Ni changamoto kubwa katika malezi hasa kwa sisi tuliopitia vyuoni na kuna vimishahara au vifaida vya kusongesha life tunajikuta mara nyingi tunalea watoto ndivyo sivyo
1. Mwanzoni mtoto wangu alikuwa anasoma hizi shule za kutoka saa 11 na shuleni wapo wachache darasani hawazidi 20. Pia maendeleo ya social skills sikuyafurahia na hii shule ilichangia katika hili tatizo.
Pesa ya muhula mzima nilikuwa nimeshalipa ila nikamuhamisha shule nyingine ambayo wanawaigi kutoka mchana na darasani wamo kama 57 hivi, nilifanya hivi ili kupanua chances zake za kuwa na marafiki wengi maana kiukweli ile shule ya zamani alikuwa na rafiki moja tu ila kwa sasa ana marafiki wengi, na kitu kingine ike shule ya zamani ilikuwa ni masomo mtundo moja mpaka jioni hii iliminya mda wa wanafunzi kupata mda wa kujuana, hii shuke ya sasa naona wana kmjuoindi cha michezo mara 2 kika wiki, na pia muda wa wanafunzi kujuana zaidi wanapowahi kutoka mchana upo.
Nafurahi sana mwanangu kwa sasa sio mpweke sana kama zamani, shuleni pia iww sehem ya kujenga social skils sio kusoma tu darasani, nami pia kila siki za shule nahakikisha usiku nakaa nae lisaa kumsaidia masomo maana nilipewa syllabus na vitabu wanavyotymia kuwafundishia na wala havinipigi chenga.
2. School bus silipii, sioni umuhimu wake labda mwanafunzi wa mtoto asiezidi miaka mitano na shuke ipo mbali sana, Shule anayosoma mwanangu ukitembea ni mwendo wa dakika 25 tu na wapo wenzake wachache ambao hawalipii school bus wanapitaga njia hii pamoja na wenzao wengi wanaosoma shule ya serikali iliyopo karibu na shule yao, Hii hali nikaona ni kumdumaza tu mtoto hizi school bus, tangu mwaka jana anatwanga mguu na wala sijaona tatizo, Wenzake wengi pia wanaopanda school bus ananiambiaga huwa wanapenda kutembea lakini wazazi hawataki, Kutembea kuna raha yake [emoji16].
3. Akitoka shuleni inabidi afue nguo zake, kuosha vyombo atavyolia chakula, kusafisha chumba chake, n.k hivi nlimpiga stop house girl kuvifanya kwa mwanangu japo wife alipinga kudai bado wadogo ila nikamwambia silei mayai, baada ya hapo ataweza kucheza na marafiki zake hapa kwangu ama kwao kwa kutoa taarifa mapema tutamkuta nyumba ya rafiki yake yupi, zamani nlikuwa nampiga geti kali ila sikuona faida, kwa sasa amekuwa msaada mkubwa kwa wenzake mageti kali ambao kwamfano nyumba flani mzazi aliniomba mtoto wangu awe anaenda pale kila jumapili maana ni siku ambayo mtoto wake anakuwa hajabanwa na hizi shule wanazotoka saa 11 juoni, hana homework, n.k ila kwake hataki kabisa mtoto wake kutoka nje, ni jambo zuri kuwapa kampani wenzake mi nikamkubalia maana huyo mtoto ndio alikuwa best wake wa shule ya zamani na hata wazazi wake tunajuana nao na ni mfano wa familia bora yenye maadili kwa hio huwa sina shaka, japo nilimuambia mwanangu akijiona hataki au kachoka kwenda awe free kuniambia, haniogopi huwa hasiti kuniambia chochote
4. Zamani nilimwekea Playstation (game ya tv) na katuni nikijidanganya ndio vitampa kampani kama rafiki, kiukweli nilijidanganya, kwanza hii playstation ikaanza kumpa kama uraibu flani wa kuwa teja, yani akisikia playstation anakuwa kama teja hivi, weekend ukifika ndo kabisa anaweza kushinda hapo kwenye screen hadi mnashangaaa. Kiukweli nikaona hizo kampani zake za katuni na magem yatamuharibu na kumfanya afikirie katika ulimwengu ambao haupi kama huo w akwene game na katuni, Ikabidi nimletee mpira awe anacheza cheza nje maana alikuwa anashinda sana ndani, ile game nikaficha nikamdanganya ipo kwa fundi, kidogo kidogo akaanza kuzoea nje, nikamletea na ka mbwa kadogo basi akawa anakapenda sana saizi ni mbwa mkubwa wa ulinzi hapa, furaha yangu ni kumuona akiwa nje, hivi na vile nikaamwamisha shule akaanza kuwa na marafiki kadhaa, nikaacha kulipia schoolbus ili awe ananyoosha vimiguu, n.k basi ndo namimi nafurahi hapo
5. Kuna kipindi flani nilipokuwa naenda kijijini (ni mwendo wa saa moja toka napishi) kwenye vikao hivi na kuwajulia hali ndugu zangu, nilikuwa naenda na huyu mwanagu nae, navyoendelea na shughuli zangu alikuwa anachangamana na wenzake, akiwa huko na wenzake aliweza kufundishwa kujipikia ugali maana kule kijijini kujipikia ni kitu cha lazima kukijua, Hii hali inamwandaa mapema hata atakapoanza maisha yake asiwe mpya kwenye kujilisha, Mke wangu hili jambo mwanzoni alichukizwa nalo sana na kuanza kuniambia mtoto wetu hafai kupika hadi awe mkubwa kwa sasa asome tu lakini kwangu nilipingana nae nikamwambia hakuna tatizo mtoto wetu kujua kupika, ipo siku atahitaji hiki alichojifunza, Hpa fundisho kuu ni kwamba mtoto inabidi ajue kujilisha, Isiwe tu kwa watoto wa kike bali hata wa kume.
6. Michezo - hapa kwanza kabisa nianze na kuelezea kwambaniliwahi kugharamie ajifunze kuogelea, maana kule kijijini nilihofia kuna siku wataenda huko mtoni na majanga yakampata, kwa hio nilichukua hii precaution haraka, Nawaasa sana wazazi mambo kama kuogelea msiyapuuze, ni kitu kinachweza kuokoa maisha ya mwanao au yeye kuokoa maisha ya wengine. Kitu kungine kwa kuchangamana na wezake huku kwetu na shuleni ameweza kuwa mchezaji mzuri tu wa mpira ni kitu kizuri ila pia kijijini kule alifundishwa hizi sarakasi aliteguka mkono mama yake tuligombana sana hii ishu, ila hakuacha aliendelea na kufanikiwa kuweza kuruka hizi sarakasi, Mwaka jana siku ya wazazi wanapofunga shule nilipata kujisikia vizuri nilipomuona mwanagu akiwa anaonyesha ujuzi wake mwele ya umati wa wanafunzi na wazazi tuliofika hapo, Ni jambo lililonifurahisha na hata marafiki zangu na wa mke wangu walipoona zile video tulipewa visifa kidgo, basi hata wife zile hasira zake za mtoto kujifunza sarakasi zikawa zinashuka
7. Kuhusu kumlimbikizia kazi house girl mbazo ni wajibu wa mtoto kuzifanya nimezingatia hili suala japo tumekorofishana sana na mke wangu anaetaka housegirl afanye karibu kila kitu watoto wakae tu, Binafsi nilikataa kabisa huu mpango na mtoto ameshauzoea na umekuwa na tija kwake kujua mapema kwamba maisha ni majukumu, Hata hivyo leo hii au kesho hali yetu inaweza ikawa mbaya watoto wakapata wakati mgumu maana hakutauwa na house girl, Ni kwamba kwa sasa kazi zilizokuwa zinafanywa na house girla anazifanya huyu mwanangu ama awanapeana zamu inapobidi baadhi ya kazi ni : Kabla hajalala inabidi apasi nguo zake, Inabidi atandike kitanda chake kila siku, asafishe chumba chake, akitoka shuleni afue uniform zake, Asubuhi akiamka anafagia uwanja kwa zamu na house girl leo yeye kesho hause gerl, Viombo anavyolia inabidi aoshe yeye, n.k Mwanzoni alikuwa mgumu ila nilimfundisha, na alipokuwa mzembe nilimuonya, na aliporudia uzembe bakora ilitumika.
8. Matumizi ya bakora yanatumika kwa sasa mwanangu napomfundisha kitu flani, akarudia nikamuonya, akarudia tena nikamkaripia ila akiendelea kuna viboko vya mpera, Matumizi ya viboko kwa usahihi ni muhimu sana katika malezi ya watoto, Yapasa atambue kuna madhara ya kutofata anachofundishwa na wazazi wake na kutokiheshimu, Hii pia hata akiwa mkubwa anajitegemea atakuwa anajua kabisa kwamba asipofata hizi sheria jela inamhusu au atafunzwa na walimwengu, Wazazi msipuuzie viboko hivi, kuna maana kubwa sana vimeruhusiwa kutumika hata kwenye biblia na korani na hata kutumuka vizazi hadi vizazi hadi hapa tulipo, haya malezi ya wazungu mnayoyaiga ni kuacha asili yenu, Narudi tena tuvitumie viboko kwa njia sahihi sio kila mda unapiga tu.