Wanawake tafuteni hela mtakosa wachumba.
Nilikutana na huyu mwanamke miaka ya nyuma huko.
Akawa abakuja gheto anapika,anafua,usafi anafanya na moto nampelekea.
Hakuwa na makuu kivile ila alikuwa na simu kali kuliko yangu,akivaa anapendeza sana nikasema mke ndio huyu twende kwenu.
Tukaenda kwao Singida ,kutoka Singida mjini hadi kwao ni masaa sita,kata inaitwaje sijui ila ni kabila la wanyisanzu,nilichokiona sikuamini,kwanza kijiji hakina mtandao wa simu mpaka upande kichuguuni,maji ya kunywa yana rangi ya chai ya maziwa,choo cha shimo hakina mlango ukisikia mtu anakuja unakohoa ili ageuze,
Kitanda cha kamba,kajumba kenyewe ukipiga teke kanadondoka.
Baada ya kurudi mjini nilifuta namba yake palepale.
Mimi ninaamini umasikini kama sio laana basi ni ufala
Sitaki wanangu wazaliwe kwenye familia yenye laana ya umasikini au ufala .
Wanawake tafuteni hela.
Na nyie makamanda mnaoa watoto masikini mna akili kweli,watoto wa kishua hamuwaoni?