Niko njia panda yenye maumivu moyoni: Biashara yangu imelala sana je, niende kwa mganga?

Je unalipa kodi kama inavopaswa? Watumishi watatu unalipa sh.ngapi? Ofisi umepanga au ni yako? Tofauti na pombe umeweka bidhaa nyingine zinazoendana kama sigara nk.?
1. Hakuna anayelipa kodi sawasawa, nakwepa sanaa mishale ya TRA, FIRE ila Afisa Biashara HATUDAIANI.
2. Sasa hivi Nina 1, mshahara kwa mwezi 70,000/= na kila siku posho 2,500/=
3. Ofisi/frame + store nimepanga@nalipa kodi ya pango.
4. Kwasasa nauza vinywaji tu (vikali na baridi). Ila lengo la mwaka huu ni kuweka/kuongeza opener, glass disposable na sigara.

#YNWA
 
Pamoja na yote Jesus love you!
 
Hehehe biashara sio simple hivyo kama unavyotaka kuaminisha watu hapa.
 
Hii n kweli kabisa 💯 kuna Duka unaliona hiv alaf unaangalia mwonekano wako unaachana nalo unaenda la mbali😀😀😀
 
Bisshara ni wave motion haiend juu tuuu mzee pambania kombe uinuke kuvuka zaidi,
 
Pamoja na ushauri wa wengi kwamba ni January ngumu vumilia,ila Bado watanzania ni wanafiki sana, na tunapenda kuficha ukweli.
Mafanikio yoyote lazima uchague upande kati ya hizi na ujitose ,Kwa Mungu mazima mazima au Kwa Shetani (waganga mazima mazima).
Ukibaki bila uchaguzi( uvuguvugu)hata Mungu mwenyewe kasema kwenye neno lake kwamba atakutapika.
Sasa wadau hapa wanasingizia sana January,yaweza ikawa kweli,je kwani wakati anaanza January 2021,2022 zilikuaje!? Mbona hajaja kuomba ushauri?
Ukiona amekuja kuomba ushauri ameona ishara mbaya kwenye biashara yake.
Chagua mkuu kuwa wa moto au baridi, usikubali kuwa vuguvugu, mafanikio sio lelemama.ni vita kubwa ya kiroho.
Umenisoma Asante.
 

Na kuna wasioupande wowote na mambo yanaenda tu.
Ipo hivi utajiri ni 💯%
40% wapo KWA MUNGU
40% wapo kwa shetani
20% none believers hawaamini kwa Mungu wala shetani.
All in all ili ufanikiwe cheza na ulimwengu wa ROHO
 
Dini yako kwanza halafu nikupe mbinu hapa sio Kwa mganga Huwa mganga ni mwisho umekwama
 
Hakuna mganga atakaekupa life insurance my dear. Kama ni kweli umechezewa na ukaenda kwa mganga nao watatafuta mganga mkubwa zaidi Ili wakupoteze itakua ni vita.

Omba kwa Imani Yako mrudie Mungu wako hakika utauona ukuu wa Mungu.
Biashara Zina mambo mengi sana humu duniani. Pole mkuu
 
huo mtaji ulio anzia bishara uliupataje? ulipewa uliokota ulianzia chini ukapanda mpaka kufikia m9 au ulipataje mtaji huo tuuanzie hapo hili tuweze kukupa ushauli mzuli
 
Nina swali kwako Mzee wa KATAA NDOA. Je, baada ya mauzo ya laki 5 kwa siku huwa net profit ni Tsh ngapi?
 
Kiufupi mtoa mada ana maamzi ambayo amesha yachukua na sidhani kama ushauri utamsaidia maana tayari kuna vitu anaamini kuwa vipo sahihi kwa mtazamo wake.

Nachoweza kumshauri just fata what your instincts is telling you brother . Whatever the consequences you are responsible with your own decision.
 
Laana hizo za kampeni yako ya kishetani ya kataa ndoa(kidding)
 
Hii n kweli kabisa [emoji817] kuna Duka unaliona hiv alaf unaangalia mwonekano wako unaachana nalo unaenda la mbali[emoji3][emoji3][emoji3]
Ni kweli kabisa ndugu wala hajakosea.
Huyo jamaa anaonekana ni mzoefu wa biashara na amesoma tabia za wateja wake.
Kwa mfano bei ya mkate kwenye supermarket ni sawasawa na bei ya mkate kwenye duka la mangi/muha lakini low income earners wataenda kununua kwa mangi/muha na si supermarket kwa sababu ya aibu ya kujishtukia muonekano wao pamoja na uwezo mdogo wa kipesa wakihisi wataaibika.
Ni baadhi tu ya watu wa middle income na kuendelea ndio huwa na confidence ya kuingia popote wakiamini bei yoyote watakayotajiwa wataimudu tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…