Niliamua kumuacha huyu 'wife material' sababu ya umasikini wa kwao

Binafsi nilishakataa kuoa au kuchepuka na mwanamke ambaye hana akili wala elimu hamna kichwani, Wanawake wa hivyo ni mzigo tu unajilimbikizia akuuee
 
Mtoa mada hutokaa upate mwanamke Bora kuliko yule uliyefuta number Yake kwenye Simu yako.

Utaendelea kupigwa matukio mixer kufilisishwa na wanawake mpaka siku unaondoka Duniani.Nakuapia.
We mwenyewe sikujui ila nina uhakika kuna wanawake uliwatamani ukawakisa sababu walikuona hauna uwezo,sijui lakini nahisi tu
 
We mwenyewe sikujui ila nina uhakika kuna wanawake uliwatamani ukawakisa sababu walikuona hauna uwezo,sijui lakini nahisi tu
Kutamani Ni sehemu ya maisha ya mwadamu.Na kwa taarifa yako Ni kwamba sio kila unachokitamani lazima ukipate.

Wapo matajiri wengi Sana waliogongewa wake zao na shamba boys wao.Usijifanye unawaelewa Sana Hawa wanawake kuwaliko watu wengine.

Japokuwa story yako Ni ya kutunga Ila kaa ukijua kamwe hutokuja kuwaelewa Hawa wanawake hata siku moja.
 
Yesu aliwapenda masikini ila hakupenda umasikini
Ukuwa na pesa hata ukiachwa maumivu yake sio sawa na hoehae
Mwenye pesa anaweza kuoa muda wowote,au hata kununua penzi kuridhisha nafsi yake tu
 
Mtoa mada, wanawake wanakufa na ww leo[emoji23]
 
Bora msema ukweli....kuliko atakaekuoa ivoivo na kukuanza kukudharau ndani coz of hali duni yenu.Yupo sahihi
Tatizo sio mtu ananini mkononi.muhimu ni mtu ana ndoto gani.


Hogopa sana mtu mwenye ndoto.dharau kila mtu lakini katika maisha yako usithubutu kumdharau mtu mwenye ndoto.


Yes naweza oana na masikini kapuku…wa fedha lakini lakini kama hana ndoto kwangu ni mzigo
 
Acha kukufuru mkuu,,hujafa hujaumbika,,kesho yako unaijua??? Mwenyezi Mungu ndo anayepanga,,,hukupaswa kumfanyia hivo huyo mwanamke,,kama mate imeniuma sana,,,hicho ulichobarikiwa na Mwenyezi Mungu ungejaribu tu kurekebisha hata choo ukweni,,,ingekuwa baraka sana,,kamwe usirudie kumtusi maskini please hujui kusudi la Mungu katika maisha yao,,hawajapenda kuwa ivo tafadhali sana ndugu yangu kwa hilo.
 
Simu ya laki tano mjini,kijijini huna choo???
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…