Nikosoe kama nimekosea kuhusu UTT Liquid acc

We ndo bado hujaelewa, na inawezekana ndo hujui kabisa, Iko hivi kuweka hela UTT kupitia NMB au CRDB, huhitaji kwenda bank, ukiwa na App unamaliza Zoezi kirahisi
 
Ukitaka kuhamisha hela kutoka mtandao wa simu (Tigopesa,M-pesa au Airtel money) kwenda account ya UTT kuna charges, kuhusu kiwango wanachokata inategemea na kiwango unachoweka
 
M Bond ili upate gawio la kila mwezi inabidi uwe na mzigo sio chini ya 10m
 
We ndo bado hujaelewa, na inawezekana ndo hujui kabisa, Iko hivi kuweka hela UTT kupitia NMB au CRDB, huhitaji kwenda bank, ukiwa na App unamaliza Zoezi kirahisi

Swali. Hizo gharama wanazotoza makampuni ya simu ni za UTT au zakwao?

Wewe umepinga kwamba kuweka pesa UTT sio Bure. Hapo ndio hoja ilipoanzia.

Sasa kama unasema sio Bure huku ukiangazia gharama za makampuni ya simu na kutokea mfano Kwa app ni Bure, kwani mtu hawezi kwenda kuweka pesa benki kama mojawapo ya chaguzi?

Kuhusu kuelewa au kutokujua kwangu kuhusu UTT siwezi kuliongelea sana na sifikirii litaleta tija hapa ila huu ni ujumbe ulioelekezwa kwangu.

 
Hamjaelewana tu mwendelee mtakaa sawa kwene mstari mmoja
 
Mkuu, Mimi nakukosoa kidogo, hapo uliposema kuweka hela ni bure. Inategemea unatumia njia gani, Kama ni kupitia CRDB au NMB ni sahihi ni Bure,
Ila kama utatumia mitandao ya simu (Vodacom, Tigo, Airtel) kuweka hela UTT kuna makato tena makubwa tuu
Ni kweli kwa mitandao ya simu Kuna gharama kubwa, tumia bank hizo
 
Si kweli hawa jamaa wamenyooka sana, haiwezi fika huko. Kuna muda inapita hata hiyo 12%
Unabisha nini sasa!

Wewe umewekeza UTT tuanzie hapo.

Vijana wa JF mnabisha hadi raha.
 
Mkuu, Hivi ukiwa na pesa UTT kwenye mfuko wowote ule, unaweza kukopea Bank?? Nikimaanisha pesa zangu zibaki UTT ila Bank wanipe hela kufanya biashara.

Bank watahitaji document gani kama uthibitisho?
 

Uko sahihi. Hii kitu wastaafu wengi wakijielekeza huko hawatakuja kunishukuru.
 
Mimi nimewekeza hapo ila hiyo 12% sijawahi Iona naona ni kama wanaingiza 8.9% kila mwezi

Basi wewe unapigwa. UTT haina income tax. Sasa kwa nini ulipwe pungufu ya 12%? Nenda kadai hela yako bro
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…