Niko njia panda yenye maumivu moyoni: Biashara yangu imelala sana je, niende kwa mganga?


Kaka umeongea Vzr sanaaa
 
pole sana ila kuwa mvumilivu na subira biashara yoyote ile ina kupanda na kushuka vuta subira huku ukipambana angalia wapi umekosea kwenye hiyo biashara pajenge upaya
 
Nyie mnaoulizaga maswali ya kipolisi kama haya, huwa mmesoma cbe cert. in business management, hata biashara ya pipi hamjawahi kufanya.
Uwe na adabu basi kidogo. Ningekuwa sina ufahamu na biashara sasa hiyo akili ya kumuuliza hayo unadhani naitoa wapi?!
 
Mbona kama haya maswali yangu yamekuchoma hadi unasema mimi nina Certificate ya program ya biashara kutoka CBE?

Kimsingi nikwambie unatakiwa kufahamu kuwa biashara unavyoijua wewe ni tofauti na ninavyoijua mimi. Mtazamo wako wa kibiashara hauwezi fanania na watu wote ndio maana kilichokushinda wewe wengine wanakifanya bila kutokwa jasho. Na unachokiweza wewe kuna ambao wanakishindwa kila siku wanafunga biashara baada ya kuchoma mitaji.

Anyways, sababu za kufeli biashara miezi umetaja inawezakana chanzo kilianza mwezi wa sita mwaka jana.

That's why nimeuliza maswali mtambuka ili muhusika atoe mwangaza.
 
Watu mnaotakaga muuze nyie na msipate ups en down huwa mnashangaza sana.

Achana kuuza hiyo 150k kuna time inafika hata 50k unakfikisha kwa mbinde na kila kitu unacho dukani kwako, huwa ni kawaida tu sababu zinaweza kua...

1- kuna competitor hapo mtaani anauza bei chee kukuzidi ilia kuvunja soko lako.
Njia rahisi wanayoingia nayo watu wengi ni kuuza vitu bei chee ili wajitangaze, ukiona ivo we tulizana tu watarudi.

2- usimamizi mbovu, kama husimamii wewe. Nenda uuze mwenyewe kuna vitu mtu kama sio mmiliki wa biashara anakosa maamuzi na kusababisha hasara au mteja kukimbia, mfano mteja wako wa kila aiku kakuungisha mzigo mkubwa tu ila kafeliwa jero. Mfanyakazi sio rahisi kumuachia hilo jero coz akiliacha itambidi alipe yeye maana boss hatamuelewa. Hivyo anamkazia na wateja wengine hujiskia vibaya na kuhama.

3- Vitu bei juu kuliko competitor wako

4-Late derivery

5-kutongoza na kugonga hovyo wateja wako/wenu.

Na kubwa zaidi ni kua mwaka huu kwa wafanyabiashara hasa wa vinywaji hali si nzuri mkuu.

Ukiona wewe unaeuza jumla huuzi basi jua huko kwenye magrocery hali ni mbaya zaidi.
Mwezi wa 3 ndo kabisaaa mgumu kuliko jan na feb.
 
Katika maelezo yako kuna makosa mengi umeyafanya na matokeo ndio haya

Kosa 1. (Mentality)Kusoma vitabu vya watu waliofanikiwa kimaisha sii kigezo cha wewe kuyapata mafanikio kama wao.

Hapa umefeli kwa kuamini kusoma vitabu vya waliofanikiwa na wewe utakuwa muongoni mwao bila kujua wewe na mwenye kitabu niwatu tofauti na nyakati zilikuwa tofauti vile vile.

kosa 2. (Income streams) ulipokuwa kileleni kwenye biashara yako ulishindwa ku diversify risk kwa kuanzia biashara nyingine ambayo wakati hii ina fall, income streams zingine zina gain momentums hapa na huku unapata pata ela kidogo. Kwenye hili elimu yako ilishindwa fanya kazi hapa

2. Kosa 3 (expenses) kosa hili huwa nkosa kubwa kuliko vyote ambayo huwa watu hawaongelei hata wewe hujatupa mchanganuo hapa..


mambo ni mengi mda ni mchache..

NB. Elimu uliyoipata haina msaada kwako kama itakushauri kwenda kwa mganga wakati wewe ndio mganga wa biashara yako.
 
What knowledge are you seeking sir/madam?
 
Ungejalibu kujiuliza hao wateja wako sasa hivi wanachukulia mzigo wapi? Hapo ndiyo pa kianzia na huko wanakochukulia kuna tofauti gani na wewe?
 

Nisiende kwa mganga ila kanisani na msikitini niende...
Nyie watu nyieeee

#YNWA
 
Nisiende kwa mganga ila kanisani na msikitini niende...
Nyie watu nyieeee

#YNWA
Hakuna kanisa wala msikiti wa mganga anayeweza mpa mtu utajiri. Utajiri ni wewe mwenyewe

Mfano nikusema naenda kanisani au msikitini kuomba mungu anisaidie kufungua account ya jamii forum hivyo hivyo kwa mganga, bila kujua kwamba wewe mwenyewe ndio waweza fungua account ya jf.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…