Niko njia panda yenye maumivu moyoni: Biashara yangu imelala sana je, niende kwa mganga?

Maliza kwanza kusort issues za biashara yako then tutajadili.
 
Mnatuchosha bana na maimani yenu. Unashindwa kuzungumza hoja zenye uhalisia unajificha kwenye kivuli cha Allah. Huo ni uvivu wa kufikiri bwana. Kama huna cha kushauri heri ukakaa kimya shekh.
 
Una beza uganga kwenye biashara?
 
Hahaaaa
 
Achana na Mganga..
Wewe ni Liverpool Fan.. Mnasema YNWA.. Tough times ndio hizi..
Wacheki kina Kloop na Mo Salah wakutafutie wateja..!
 
Oa!
Mke Ni mshauri na baraka!
Jali afya yako ya akili😁
NIOE hawahawa
Unazungumzia hawahawa wenye
1. Kuamka asubuhi wamenuna
2. Wenye midomo ya kupepeta kama feni
3. Wenye kununanuna tuuu
4. Wenye kuwapa maEX

Hawahawa ambao mkiachana mnagawana Mali?

NB:- afya yangu ya akili iko vizuri.
KUWAZA African religion sio kisa kama wewe unavyowaza ukasali mbele ya sanamu la rozari na sanamu la bikra maria.

Umeamua kuchagua mababu wa wazungu HUNA KOSA
nimeamua kuchagua mababu ya kiafrica SINA KOSA.

#YNWA
 

Inategemea na mtaji wako kiongozi,ila kwenda kwa mganga ni matumizi mabovu ya akili
 
Nitakachokufundisha sio uchawi nia mambo yapo na yanafanyika

Kama kuna mtu anaichezea biashara yako fanya hivi tafuta chumvi ya mawe ogea kwa siku 7, 14 au 21 hapo utachagua wewe hasa nyakati za usiku kabla ya kulala(usiogee chooni) kama kuna mtu anajaribu kukuchezea majibu atayapata

Unaweza kudharau ila kama unaijua nguvu ya mawe basi utarudi kunishukuru baadae
 
kwanza hujataja lokeshen yani sehemu unayo fanyia biashara niwapi.maranyingi iko hivii..usiweke dukalako lionekane lakishua Sana sehemu ya waswahili Kuna wateja hawata kuja kabisa humo.wabongo tuna zarau ,aibu na wivu.

unaweka tailiz zako mteja mwingine anajiangalia kwanza yeye jinsi alivyo na sehemu anayo enda kununua bizaa.anajifikiria kwanza nikienda pale michoro mingi nimevaa ndala duka lenyewe lakishua ngoja niendezangu kwa muha pale.anaenda kwa muha anakuta kwanza sakafu imebomoka muha mwenyewe tisheti imechanika haja vaa hata ndala

hapo anakuwa huru kununua hatakama niunga robo ananunua kwa kujiamini.wee umevaa vizuri utawasubiri washua wenzako waje kukuungisha maamae🤣🤣

Mimi ndio Mana saazingine wale wateja wangu waaminifu nikiwa nawateja wengi akija anataka sukari namuonyesha jiwe lakupimia anajipimia mwenyewe anatoa hela anaondoka zake unamfanya ajione pale nikwake usitumie nguvu tumia akili..🤣🤣🤣
 
Unatakiwa uwekeze mtaji mwingine na kufanya innovation wakati ulipofikia kwenye peak yako,hicho ndio kitu kinaitajika kwenye hiyo biashara yako,pia badilisha human capital ,na mazingira ya hiyo biashara,ukienda Kwa mhanga atakuambia utoe mtoto sadaka,ni mambo mazito,
 

Huna ulijualo
 

Imani zakuja zimewaharibu waafrika,fuvk
 
Kaka nakusalimia,
Nakushauri mambo machache
1😛unguza presha (chukulia kawaida )
2; kamwe usijaribu kwenda kwa mganga (baadae utakuja kujuta maisha yako yote)
3;January Ina tabia hiyo(majukumu mengi)
4:Mrudishe mtu mmoja dukan wawe 2 ili huduma ya delivery awesome
5chunguza kauli au utendaji kazi wa wafanyakazi wako yawezekana wamejisahau ukiwa haupo wanajibu wateja vibaya au wanapikea muzigo bubu (mizigo isiyoingizwa kwenye maandishi)we ukija unaona pombe zipo kumbe zimefanyiwa replacement

Sugua magoti umuombe mungu kwenye biashara Kuna vita sana,
Kama umeowa muweke mkeo kama controller
Pia weka kamera utagundua kitu

Uwe na usiku mwema


Sent from my Infinix X680 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…