Niko njia panda yenye maumivu moyoni: Biashara yangu imelala sana je, niende kwa mganga?

Umetoa details kirahisi sana. Biashara inaangukaje kirahisi namna hiyo bila kuwapo na vyanzo vya wazi wazi?

Mimi nina maswali:

1. Nani ni manager wa biashara yako?

2. Nani anasimamia vitabu vya mahesabu ya mauzo?

3. Wewe katika biashara hii unasimama kama nani au una shirikije katika biashara hii?

4. Kama wewe ndie unawasiliana na hawa wateja, je kuna complain zozote ambazo ulikuwa ukizisikia kutoka kwao na haukuzipa uzito?! ( Hili swali muhimu sana)

5. Hawa vijana wako uliowaajiri umeshafanya nao kikao maalumu kujadili hii hali ya biashara ili wakwambie tatizo au matatizo wanayoyaona upande wao?!

6. Je, unawalipaje vijana wako, na katika kuwalipa wanaridhika?!

7. Competitors wako ni akina nani na je umejaribu kuchunguza kama wateja wako wanakwenda kwa wenzako?!


Kuna maswali mengi sana ya kuhoji hapa.
 
Nyie mnaoulizaga maswali ya kipolisi kama haya, huwa mmesoma cbe cert. in business management, hata biashara ya pipi hamjawahi kufanya.
 
Skia mkuu acha kumpa stress mwenzio. Maswali ya kukariri darasani wakati mnasoma certificate ni tofauti sana na uhalisia wa biashara zenyewe. Kasema biasharavyake imeshuka kuanzia January hadi hii March, sisi tunaoziishi biashara ndio tunaona uhalisia mitaani. Biashara zote zimeshuka tangu huu mwaka uanze, tofauti kabisa na miezi ya August hadi December mwaka jana. Watu hawana pesa mifukoni ukizingatua biashara yake sio basosic need ni ya vinywaji. Mtu hadi ashibe na familia ile ndio afikiri kunywa. Vyakula vimepanda sana bei, mbona logic ndogo sana, kutiana stress tu.

Mkuu mtoa mada fuata ushauri wangu hapo juu. Utakuja kunishukuru. Hujarogwa na wala ww sio tatito, shida ni mzunguko tu wa pesa umeshuka. Hii sio kwa tu ni kwetu sote tunaoishi biashara. Am sure kufikia July mambo yatakaa sawa na tutaendelea kupiga pesa tena
 
Ndio hivyo mkuu.
Watu wanalalamika sana mtaani hakuna hela.
So automatically watapunguza matumizi hasa kwenye mambo ya anasa.
 
Pole,ila kushauri,hapo kwenye uganga,wanaenda kufilisi kabisa.Hujasema kama ushindani umebadilika je,mazingira ya biashara yako mwanzo na sasa nini kimebadilika?Kama wewe ni mtumishi najua huna muda wa kutosha kujua mazingira ya biashara yako kwa karibuπŸ€”.Vipi mienendo ya waliokuwa wafanyakazi wako.Haiku athiri biashara yako bila wewe kutambua?Je hawakutumia na wash indani wako ili kupata wateja wako?Je haijakuwa na migogoro ya kikodi,au leseni?Tuliza akili jifunze wapi palipo na shida , ikiwezekana igawe biashara nenda sehemu nyingine.
 
Nyie mnaoulizaga maswali ya kipolisi kama haya, huwa mmesoma cbe cert. in business management, hata biashara ya pipi hamjawahi kufanya.
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]Hata pipi hawajawahi kuuza
 
Ndio hivyo mkuu.
Watu wanalalamika sana mtaani hakuna hela.
So automatically watapunguza matumizi hasa kwenye mambo ya anasa.
Halafu anatokea mtu na degree ya uchumi ya kukaririshwa anaanza kukuliza maswali ya kukustress tu. Watu wengi wanaofanyaga biashara na kujifanya wanaendesha biashara zao kwa misingi sanaa huwa hawadumu, ila yule anaefanya kwa elimu kitaa tu huwa wana survive sana
 
Wazo zuri unaweza kuta hata wateja wakichukua mzigo unakawia kuisha kwan walaji hawana tena hela ming
 
Umempatia wazk zuri sema naona tayari Imani yake iko rigid akadai kuwa Ana masters amesoma vitabu vya robati kiyosaki as if ni guarantee ukivisoma unatoka
Huyu ni kumwambia au kumpa namba ya mganga
 
Anataman dunia izunguke tofauti kwake tu
 
Nami nipo kwenye dilemma kama wewe na nimeshawatembelea manabii kama wote na waganga wale wanaosifiwa sana Tanga, Pemba, Masasi lakini bado nipo chali ......najipanga kwenda labda kwa nabii ambaye sijawahi kwenda kwake Kuhani Musa au waganga wa Msumbiji....Kwa kweli najionea mazingaombwe mengi sana.....nimechoka sana sana.......kwa mtu ambaye hayajamkuta najua atatoa povu sana humu lakini huyo mtoa mada nimemuelewa sana...mpaka yakukute
 

Maswali ya Msingi :

- Ulipoanza hao wateja walitoka wapi na ukua na Mganga?

- Hakuna mpinzani karibu kweli? Mzee wa marketing ume study customers and business behaviors?

- Kuna namna biashara imekusaidia mfano kujenga nyumba, au gharama fulani? Kubwa?

- Je kuna kiasi kikubwa cha hela ya Biashara umekitoa nje ya mzunguko?

- Staff ni wale wale au umsbadili? Una any feud na staff yeyote ambaye ameondoka kwa hasira?

Tabia zako:

- Jifunze kuwa na shukran, una ajira na kipago. Hicho kakupa Mungu, tamaa inayokupeleka kwa Mganga, utaharibu mpaka ajira.

- Love for money, inayokupeleka kwa mganga ni mbaya sana na itakuharibia maisha, yaweza kukufurahisha tu kwa Kitambo.

Ushauri:

Kama mtaji wako unafika 20m kwa sasa, funga biashara, weka hela kwenye account, halafu tulia, maana ni mara 2 ya hela uliyowekeza.

Ukiendelea na hiyo biashara baada ya kuonyesha kutokuwa na shukrani kwa kiwango hiki cha Mungu ambavyo ameshakupa, utafilisika mazima, take my worda.
 
chuki za nini kijana kueneza uongo? Huyo Yesu wenu anajua kiswahili?
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ Ushasikia kuna kanisa linamuita yesu kwa kiyahudi yesu fundi anasikia lugha zote sio allah mpka umwage kiarabuπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ Ushasikia kuna kanisa linamuita yesu kwa kiyahudi yesu fundi anasikia lugha zote sio allah mpka umwage kiarabuπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
kumbe ni yahudi basi anajua kiyahudi tu na alikuwa anaitwa Issa (au Aissa). Tafuta kwenye youtube utaona.
 
Maisha ya watu ni uwongo mtup na watakwambia nenda Kwa doctor kumbe wao hawaendi au usiende kumbe wao wanaend chamsingi unacho weza Fanya kunusulu biashar we Fanya tu chamsingi utoke maana kutoka kuliwatesa ata Wanawaisraile kama unaweza kuloga Loga na kamaunaweza kusalisa ili kutoka kwenye umaskini
 
Jaribu kuomba kwa imani yako huenda ikawa njia sahihi zaidi kuliko kwenda kwa mganga ijapokuwa anaweza kukusaidia pia
 
Najua huu uzi ni wamda mrefu sana, lakini labda niwaambie tu wengine mtakaokuja kupitia koments. Kila mfanyabiashara ana kimoja kati ya viwili 1:MUNGU,2: SHETANI.
Kwaiyo hakikisha unachagua kimoja chakwenda nacho ukiwa mtupu utafanikiwa kama biashara yako inamtaji wa laki kushuka.
 
Tangu tulipofika katikati ya November biashara nyingi zilianza kushuka. January na February 2023 ndio imekuwa balaa ukitia ndani mwezi March . Kwa sasa tunasubiri mstakabali wa mwezi April.

Ila kuna uhusiano wa mvua nyingi na biashara. Kukiwa na mvua nyingi biashara nyingi zinadorola na biashara za viwatilifu zinapaa juu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…