Nikosoe kama nimekosea kuhusu UTT Liquid acc

Nikosoe kama nimekosea kuhusu UTT Liquid acc

Ni kwamba, hizo ni gharama za mitandao ya simu au wakala wa kuihamisha pesa lakini sio gharama za UTT kuweka pesa.

Hata kwenye benki ulizozitaja kwamba ni Bure, Bado Kuna gharama ya usafiri na muda utatumia kwenda benki, ni gharama.

Anachomaanisha mleta mada ni UTT kutokutoza pesa unapoweka pesa zako kwao.
We ndo bado hujaelewa, na inawezekana ndo hujui kabisa, Iko hivi kuweka hela UTT kupitia NMB au CRDB, huhitaji kwenda bank, ukiwa na App unamaliza Zoezi kirahisi
 
sijawai kuweka kwa kutumia simu
Pia ni vizuri ungetuambia makato ni sh ngap

Maana hata kuingia Menu yao ni bure ila kama unatumia au umeunga na namba ya tigo.
Kama umeunga na mtandao mwingine wanakata 20.
Kwaiyo kama una sh 100 utaangalia mara 5 ni gharam ndogo.
So unachagua kati ya bure na gharama ndogo
Ukitaka kuhamisha hela kutoka mtandao wa simu (Tigopesa,M-pesa au Airtel money) kwenda account ya UTT kuna charges, kuhusu kiwango wanachokata inategemea na kiwango unachoweka
 
M
Hapana Kwa UTT ni mifuko miwili tu ndio inatoa dividends, Jikimu inakupa kila baada ya miez 3 lakini kama kumbukumbu zangu Iko sawa kigezo lazima uwe juu ya 5m na Bond inakupa kila mwez kwa same the same kigezo pia kwa bond chini ya 5m nafikiri utakuwa unapokea Bi-annual

Mifuko Iliobaki Ni ya kukuza mtaji 100%
Bond ili upate gawio la kila mwezi inabidi uwe na mzigo sio chini ya 10m
 
We ndo bado hujaelewa, na inawezekana ndo hujui kabisa, Iko hivi kuweka hela UTT kupitia NMB au CRDB, huhitaji kwenda bank, ukiwa na App unamaliza Zoezi kirahisi

Swali. Hizo gharama wanazotoza makampuni ya simu ni za UTT au zakwao?

Wewe umepinga kwamba kuweka pesa UTT sio Bure. Hapo ndio hoja ilipoanzia.

Sasa kama unasema sio Bure huku ukiangazia gharama za makampuni ya simu na kutokea mfano Kwa app ni Bure, kwani mtu hawezi kwenda kuweka pesa benki kama mojawapo ya chaguzi?

Kuhusu kuelewa au kutokujua kwangu kuhusu UTT siwezi kuliongelea sana na sifikirii litaleta tija hapa ila huu ni ujumbe ulioelekezwa kwangu.

Screenshot_2024-11-23-08-10-54-69_0ce57feeccaa51fb7deed04b4dbda235.jpg
 
Swali. Hizo gharama wanazotoza makampuni ya simu ni za UTT au zakwao?

Wewe umepinga kwamba kuweka pesa UTT sio Bure. Hapo ndio hoja ilipoanzia.

Sasa kama unasema sio Bure huku ukiangazia gharama za makampuni ya simu na kutokea mfano Kwa app ni Bure, kwani mtu hawezi kwenda kuweka pesa benki kama mojawapo ya chaguzi?

Kuhusu kuelewa au kutokujua kwangu kuhusu UTT siwezi kuliongelea sana na sifikirii litaleta tija hapa ila huu ni ujumbe ulioelekezwa kwangu.

View attachment 3159310
Hamjaelewana tu mwendelee mtakaa sawa kwene mstari mmoja
 
Mkuu, Mimi nakukosoa kidogo, hapo uliposema kuweka hela ni bure. Inategemea unatumia njia gani, Kama ni kupitia CRDB au NMB ni sahihi ni Bure,
Ila kama utatumia mitandao ya simu (Vodacom, Tigo, Airtel) kuweka hela UTT kuna makato tena makubwa tuu
Ni kweli kwa mitandao ya simu Kuna gharama kubwa, tumia bank hizo
 
Si kweli hawa jamaa wamenyooka sana, haiwezi fika huko. Kuna muda inapita hata hiyo 12%
Unabisha nini sasa!

Wewe umewekeza UTT tuanzie hapo.

Vijana wa JF mnabisha hadi raha.
 
Uliyoyaandika hapo juu ni sahihi ila kuna sehem nakurekebisha au kuongezea

Yes Riba ndio wastan wake huo kati ya 10 % hadi 12% na hii ni kwa kifuko yote waliyonayo ndan ya kupindi cha miaka 10 iliopita.. yaan maana yake kuna mwaka itapiga 10% na kuna mwaka itakwenda hadi 14% au 15% mfano mwaka jana kuna mifuko ilipiga 14% na kuna mifuko ilipiga 12% mwaka huu ile iliopiga 12 minginr imekwenda had 12.9% au 14% na ile iliopiga 14% imeshuka hadi 12%

So ili kuwa conservative we chukulia UTT inakupa 10%. Flat kila Mwaka.

Pili umeongelea kupata 1% kila mwez kwa maana ya kuigawa 12% ya mwaka.. kiuhalisia kama utajiunga na Bond au Jikimu utapata magawio ya kila mwez kwa bond na ya kila robo mwaka kwa Jikimu ILA HUPEWI 1% ya faida.. utapewa kati ya 0.7% hadi 0.86% maana yake kama umeweka miliona 10 kwa bond kila mwez utapata kati ya 80,000 hadi 90,000 na sio laki moja

Maana yake ni kuwa kwa mwaka mfuko unaweza kuwa umeingiza faida ya 12% ila wewe ukipiga hesabu ya magawio yako utaona umepokea around 8% hadi 9% hi ni sababu % zilizobaki zinakava vitu vifuatavyo

1. Gharama za uendeshaji. Maana yake kuna vipoint vya silimia ya faida UTT wanachukua kama service charges

2. Kuna vipoint vya asilimia ya faida
Vinarudishwa kwenye mtaji wako kukuza mtaji. Ndio maana ukiweka 10m pamoja na kuchukua faida kila
Mwez ila Mtaji wako bado unaongezeka utajikuta mwisho wa mwaka uko na 10M na laki kadhaa.. plus ile faida uliyokuwa unabeba kila mwezi

Kwa sasa ili upate faida ya 100k kila mwez we weka 12M na sio 10M

yote kwa yote mifuko ya aina ya UTT ni moja ya uwekezaji bora zaidi mtu anaweza akafanya.. kama taifa tumechelewa kuanzisha hii mifuko sasa hivi ndio inachipukia mingine ila ni mifuko ambayo ingewainua maskin wengi

by the way kwenye maisha tuna trade mda wetu kwa fedha.. mtu atasema kwa 10m ninaweza kuanzisha biashara ya kunipa 100k had 300k kwa siku ila utaona ameangalia mtaji wa pesa tu hajaangalia mtaji wa mda.

Kwa mfanyakazi mwenye ajira anayetafuta mrija wa kipato cha pili ..asikimbilie kuwekeza kwenye biashara itakayompa kipato sawa na mshahara anaopata akifanya hivyo ni lazima akubali upande mmoja uathirike mda ni ulele.. bora awekeze kwenye uwekezaji wa muda mrefu target ziwe 20 years baadae awe na uwezo wa kuishi kutokana na gawio.. sehemu ya mshahara itupe UTT afanye kama
Fixed deposit italinda thaman ya pesa yame
Mkuu, Hivi ukiwa na pesa UTT kwenye mfuko wowote ule, unaweza kukopea Bank?? Nikimaanisha pesa zangu zibaki UTT ila Bank wanipe hela kufanya biashara.

Bank watahitaji document gani kama uthibitisho?
 
UTT n mfuko wa hisa

✅Unatoa riba ya 12% kwa mwaka
✅kutoa pesa inachukua siku 3
✅Unaweza chukua pesa zako muda wowote
✅Riba yake haibadiliki kama mifuko mingine
✅Haina makato ya kila mwezi kama benk
✅Kutoa hela ni bure kabisa na kuweka ni bure
✅Unaweza kuuza na kununua vipande muda wote
✅Ukiweka hela weekend Jumamosi na jumapili utasubiri mpaka j4 ndo utaiona kwene acc yako ya UTT (48/72hrs)
✅Ukihamisha hela inachukua 24hrs ya siku za kazi kuonekana kwene acc
✅Faida hawaweki kila siku…Ila wataweka tu punguza waswas



🟥HESABU YA MILION 1
Ukiweka milion 1 utapata kwa mwezi
12% kwa mwaka kwa mwezi ni 1%

1,000,000 x 1%= 100,000
Hivo ukiwekeza milion 1 kwa mwezi utajipatia 10000

KWA MWAKA
12% X 1,000,000= 120,000
Kwa mwaka utapata lak na 20

🟥HESABU YA MILION 10
10,000,000* 1%= 100,000 kwa mwezi

10,000,000*12= 1,200,000kwa mwaka

Kwa kifupi ukiweka milion kumi unalipwa laki kila mwezi ni sawa na mshahara wa mtu sehemu fulani

Uko sahihi. Hii kitu wastaafu wengi wakijielekeza huko hawatakuja kunishukuru.
 
Mimi nimewekeza hapo ila hiyo 12% sijawahi Iona naona ni kama wanaingiza 8.9% kila mwezi

Basi wewe unapigwa. UTT haina income tax. Sasa kwa nini ulipwe pungufu ya 12%? Nenda kadai hela yako bro
 
Back
Top Bottom