Niliamua kumuacha huyu 'wife material' sababu ya umasikini wa kwao

Niliamua kumuacha huyu 'wife material' sababu ya umasikini wa kwao

Wanawake tafuteni hela mtakosa wachumba.

Nilikutana na huyu mwanamke miaka ya nyuma huko.
Akawa abakuja gheto anapika,anafua,usafi anafanya na moto nampelekea.

Hakuwa na makuu kivile ila alikuwa na simu kali kuliko yangu,akivaa anapendeza sana nikasema mke ndio huyu twende kwenu.

Tukaenda kwao Singida ,kutoka Singida mjini hadi kwao ni masaa sita,kata inaitwaje sijui ila ni kabila la wanyisanzu,nilichokiona sikuamini,kwanza kijiji hakina mtandao wa simu mpaka upande kichuguuni,maji ya kunywa yana rangi ya chai ya maziwa,choo cha shimo hakina mlango ukisikia mtu anakuja unakohoa ili ageuze,
Kitanda cha kamba,kajumba kenyewe ukipiga teke kanadondoka.

Baada ya kurudi mjini nilifuta namba yake palepale.
Mimi ninaamini umasikini kama sio laana basi ni ufala

Sitaki wanangu wazaliwe kwenye familia yenye laana ya umasikini au ufala .

Wanawake tafuteni hela.
Na nyie makamanda mnaoa watoto masikini mna akili kweli,watoto wa kishua hamuwaoni?
Binafsi nilishakataa kuoa au kuchepuka na mwanamke ambaye hana akili wala elimu hamna kichwani, Wanawake wa hivyo ni mzigo tu unajilimbikizia akuuee
 
Mtoa mada hutokaa upate mwanamke Bora kuliko yule uliyefuta number Yake kwenye Simu yako.

Utaendelea kupigwa matukio mixer kufilisishwa na wanawake mpaka siku unaondoka Duniani.Nakuapia.
We mwenyewe sikujui ila nina uhakika kuna wanawake uliwatamani ukawakisa sababu walikuona hauna uwezo,sijui lakini nahisi tu
 
We mwenyewe sikujui ila nina uhakika kuna wanawake uliwatamani ukawakisa sababu walikuona hauna uwezo,sijui lakini nahisi tu
Kutamani Ni sehemu ya maisha ya mwadamu.Na kwa taarifa yako Ni kwamba sio kila unachokitamani lazima ukipate.

Wapo matajiri wengi Sana waliogongewa wake zao na shamba boys wao.Usijifanye unawaelewa Sana Hawa wanawake kuwaliko watu wengine.

Japokuwa story yako Ni ya kutunga Ila kaa ukijua kamwe hutokuja kuwaelewa Hawa wanawake hata siku moja.
 
Yesu ana pepo!?

"Amin amin nakuambia mimi hamnami siku zote lakini maskini watakuwepo hata ukamilifu wa dahari"

Maskini WAPO watakuwepo Hadi Mwisho wa Dunia!

CHUKUA hiyo itakusaidia!

Halafu kuna HUU ujinga unaitwa "tafuta pesa" kana kwamba ukipata pesa utapata ridhiko la nafsi na Roho ni ujinga sana mkuu!!

Unajisikiaje unapotambua Kuwa huyo mwenzi ulienae alikupendea pesa au uwezo fulani!unajisikiaje!?kwani we ni roboti la kuchapisha noti!?yaani WEWE huna cha maana ulichomvutia huyo ulienae ni pesa tu,yaani pesa ina thamani kuliko muonekano na utu wako!?

Binafsi huwa nahisi mnyonge Sana nikigundua Kuwa nakubalika kwasababu ya materials badala ya my uniqueness!

Naumia sana mkuu, SIPATI ridhiko kwa mvuto wa materials!
Yesu aliwapenda masikini ila hakupenda umasikini
Ukuwa na pesa hata ukiachwa maumivu yake sio sawa na hoehae
Mwenye pesa anaweza kuoa muda wowote,au hata kununua penzi kuridhisha nafsi yake tu
 
Wanawake tafuteni hela mtakosa wachumba.

Nilikutana na huyu mwanamke miaka ya nyuma huko.
Akawa abakuja gheto anapika,anafua,usafi anafanya na moto nampelekea.

Hakuwa na makuu kivile ila alikuwa na simu kali kuliko yangu,akivaa anapendeza sana nikasema mke ndio huyu twende kwenu.

Tukaenda kwao Singida ,kutoka Singida mjini hadi kwao ni masaa sita,kata inaitwaje sijui ila ni kabila la wanyisanzu,nilichokiona sikuamini,kwanza kijiji hakina mtandao wa simu mpaka upande kichuguuni,maji ya kunywa yana rangi ya chai ya maziwa,choo cha shimo hakina mlango ukisikia mtu anakuja unakohoa ili ageuze,
Kitanda cha kamba,kajumba kenyewe ukipiga teke kanadondoka.

Baada ya kurudi mjini nilifuta namba yake palepale.
Mimi ninaamini umasikini kama sio laana basi ni ufala

Sitaki wanangu wazaliwe kwenye familia yenye laana ya umasikini au ufala .

Wanawake tafuteni hela.
Na nyie makamanda mnaoa watoto masikini mna akili kweli,watoto wa kishua hamuwaoni?
Mtoa mada, wanawake wanakufa na ww leo[emoji23]
 
Bora msema ukweli....kuliko atakaekuoa ivoivo na kukuanza kukudharau ndani coz of hali duni yenu.Yupo sahihi
Tatizo sio mtu ananini mkononi.muhimu ni mtu ana ndoto gani.

Hogopa sana mtu mwenye ndoto.dharau kila mtu lakini katika maisha yako usithubutu kumdharau mtu mwenye ndoto.

Yes naweza oana na masikini kapuku…wa fedha lakini lakini kama hana ndoto kwangu ni mzigo
 
Acha kukufuru mkuu,,hujafa hujaumbika,,kesho yako unaijua??? Mwenyezi Mungu ndo anayepanga,,,hukupaswa kumfanyia hivo huyo mwanamke,,kama mate imeniuma sana,,,hicho ulichobarikiwa na Mwenyezi Mungu ungejaribu tu kurekebisha hata choo ukweni,,,ingekuwa baraka sana,,kamwe usirudie kumtusi maskini please hujui kusudi la Mungu katika maisha yao,,hawajapenda kuwa ivo tafadhali sana ndugu yangu kwa hilo.
 
Mkuu huyo mwanamke ungepambana naemwanzo mwisho umeshindwa kumalizia hicho choo au kupeleka kitanda..
Hata mibaraka ingekufata na labda mafanikio yao yanapitia kwako..
Unaoa tajiri ila wewe ndio unaolewa na ukoo mzima
Mshukuru mungu sana hamna aliyeomba kuwa maskini
Simu ya laki tano mjini,kijijini huna choo???
 
Back
Top Bottom