Nilibahatika sikupitia njia hii ila najua ni njia inayowaumiza sana watoto kisaikolojia na kuwaacha na chuki kwa wazazi

Mwanamke wa kibongo bila makofi ndoa haifiki mbali, hivyo vibao ndio vimesaidia wazazi wetu hata wazazi wa huyo jamaa kudumu kwenye ndoa, piga makofi tafadhali utakuja kunishukuru
Ukiona hivyo ndiyo umelelewa kwenye taswira hiyo.
Sisi wengine tumelelewa na wazazi ambao hawajawahi kupigwa wala kupigana.
 
Huyo chalii yako bado mvulana, ngoja akinyooshwa na mkewe akili zitamrejea.
Hivi unajua kipigo cha mume kwa mke hakinaga huruma ye anapiga ilimradi amkomeshe aue asiue, vyote sawa, imagine unashuhudia mama ako mzazi anapigwa vile afu baadaye we ndo unamkanda maji moto, na mijanaume mingine mikorofi tu mtoto anakosea afu anapigwa mama
 
Mwanamke wa kibongo bila makofi ndoa haifiki mbali, hivyo vibao ndio vimesaidia wazazi wetu hata wazazi wa huyo jamaa kudumu kwenye ndoa, piga makofi tafadhali utakuja kunishukuru
😎😎😎😕 utakuja ua mwanangu, uozee jela. Vibao sio suluhisho la kadhia za ndoa
 
Matendo yoyote ya wazazi huwa ni faida/hasara kwa watoto
 
pole sana Mungu akujalie kipato ww ushasamehe ila mambo yako bado magumu. Mwenzio nishanyimwa hela lkn nilshasamehe na nikawasomesha madogo na bado natekeleza wajibu kwake na familia yangu kwa kdg hichohicho. Nimejifunza kuwa baba ni issue sana.Kuwa kiongozi wa familia kuwa mkali, mtiifu, mnyenyekevu,mvumilivu, mtulivu, busara bila kuumiza. wazee wanakumbuka but no point of return maji yashamwagika. Samehe sahau songa mbele A humble and stronger man character. All the best.
 
mwanaume akikuta msg tu ya mahusiano kwa mkewe anahisi hata watoto sio wake...!! ndoa nyingi watu wanaishi kwa kuvumilia tu kikweli moyoni zilishakwisha au kufa....watoto ni machache sana mnayoelewa kwa wazazi wenu....kiwaheshimu wazazi ndio agizo Mungu aliloacha...ili upate siku nyingi za kuishi duniani. Kubalance mambo ndoani kazi sana...
 
issue nyingi wazee hawasemi ila wanapitia changamoto nyingi watoto mnakuja shuhudia kibano tu..mzee hawezi sema nimemfumania mama yenu....!!
 
Ahsante sana mkuu...
Ni kweli kabisa ningekuwa na kipato toshelezi ningemjali ila siko hivyo...nilichonacho nakomaa na wanangu.
 
Usilolijua ni sawa na usiku wa kiza. Ndoa haina cheti cha kuhitimu. Ina cheti cha upimaji wa awali usio na ithibati. Kua uyaone mwanangu.
 
Ni kweli kabisa...
Ndiyo maana wanasema mtoto umleavyo ndivyo akuavyo...
 
Ahsante kwa baba yangu, tena upendo wangu kwa baba hata hauna kipimo
 
Mwanaume oa mwanamke unayempenda na anayekuheshimu. Kuna ndoa nyingi ambazo hawapigani. Binafsi sikuwahi ona mzee wangu kumkejeli wala kumtukana au kumshushia heshima mama na huko kumpiga ndo kabisa sijawahi sikia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…