Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Na kama amekutusi mbele ya watoto? Hii inakuaje mkuu. Ukizingatia unafundisha watoto kutotumia lugha ya matusiMara nyingine tatizo sio kumpiga ila kumpiga mbele ya watoto. Kama baba wa huyo jamaa angekua anampiga mama yake chumbani unafikiri huyo jamaa angejuaje? Kumpiga tu mwanamke sio vzr lakni kumpiga mwanamke mbele ya watoto wenu ni kumdhalilisha kukubwa mno.
Mkuu...lakini hoja ni kupiga mbele ya watoto..Haijazungumzia maswala ya kutopiga kabisaa..Yaani unampiga mkeo huku watoto wanashuhudia..kabla sijaoa niliwaona wanaume wote waliooa ambao wanawapiga wake zao hawana akili na wala hawana upendo kwa wake zao, nilipoingia kwenye ndoa nikagundua walikuwa na akili na mapenzi ya dhati, ila za kuambiwa changanya na zakwako
Hilo ni kosa kupiga mbele ya watotoMkuu...lakini hoja ni kupiga mbele ya watoto..Haijazungumzia maswala ya kutopiga kabisaa..Yaani unampiga mkeo huku watoto wanashuhudia..
Huwezi kuzuia kosa kwa kufanya kosa jingine mkuu. Mwanamke kukutukana tu ni kosa achilia mbali kukutukana mbele ya watoto, lakin njia ya kumzuia asikutukane tena sio kumpiga mbele za watoto ukifanya hivyo utakua unatengeneza mfumo wa jino kwa jino kati yenu. Kama umeona kuwa hana busara basi wewe tumia busara.Na kama amekutusi mbele ya watoto? Hii inakuaje mkuu. Ukizingatia unafundisha watoto kutotumia lugha ya matusi
Mkuu pole kwa unachopitia. Mara Fulani wanaume pia wanafanyiwa vitu vibaya na wanawake kiasi Cha kuchukia rohoni. Inawezekana kabisa mama yako alifanya usaliti uliomfanya baba yako awe na wasiwasi na uhalali wa kizazi chake. Hapo ndio shida inapoanza kwa mwanaume. Mtoto anakuwa muhanga wa kukosa kupata upendo na malezi kutokana na huo wasi wasi na hasa anapokosa kufanana na baba.Binafsi na mimi niko na hii hali,simkubali kabisa mzee wangu kwani sijawahi kuyajua mapenzi yake kwangu wala malezi yake ningali mdogo...mama hakuniambia mambo mengi kuhusu baba ila nilipomaliza darasa la saba na kwenda kwake ili ikiwezekana aniendelele kielimu ilitosha kabisa kunionyesha baba yangu ananichukuliaje.
Sasa wewe unadhani ni jina au ID inayo-matter hapa au content ya kuwa unatoa siri za watu. Unajuaje kama jamaa yupo humu unadhani atakuchukulia wewe ni rafiki wa namna gani?Ndio maana tunatumia fake ID mkuu..halafu huu so umbea, ni mijadala ya kujifunza...Karibu na endelea kufurahia umbea mkuu.
Samahani mkuu ila mara nyingine mama zetu huwa wanakua na siri sana na nyingine huwa zinabomoa familia. Hizi mambo mtu unaoa halafu unasikia kwa watu kuwa mtoto wenu wa pili sio wako huwa zinachanganya kweli kweli. Hivi umewahi kujiuliza kwa nini baba alikutenga? Au kuna vitu ulifanya haujatueleza humu mkuu?Binafsi na mimi niko na hii hali,simkubali kabisa mzee wangu kwani sijawahi kuyajua mapenzi yake kwangu wala malezi yake ningali mdogo...mama hakuniambia mambo mengi kuhusu baba ila nilipomaliza darasa la saba na kwenda kwake ili ikiwezekana aniendelele kielimu ilitosha kabisa kunionyesha baba yangu ananichukuliaje.
Alisomesha watoto wake wengine na kuwajali pia...mambo yake yalipoanza kuyumba aliamua kuuza nyumba yake (Tandale) na akawapa watoto wake wengine (wadogo zangu) almost 2M kila mmoja but mimi sikukumbukwa hata kwa buku.
Watoto aliowathamini leo hii hawamjali,mzee ameamua kurudi kwangu na kuhitaji msaada kila leo..mimi mwenyewe sina kipato cha kutosheleza maana nakomaa na wanangu wapate elimu iliyo bora.
Inafika mahali sipokei kabisa simu zake,najitahidi kusahau na kusamehe lakini kutokana na niko na kipato duni inakuwa ngumu sana kusahau aisee.
Swala sio kupiga !!Nasikitika ninyi wawili mliokomenti hamjamuelewa mtoa mada
Nakubali kabisa kuna makosa akina mama hufanya ambayo hupelekea utengano au kupandikiza chuki toka kwa baba kwenda kwa mama na mama kumlisha sumu mtoto baba.Samahani mkuu ila mara nyingine mama zetu huwa wanakua na siri sana na nyingine huwa zinabomoa familia. Hizi mambo mtu unaoa halafu unasikia kwa watu kuwa mtoto wenu wa pili sio wako huwa zinachanganya kweli kweli. Hivi umewahi kujiuliza kwa nini baba alikutenga? Au kuna vitu ulifanya haujatueleza humu mkuu?
Nimekupa like mkuuAmekua au bado mvulana?? Anaisha na mwanamke?
Hajawahi mchapa mwanamke yoyote hata kibao??
Kama hajawahi good for him ila kama keshawahi ajue huyo mwanamke ni mama wa mtu na yeye atachukiwa tu.
Hawa watoto wakifanikiwa ndio wanajifanya wanachuki ma wazazi
PUMBAAAAAVU SANA.
Ndio mambo ya akina SADALA
Uko sahihi kabisa mkuu, cha kufanya ni hivii..kama kweli baba una mapenzi na watoto wako utavumilia kila aina ya kioja ili tu watoto wapate kukua katika malezi ya pande zote mbili,. Ni hivyo tuu vinginevyo tutakuwa tunatengeneza jamii iliyojaa chuki.Mkuu pole kwa unachopitia. Mara Fulani wanaume pia wanafanyiwa vitu vibaya na wanawake kiasi Cha kuchukia rohoni. Inawezekana kabisa mama yako alifanya usaliti uliomfanya baba yako awe na wasiwasi na uhalali wa kizazi chake. Hapo ndio shida inapoanza kwa mwanaume. Mtoto anakuwa muhanga wa kukosa kupata upendo na malezi kutokana na huo wasi wasi na hasa anapokosa kufanana na baba.
Kuna mambo yanafanyika ila athari zake huja huonekana baada ya muda mrefu sana..Ukifatilia asilimia kubwa watoto wanakuwa na migogoro na baba zao kuliko mama zao...Yaani ukisikia mtoto ana bifu na mzazi mmoja au amemtelekeza, basi asilimia 99% ya mzazi aliyetelekezwa anakuwa ni Baba...Moja kwa moja hisia za wengi huwa tunaw.
Nimekuwa nikishuhudia mama anadundwa vilivyo na mshua kiukweli ilikuwa inaniuma sana pia, hata mimi nilimchukia sana mzee sema ndo nilikuwa namtegemea kwa kila kituMara nyingine tatizo sio kumpiga ila kumpiga mbele ya watoto. Kama baba wa huyo jamaa angekua anampiga mama yake chumbani unafikiri huyo jamaa angejuaje? Kumpiga tu mwanamke sio vzr lakni kumpiga mwanamke mbele ya watoto wenu ni kumdhalilisha kukubwa mno.