Niko njia panda yenye maumivu moyoni: Biashara yangu imelala sana je, niende kwa mganga?

MGANGA ATANIRUDISHA KWELI KWENYE RELI.

INTRODUCTION:

Mimi ni mtumishi wa umma Ila pia nina ndoto za kuwa mfanyabiashara mkubwa sanaa...

Na nikiri NAPENDA HELA SAA.
Yaani ukitaka niwe na Amani basi laki kadhaa ziwe kwenye wallet yangu.

Katika kukimbiza ndoto zangu niliamua kufungua biashara ya vinywaji ya Jumla na rejareja (jina la mtaani tunaita Depo).

Nilikusanya mtaji nikiwa tayari nina idea na ilipofika mil 9 nikafungua depo.
Mil 6 bidhaa na mil 3 sunk cost kama kodi, Matengenezo frame na mengine yale ya maandalizi ya biashara.

Nauza vinywaji vyotee vikali na baridi, kwa jumla na reja reja, na kwasasa biashara yangu ina mtaji wa mil 25.

SCENARIO
Biashara ilianza vizurii mpaka nikawa nadata, yaani wateja walikuwa wengii.

Hawa wakani-force kukuza mtaji fasta mpaka kufika hizo mil 25.

Pia nikawa na vijana wa3 wa dukani, yaani ni fast delivery. Yaani mteja akikata tu simu basi bidhaa ipo mlangoni mwake.

Aisee nilipata jina fasta na kubwaa sanaa.

Mauzo yangu yalikuwa makubwa ya mil 3 Kwa siku na siku nisipouza yalikuwa hayashuki mil 1.

Kwasasa Nina Miaka kadhaa kwenye biashara (from July 2020).

Ila ndugu sasa biashara sielewi..

PROBLEM
Tokea January 2023 BIASHARA IMEKUWA NGUMU mnooo.

Mauzo mil 1 Tena jana ndio Majanga, nimefunga na laki 5..!!!

Pia hapa Nina miamala ya simu, na juzi (01/02) nililipwa commission ya 150k kwa mitandao yotee mi 4.

Wakati nilifika commison ya laki 5 kwa mitandao yote mi4.

Wateja simu sizioni, wakati Kuna kipindi walikua wanapiga simu mpaka saa 7 usiku kuniomba niwauzie bidhaa.

Hiyo saa 7 usiku watakukodia boda utakuja kufungua store utawauzia, wanakulipa na boda inakurudisha gheto kwa gharama zao.

Nina masters na bachelor ya mambo ya biashara, hivyo nimejaribu marketing skills kibao kama za kutuma sms kila asubuhi kuomba order kwa wateja, kupost status za WhatsApp ila 2023 bado ngumu kwenye biashara.

Sasa nimeshauriwa na raia NIENDE KWA MTAALAMU NIKAPIKWE.

Naambiwa, nilikua na nyota kalii hivyo competitor wameona waizime ili wao wauze.

DILEMA
Nimedata mwenzenu, ukicheki hii biashara ndio naitegemea kuwa ndio tobo la kunifanya nije kuachana na ajira za serikali ya CCM ila MBELE NAONA GIZA.

Nina mengi aisee siwezi kuandika yote, mfano: siku hizi nafungua saa 1 kamili asubuhi na kufunga saa 5 usiku.
Na hata kazini (halmashauri) nimepasusa naona pananichanganya tu (wiki yotee hii (Tokea 30/01)SIJAFIKA KAZINI.

KUHUSU VITABU-
Hivi vitabu sijui vya Robert koyasaki na wengine NIMESOMA SANAAA.
Tokea 2020 nishasoma vitabu kama 30 hivi vya mambo ya biashara na fedha na Robert Koyasaki pekee yake ni vitabu vi5 kuanzaia Rich Dad mpaka Money Quadrant.

Vingi vinazungumzia "Kwenye financial world Usikate tamaa, pambana"" ila nahisi Kuna kamba ipo nyuma ya mapambano yangu inanivuta nyuma.

NAPAMBANA NYIE...
1. Muda wote duka nalifanya safi
2. Rangi zinavutia (mashelf na ukuta)
3. Kama elimu, Nina degree mbili za biashara (bachelor + masters)
4. Kama ni experince, nishauza sanaa biashara za watu Tena bila mshahara (kipindi najifunza biashara)
5. Kama ni ukarimu, basi ni mkarimu sanaa. Humu Kuna watu wawili tulishaongea sanaa Japo kwa simu (kama wako comfortable wanaweza thibitisha hapa).

Kifupi nafanya mengii ila 2023 imekua ngumu.
Imefikia mpaka kupunguza wafanyakazi dukani kutoka 3 mpaka 1..!!!

Na kilichonifanya nipost ni baada ya commision kushuka kutoka 500k mpak 150k kwa Jauary/2023.

Huwezi amini:-
Jumapili ya wiki hii sikufungua, ili tu nione upepo wa wateja, ila chakusangaza mpaka unaingia usiku sijapokea simu hata ya mteja mmoja kulalamika "Mbona nimefunga"

Kwasasa sijui si-exist kwenye phone book zao..!! Niko kudata balaaa yaani waliokuwa wakinipigia simu usiku nao hawapigi hata mchana..!!!

Kazini sijaenda wiki maana kichwa ni cha moto balaaa.

Nipeni mawazo wajasiliamali wenzangu.
Nipeni mawazo wafanyabiashara wenzangu.

Nishapitia msoto mkubwa sanaa kwenye maisha ya uyatima, kazini, kwenye ujana wangu ila Jambo gumu linapogusa biashara NADATA KABISAAAA.

Nahitaji kuacha Kazi na hili ndio TOBO LANGU.

MGANGA ATANIRUDISHA KWELI KWENYE RELI?

#YNWA
Suala la Commission ya miamala nadhani ni kupungua kwa mzunguko januari hii
 
Tuliza akili acha ujinga January hii biashara imekuwa mbaya zaid ya kawaida kwa kila mtu

Mimi na biashara kubwa na maarufu sana hapa dar duka langu linafurikaga wateja muda wote

Ila January hii mauzo yamekuwa yaa ajabu kuliko kawaida

Jana tra wamekuja dukan sijatoa risit siku tatu mfululizo nikawaambia hali mbaya siuzi hawaamin nikwaambia kaen hapo
Wakakaa nusu saa amna mteja wakachoka " yaan wewe ..... huuuzi sasa wengine watakuwa na hali gan?"

Hali ni mbaya kuliko kwaida kuna upepo mbaya unapita tulia acha wenge
 
Dec nikikuwa najaza wateja mpk wengine wanakaa nje wanasubir ila January naweza kaa masaa mawili hajaingia mtu tuliza wenge utaharibu ni kipind cha mpito
 
Tuliza akili acha ujinga January hii biashara imekuwa mbaya zaid ya kawaida kwa kila mtu

Mimi na biashara kubwa na maarufu sana hapa dar duka langu linafurikaga wateja muda wote

Ila January hii mauzo yamekuwa yaa ajabu kuliko kawaida

Jana tra wamekuja dukan sijatoa risit siku tatu mfululizo nikawaambia hali mbaya siuzi hawaamin nikwaambia kaen hapo
Wakakaa nusu saa amna mteja wakachoka " yaan wewe ..... huuuzi sasa wengine watakuwa na hali gan?"

Hali ni mbaya kuliko kwaida kuna upepo mbaya unapita tulia acha wenge

Thanks.
The words from Legend..!!

#YNWA
 
Labda ukioa utafanikiwa mkuu embu oa wanawake wana ridhiki zao
 
Huko ulipoenda kufanya uzinifu ndo umeenda kuzoa mabalaa na nuksi ..Kaa kwa kutulia !!

Badili mienendo na tabia zako kama mchawi ni wewe umajiroga .
 
Nani amekwambia kuwa nimetoka kuzini?

Stop personal attacks.

Turudi kwenye mada...

#YNWA
 
Ukienda kwa huyo mchawi unayemuita mtaalamu utazikwa ukiwa lofa.
Biashara yako haijayumba Bali akili zako zimekuza sana tatizo.
Bado unatengeneza faida, mtaji bado upo na kuyumba ni kwa siku chache tu.
Unasema unataka kuwa tajiri, sahau kuwa tajiri ikiwa unayumba kwa vitu vidogo kama hivi. Unaitaji kuwa jasiri mwenye roho ngumu na usiyekata tamaa hili uwe tajiri.
Matajiri hawana moyo wa kizembe kama wako.
Kilichotokea kwako ni mabadiliko ya kawaida kwenye biashara zako, na mabadiliko haya hutokea kwenye biashara zote.
Wateja walikuwa wanashughulikia ulipaji wa ada, pango na madeni yaliyokopwa wkt wa sikukuu, wasingefikiria ulevi ikiwa hawajafanya mambo muhimu.
Usiende kwa huyo mchawi, kaza buti, badili fikra, soma mazingira ya sasa hapo ulipo kisha funga mkanda songa mbele.
 
MGANGA ATANIRUDISHA KWELI KWENYE RELI.

INTRODUCTION:

Mimi ni mtumishi wa umma Ila pia nina ndoto za kuwa mfanyabiashara mkubwa sanaa...

Na nikiri NAPENDA HELA SAA.
Yaani ukitaka niwe na Amani basi laki kadhaa ziwe kwenye wallet yangu.

Katika kukimbiza ndoto zangu niliamua kufungua biashara ya vinywaji ya Jumla na rejareja (jina la mtaani tunaita Depo).

Nilikusanya mtaji nikiwa tayari nina idea na ilipofika mil 9 nikafungua depo.
Mil 6 bidhaa na mil 3 sunk cost kama kodi, Matengenezo frame na mengine yale ya maandalizi ya biashara.

Nauza vinywaji vyotee vikali na baridi, kwa jumla na reja reja, na kwasasa biashara yangu ina mtaji wa mil 25.

SCENARIO
Biashara ilianza vizurii mpaka nikawa nadata, yaani wateja walikuwa wengii.

Hawa wakani-force kukuza mtaji fasta mpaka kufika hizo mil 25.

Pia nikawa na vijana wa3 wa dukani, yaani ni fast delivery. Yaani mteja akikata tu simu basi bidhaa ipo mlangoni mwake.

Aisee nilipata jina fasta na kubwaa sanaa.

Mauzo yangu yalikuwa makubwa ya mil 3 Kwa siku na siku nisipouza yalikuwa hayashuki mil 1.

Kwasasa Nina Miaka kadhaa kwenye biashara (from July 2020).

Ila ndugu sasa biashara sielewi..

PROBLEM
Tokea January 2023 BIASHARA IMEKUWA NGUMU mnooo.

Mauzo mil 1 Tena jana ndio Majanga, nimefunga na laki 5..!!!

Pia hapa Nina miamala ya simu, na juzi (01/02) nililipwa commission ya 150k kwa mitandao yotee mi 4.

Wakati nilifika commison ya laki 5 kwa mitandao yote mi4.

Wateja simu sizioni, wakati Kuna kipindi walikua wanapiga simu mpaka saa 7 usiku kuniomba niwauzie bidhaa.

Hiyo saa 7 usiku watakukodia boda utakuja kufungua store utawauzia, wanakulipa na boda inakurudisha gheto kwa gharama zao.

Nina masters na bachelor ya mambo ya biashara, hivyo nimejaribu marketing skills kibao kama za kutuma sms kila asubuhi kuomba order kwa wateja, kupost status za WhatsApp ila 2023 bado ngumu kwenye biashara.

Sasa nimeshauriwa na raia NIENDE KWA MTAALAMU NIKAPIKWE.

Naambiwa, nilikua na nyota kalii hivyo competitor wameona waizime ili wao wauze.

DILEMA
Nimedata mwenzenu, ukicheki hii biashara ndio naitegemea kuwa ndio tobo la kunifanya nije kuachana na ajira za serikali ya CCM ila MBELE NAONA GIZA.

Nina mengi aisee siwezi kuandika yote, mfano: siku hizi nafungua saa 1 kamili asubuhi na kufunga saa 5 usiku.
Na hata kazini (halmashauri) nimepasusa naona pananichanganya tu (wiki yotee hii (Tokea 30/01)SIJAFIKA KAZINI.

KUHUSU VITABU-
Hivi vitabu sijui vya Robert koyasaki na wengine NIMESOMA SANAAA.
Tokea 2020 nishasoma vitabu kama 30 hivi vya mambo ya biashara na fedha na Robert Koyasaki pekee yake ni vitabu vi5 kuanzaia Rich Dad mpaka Money Quadrant.

Vingi vinazungumzia "Kwenye financial world Usikate tamaa, pambana"" ila nahisi Kuna kamba ipo nyuma ya mapambano yangu inanivuta nyuma.

NAPAMBANA NYIE...
1. Muda wote duka nalifanya safi
2. Rangi zinavutia (mashelf na ukuta)
3. Kama elimu, Nina degree mbili za biashara (bachelor + masters)
4. Kama ni experince, nishauza sanaa biashara za watu Tena bila mshahara (kipindi najifunza biashara)
5. Kama ni ukarimu, basi ni mkarimu sanaa. Humu Kuna watu wawili tulishaongea sanaa Japo kwa simu (kama wako comfortable wanaweza thibitisha hapa).

Kifupi nafanya mengii ila 2023 imekua ngumu.
Imefikia mpaka kupunguza wafanyakazi dukani kutoka 3 mpaka 1..!!!

Na kilichonifanya nipost ni baada ya commision kushuka kutoka 500k mpak 150k kwa Jauary/2023.

Huwezi amini:-
Jumapili ya wiki hii sikufungua, ili tu nione upepo wa wateja, ila chakusangaza mpaka unaingia usiku sijapokea simu hata ya mteja mmoja kulalamika "Mbona nimefunga"

Kwasasa sijui si-exist kwenye phone book zao..!! Niko kudata balaaa yaani waliokuwa wakinipigia simu usiku nao hawapigi hata mchana..!!!

Kazini sijaenda wiki maana kichwa ni cha moto balaaa.

Nipeni mawazo wajasiliamali wenzangu.
Nipeni mawazo wafanyabiashara wenzangu.

Nishapitia msoto mkubwa sanaa kwenye maisha ya uyatima, kazini, kwenye ujana wangu ila Jambo gumu linapogusa biashara NADATA KABISAAAA.

Nahitaji kuacha Kazi na hili ndio TOBO LANGU.

MGANGA ATANIRUDISHA KWELI KWENYE RELI?

#YNWA
Bad time of yours can give u all the knowledge that scholl can't.
 
Naam hivi ndivyo allah huadhibu waja wake, wewe si humtambui? kwasababu tu ulijiona umejitosheleza.

"hapana! sivyo hivyo!, hakika mwanadamu ni mwenye kuvuka mpaka mno, pale anapojiona amejitosheleza."

Quran 96:6-7

Tiba ya hayo mambo sio kwenda kwa waganga huko sasa unaenda ulimwengu mwingine na hasara zitakuzidi mpaka utajinyonga, rudi kwa mola wako muombe msamaha na unyenyekee kwake, atakufungulia milango ya rizki na baraka nyingi, hakika yeye ni msamehevu mwenye huruma mno.
Sasa hapa Allah kaingiaje? Kwani jamaa kafanya kosa gani la kuadhibiwa?
 
Kwamba jamaa ni malaika? allah ameingia kwasababu ndiye mwenye kuwaruzuku viumbe na ndiye mwenye kuzibana rizki zao na kuwa finyu, ndiye mwenye kuzikunjua mpaka wakawa matajiri wakubwa na yeye ndiye mwenye kuwafanya wacheke na walie machozi wakati mwingine.
 
Back
Top Bottom