Niko njia panda yenye maumivu moyoni: Biashara yangu imelala sana je, niende kwa mganga?

Niko njia panda yenye maumivu moyoni: Biashara yangu imelala sana je, niende kwa mganga?

Boss kila mtu atakushauri hatawasifanya biashara. Nisikilize mm mfabya biashara mwenzako. Iko hiv, tangu januari hadi sasa march, biashara zote zimeshika. Sio wewe tu, mm nafanya biashara ya nguo dodoma. Juzi kati nilikua naangalia trend ya biashara yangu tangu mwaka uanze maana huwa natunza kumbukubu za mauzo kwa software kabisa. Aisee mauzo yameshjka kwa zaidi ya asilimia 30 kwa miez ya jan, feb hii mar, ukilinganisha na miezi ya oct, nov na dec 2022.

Sio mm tu hata majirani zangu hali sio sawa na mwaka jana. Kuna jitani yangu hapa yeye huwa anauza spea za pkpk na bajaj. Mwaka jana alikua bize sana muda wote ila tangu mwaka huu uanze, analala sana dukani, muda mwingi anachat tu.

Yaan uliposema tu tangu msaka huu uanze nikakuelewa. Usiemde popote, hujarogwa. Ni pesa tu imeadimika kitaa. Pia ujue kuwa biashara yako na hii yangu sio basic need. Mtu atakunywa na kuvaa kama ana pesa na watoto wameshiba. Nei za vyakula na mahitaji mengine muhimu zimepanda sana hivyo vipato vya watu haviruhusu kufanya vitu vya ziada.

Mm niko mpole tu kwa sasa. Tulia hali itarudi tu. Kila la heri

Kaka umeongea Vzr sanaaa
 
pole sana ila kuwa mvumilivu na subira biashara yoyote ile ina kupanda na kushuka vuta subira huku ukipambana angalia wapi umekosea kwenye hiyo biashara pajenge upaya
 
Nyie mnaoulizaga maswali ya kipolisi kama haya, huwa mmesoma cbe cert. in business management, hata biashara ya pipi hamjawahi kufanya.
Uwe na adabu basi kidogo. Ningekuwa sina ufahamu na biashara sasa hiyo akili ya kumuuliza hayo unadhani naitoa wapi?!
 
Skia mkuu acha kumpa stress mwenzio. Maswali ya kukariri darasani wakati mnasoma certificate ni tofauti sana na uhalisia wa biashara zenyewe. Kasema biasharavyake imeshuka kuanzia January hadi hii March, sisi tunaoziishi biashara ndio tunaona uhalisia mitaani. Biashara zote zimeshuka tangu huu mwaka uanze, tofauti kabisa na miezi ya August hadi December mwaka jana. Watu hawana pesa mifukoni ukizingatua biashara yake sio basosic need ni ya vinywaji. Mtu hadi ashibe na familia ile ndio afikiri kunywa. Vyakula vimepanda sana bei, mbona logic ndogo sana, kutiana stress tu.

Mkuu mtoa mada fuata ushauri wangu hapo juu. Utakuja kunishukuru. Hujarogwa na wala ww sio tatito, shida ni mzunguko tu wa pesa umeshuka. Hii sio kwa tu ni kwetu sote tunaoishi biashara. Am sure kufikia July mambo yatakaa sawa na tutaendelea kupiga pesa tena
Mbona kama haya maswali yangu yamekuchoma hadi unasema mimi nina Certificate ya program ya biashara kutoka CBE?

Kimsingi nikwambie unatakiwa kufahamu kuwa biashara unavyoijua wewe ni tofauti na ninavyoijua mimi. Mtazamo wako wa kibiashara hauwezi fanania na watu wote ndio maana kilichokushinda wewe wengine wanakifanya bila kutokwa jasho. Na unachokiweza wewe kuna ambao wanakishindwa kila siku wanafunga biashara baada ya kuchoma mitaji.

Anyways, sababu za kufeli biashara miezi umetaja inawezakana chanzo kilianza mwezi wa sita mwaka jana.

That's why nimeuliza maswali mtambuka ili muhusika atoe mwangaza.
 
Watu mnaotakaga muuze nyie na msipate ups en down huwa mnashangaza sana.

Achana kuuza hiyo 150k kuna time inafika hata 50k unakfikisha kwa mbinde na kila kitu unacho dukani kwako, huwa ni kawaida tu sababu zinaweza kua...

1- kuna competitor hapo mtaani anauza bei chee kukuzidi ilia kuvunja soko lako.
Njia rahisi wanayoingia nayo watu wengi ni kuuza vitu bei chee ili wajitangaze, ukiona ivo we tulizana tu watarudi.

2- usimamizi mbovu, kama husimamii wewe. Nenda uuze mwenyewe kuna vitu mtu kama sio mmiliki wa biashara anakosa maamuzi na kusababisha hasara au mteja kukimbia, mfano mteja wako wa kila aiku kakuungisha mzigo mkubwa tu ila kafeliwa jero. Mfanyakazi sio rahisi kumuachia hilo jero coz akiliacha itambidi alipe yeye maana boss hatamuelewa. Hivyo anamkazia na wateja wengine hujiskia vibaya na kuhama.

3- Vitu bei juu kuliko competitor wako

4-Late derivery

5-kutongoza na kugonga hovyo wateja wako/wenu.

Na kubwa zaidi ni kua mwaka huu kwa wafanyabiashara hasa wa vinywaji hali si nzuri mkuu.

Ukiona wewe unaeuza jumla huuzi basi jua huko kwenye magrocery hali ni mbaya zaidi.
Mwezi wa 3 ndo kabisaaa mgumu kuliko jan na feb.
 
Katika maelezo yako kuna makosa mengi umeyafanya na matokeo ndio haya

Kosa 1. (Mentality)Kusoma vitabu vya watu waliofanikiwa kimaisha sii kigezo cha wewe kuyapata mafanikio kama wao.

Hapa umefeli kwa kuamini kusoma vitabu vya waliofanikiwa na wewe utakuwa muongoni mwao bila kujua wewe na mwenye kitabu niwatu tofauti na nyakati zilikuwa tofauti vile vile.

kosa 2. (Income streams) ulipokuwa kileleni kwenye biashara yako ulishindwa ku diversify risk kwa kuanzia biashara nyingine ambayo wakati hii ina fall, income streams zingine zina gain momentums hapa na huku unapata pata ela kidogo. Kwenye hili elimu yako ilishindwa fanya kazi hapa

2. Kosa 3 (expenses) kosa hili huwa nkosa kubwa kuliko vyote ambayo huwa watu hawaongelei hata wewe hujatupa mchanganuo hapa..

mambo ni mengi mda ni mchache..

NB. Elimu uliyoipata haina msaada kwako kama itakushauri kwenda kwa mganga wakati wewe ndio mganga wa biashara yako.
 
What knowledge are you seeking sir/madam?
 
MGANGA ATANIRUDISHA KWELI KWENYE RELI.

INTRODUCTION:

Mimi ni mtumishi wa umma Ila pia nina ndoto za kuwa mfanyabiashara mkubwa sanaa...

Na nikiri NAPENDA HELA SAA.
Yaani ukitaka niwe na Amani basi laki kadhaa ziwe kwenye wallet yangu.

Katika kukimbiza ndoto zangu niliamua kufungua biashara ya vinywaji ya Jumla na rejareja (jina la mtaani tunaita Depo).

Nilikusanya mtaji nikiwa tayari nina idea na ilipofika mil 9 nikafungua depo.
Mil 6 bidhaa na mil 3 sunk cost kama kodi, Matengenezo frame na mengine yale ya maandalizi ya biashara.

Nauza vinywaji vyotee vikali na baridi, kwa jumla na reja reja, na kwasasa biashara yangu ina mtaji wa mil 25.

SCENARIO
Biashara ilianza vizurii mpaka nikawa nadata, yaani wateja walikuwa wengii.

Hawa wakani-force kukuza mtaji fasta mpaka kufika hizo mil 25.

Pia nikawa na vijana wa3 wa dukani, yaani ni fast delivery. Yaani mteja akikata tu simu basi bidhaa ipo mlangoni mwake.

Aisee nilipata jina fasta na kubwaa sanaa.

Mauzo yangu yalikuwa makubwa ya mil 3 Kwa siku na siku nisipouza yalikuwa hayashuki mil 1.

Kwasasa Nina Miaka kadhaa kwenye biashara (from July 2020).

Ila ndugu sasa biashara sielewi..

PROBLEM
Tokea January 2023 BIASHARA IMEKUWA NGUMU mnooo.

Mauzo mil 1 Tena jana ndio Majanga, nimefunga na laki 5..!!!

Pia hapa Nina miamala ya simu, na juzi (01/02) nililipwa commission ya 150k kwa mitandao yotee mi 4.

Wakati nilifika commison ya laki 5 kwa mitandao yote mi4.

Wateja simu sizioni, wakati Kuna kipindi walikua wanapiga simu mpaka saa 7 usiku kuniomba niwauzie bidhaa.

Hiyo saa 7 usiku watakukodia boda utakuja kufungua store utawauzia, wanakulipa na boda inakurudisha gheto kwa gharama zao.

Nina masters na bachelor ya mambo ya biashara, hivyo nimejaribu marketing skills kibao kama za kutuma sms kila asubuhi kuomba order kwa wateja, kupost status za WhatsApp ila 2023 bado ngumu kwenye biashara.

Sasa nimeshauriwa na raia NIENDE KWA MTAALAMU NIKAPIKWE.

Naambiwa, nilikua na nyota kalii hivyo competitor wameona waizime ili wao wauze.

DILEMA
Nimedata mwenzenu, ukicheki hii biashara ndio naitegemea kuwa ndio tobo la kunifanya nije kuachana na ajira za serikali ya CCM ila MBELE NAONA GIZA.

Nina mengi aisee siwezi kuandika yote, mfano: siku hizi nafungua saa 1 kamili asubuhi na kufunga saa 5 usiku.
Na hata kazini (halmashauri) nimepasusa naona pananichanganya tu (wiki yotee hii (Tokea 30/01)SIJAFIKA KAZINI.

KUHUSU VITABU-
Hivi vitabu sijui vya Robert koyasaki na wengine NIMESOMA SANAAA.
Tokea 2020 nishasoma vitabu kama 30 hivi vya mambo ya biashara na fedha na Robert Koyasaki pekee yake ni vitabu vi5 kuanzaia Rich Dad mpaka Money Quadrant.

Vingi vinazungumzia "Kwenye financial world Usikate tamaa, pambana"" ila nahisi Kuna kamba ipo nyuma ya mapambano yangu inanivuta nyuma.

NAPAMBANA NYIE...
1. Muda wote duka nalifanya safi
2. Rangi zinavutia (mashelf na ukuta)
3. Kama elimu, Nina degree mbili za biashara (bachelor + masters)
4. Kama ni experince, nishauza sanaa biashara za watu Tena bila mshahara (kipindi najifunza biashara)
5. Kama ni ukarimu, basi ni mkarimu sanaa. Humu Kuna watu wawili tulishaongea sanaa Japo kwa simu (kama wako comfortable wanaweza thibitisha hapa).

Kifupi nafanya mengii ila 2023 imekua ngumu.
Imefikia mpaka kupunguza wafanyakazi dukani kutoka 3 mpaka 1..!!!

Na kilichonifanya nipost ni baada ya commision kushuka kutoka 500k mpak 150k kwa Jauary/2023.

Huwezi amini:-
Jumapili ya wiki hii sikufungua, ili tu nione upepo wa wateja, ila chakusangaza mpaka unaingia usiku sijapokea simu hata ya mteja mmoja kulalamika "Mbona nimefunga"

Kwasasa sijui si-exist kwenye phone book zao..!! Niko kudata balaaa yaani waliokuwa wakinipigia simu usiku nao hawapigi hata mchana..!!!

Kazini sijaenda wiki maana kichwa ni cha moto balaaa.

Nipeni mawazo wajasiliamali wenzangu.
Nipeni mawazo wafanyabiashara wenzangu.

Nishapitia msoto mkubwa sanaa kwenye maisha ya uyatima, kazini, kwenye ujana wangu ila Jambo gumu linapogusa biashara NADATA KABISAAAA.

Nahitaji kuacha Kazi na hili ndio TOBO LANGU.

MGANGA ATANIRUDISHA KWELI KWENYE RELI?

#YNWA
Ungejalibu kujiuliza hao wateja wako sasa hivi wanachukulia mzigo wapi? Hapo ndiyo pa kianzia na huko wanakochukulia kuna tofauti gani na wewe?
 
Katika maelezo yako kuna makosa mengi umeyafanya na matokeo ndio haya

Kosa 1. (Mentality)Kusoma vitabu vya watu waliofanikiwa kimaisha sii kigezo cha wewe kuyapata mafanikio kama wao.

Hapa umefeli kwa kuamini kusoma vitabu vya waliofanikiwa na wewe utakuwa muongoni mwao bila kujua wewe na mwenye kitabu niwatu tofauti na nyakati zilikuwa tofauti vile vile.

kosa 2. (Income streams) ulipokuwa kileleni kwenye biashara yako ulishindwa ku diversify risk kwa kuanzia biashara nyingine ambayo wakati hii ina fall, income streams zingine zina gain momentums hapa na huku unapata pata ela kidogo. Kwenye hili elimu yako ilishindwa fanya kazi hapa

2. Kosa 3 (expenses) kosa hili huwa nkosa kubwa kuliko vyote ambayo huwa watu hawaongelei hata wewe hujatupa mchanganuo hapa..

mambo ni mengi mda ni mchache..

NB. Elimu uliyoipata haina msaada kwako kama itakushauri kwenda kwa mganga wakati wewe ndio mganga wa biashara yako.

Nisiende kwa mganga ila kanisani na msikitini niende...
Nyie watu nyieeee

#YNWA
 
Nisiende kwa mganga ila kanisani na msikitini niende...
Nyie watu nyieeee

#YNWA
Hakuna kanisa wala msikiti wa mganga anayeweza mpa mtu utajiri. Utajiri ni wewe mwenyewe

Mfano nikusema naenda kanisani au msikitini kuomba mungu anisaidie kufungua account ya jamii forum hivyo hivyo kwa mganga, bila kujua kwamba wewe mwenyewe ndio waweza fungua account ya jf.
 
Back
Top Bottom