Tuliozaliwa kijijini na Kisha kuja mjini ukubwani aloo tunayajua maisha kinoma.
Utotoni Kwanza full kucheza porini michezo ya kujificha, kombolela, rede, kuruka kamba, kuwinda ndege, kuwinda nyani, kuchoma misitu Moto (utukutu), kutafuta uyoga, kugema ulimbo wankutegea ndege, kutega kware na tetere kwa mitego.
Kuchonga PIA, kuchonga ngorogojo (sijui Ni kkswahili sahihi??) Kuchonga magari ya udongo na magunzi.
Kuchunga mbuzi porini masafa ya mbaaaaali huko milimani na mabondeni mnakutana kundi kubwa na wachungaji mnafurahi pamoja. Kuogelea mtoni na mabwawani, kuvua samaki kwa ndoano mtoni.
Kwenda kuvua samaki kwa nyavu mnakaa porini huko wiki nzima. Kufanya vibarua vya kulima maporini hukoo mnakuwa mnalala huko kama wiki nzima. Kuwinda nyani, sungura, swala n.k kwa mbwa!!
Daaah let me go to the village next year!!!!!!