamba hakutaka mtu kugusa simu yake, hata mtoto akigusa simu, anakuwa mkali, anatukana hadi basi.

Mimi password yake nilijua muda mrefu, ila sikujisumbua naye kwani alijua siijui. Nilipoona mabadiliko, nikaamua kufuatilia kujua ni nini. Nikakuta analalamika kwenye meseji nyingi tu anazotuma kwa mtu mmoja, ambaye hajahifadhiwa kwenye simu. Mwanzoni, meseji zilikuwa zinazungumzia mambo ya ujauzito, baadhi zilikuwa zimefutwa, lakini ni kama alikuwa anamwambia kuhusu watoto wake na mambo kibao, ikionyesha kuwa yeye ndiye baba wa watoto na walionysha kuwa vizuri sana.

Baadaye nikaona Mke wangu alikuwa analalamika, "Utambarikije ndoa na mke wako wakati uliniambia umemuacha? Kwanini uliniambia nibebe mimba kama ulikua na mpango wa kumuacha huyo mwanamke?" Mwanaume alikuwa hajibu, hivyo anatuma meseji tu zaidi ya mia mbili analalamika ila hajajibiwa.

Kwa kweli nilipaniki, nikaamua kufuatilia, nikagundua kuwa hata kadi ya kliniki sijaandikwa mimi kama baba wa mtoto, amemuandika huyo mtu ambaye nilipofuatilia ni mtu namjua. Alishawahi kuja mpaka kwangu kipindi fulani, akaniambia ni baba wa rafiki yake. Aliniomba huyo baba aje kulala kwangu kwa sababu alikuja yuko kwenye matibabu, mpaka rafiki ayke ananipigia simu kunishukuru, akakaa kwangu wiki mbili. Najua alikuwa anaenda hospitalini Muhimbili kumbe ndiyo walikuwa wanatafuta mtoto.

Kwa maana kuwa kumbe walishangaika kupata mtoto kwa muda mrefu kwa sababu mwanaume yuko mkoani. Mke wangu ndiye aliamua kumkaribisha nyumbani ili iwe rahisi kwake kubeba mimba, kwamba wakati mimi niko kazini wao wanahangaika kupata mtoto. Na kwa kweli nilipoangalia tarehe, zinalingana na kipindia licjhobeba mimba.

Sijamuuliza mke wangu kitu chochote, bado nipo kimya. Wiki ijayo ndiyo nampeleka kwao kwa ajili ya kujifungua kwani alisisitiza sana kuhusu mimi kumpeleka. Sasa najiuliza nifanye nini? Sina amani, sina raha, bado nimeshangaa. Hii mimba imenisumbua sana, amenitukana sana na kunidhalilisha sana, nilijua ni kisirani cha mimba kumbe hata si mimba yangu. Naomba ushauri, nifanye nini?
🤣🤣Hizi ndio zile stori za sungura na fisi zinaleta hadithi
 
Back
Top Bottom