ruaharuaha
JF-Expert Member
- Feb 14, 2018
- 3,586
- 3,857
Kila kitu. Changamoto, wahuni watakuwepo. Muhimu kujua how to deal with them.Ngangari wa nini?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kila kitu. Changamoto, wahuni watakuwepo. Muhimu kujua how to deal with them.Ngangari wa nini?
kukulia kijijini ndio kuyajua maisha,Mara nyingi hua naona watoto wanaokua na akili za maisha ni wale haswa waliokulia kijijini na kusoma huko angalau mpaka std 7. Huyu akija kutoka huko akaja mjini humuambii kitu maisha anakua anayajua hasa.
Hawa wanaoenda mara moja moja kipindi cha krismasi sawa sio mbaya sana ila ukute na yeye mtoto ana akili kichwani. Wengine wakifika vijijini ndio anaanza kujikuta supastaa kila kitu anajua yeye na maneno mengi kama chiriku. Akiamka asubuhi anaoga na kuvaa raba anaanza kuzunguka zunguka tu kama mtalii.
Olu in olu ni vizuri mzazi kumu ekspozi mtoto kwenye hali tofauti tofauti za maisha.y
Hii ni experience ya kujiProud kweli, nothing to offer in our future just a wild life.Hahahaha watoto wa sikuizi wanakosa sana haya maajabu.
Hapo kuzurula hosptal na kuokota sindano.
Nakumbuka jion moja tukaenda kuzurula maeneo ya kituo cha afya, timu ya vijana si chini ya saba na mbwa watatu.
Kando kando tunapitachocho hapa na hapa
Tukaona mbwa anakuja na kitu kama linyama hivi,sasa wakati anatusogelea kuna midewife mmoja (hakua zamu ila anakaa kota)akamuona mbwa yule akatuambia tumuamuru yule mbwa aache au tumnyang'anye hilo linyama na tulifukie haraka.
Hatukua wabishi tukafanya hivyo.
Kesho yake shule tukaitwa na mwalimu akatuonya kutembelea mazingira hatarishi huko hosptali tuache.
Akatuuliza mnajua yule mbwa jana alibeba nini,tukamwambwia hatujui.
Akasema ni kondo.
Mbwa alifukua mahali lilipotupwa na kufukuwa kondo la uzazi.
Hata sikuelewa kondo ni nini nilikuja kuelewa nipo darasa la sita,kwenye somo la sayansi.
Tuashateleza sana kwny mizambarao..
Tumekwea hadi mipapai...😂😂
Kuna rafiki yangu alishawahi niambia - kuna umuhimu wa kuinvest kwenye elimu ya watoto wako hata kama ni shule nzuri ukiweza kama Aga Khan etc. hata kwa kujinyima. Nikamuuliza kwa nini...alinielezea vizuri sana.. shule hizi zina watoto wa influencers na tukubali tukatae ni muhimu kuinvest kwenye social networking(ambayo inatofauti kubwa na socializing) maana mtoto wako anaanza kujijengea hazina ya watu muhimu akiwa mdogo. Na kumbuka lasting friendships and connections zinaanzia huko siyo chuo kikuu ambako ni too artificial.Waafrika huwa wanajiandaa kuishi maisha duni. Mtoto akipelekwa shule nzuri kila mtu anashangaa... roho ya umaskini.
Punguani.Hii ni experience ya kujiProud kweli, nothing to offer in our future just a wild life.
Ndio yeye ni low class inawezekana wewe high class unakojoa soda na kunya keki hongera mkuu.Mleta mada inaonyesha unakaa eneo la low class kwa Walala hoi ila wewe una kanafuu kidogo ni kama wewe ni katajiri fulani katikati ya maskini kwa ulivyojieleza lakini ungekuwa unakaa high class areas hicho ulichoandika chote ni hopeless mfano hakuna mtoto high class anatembea kwa miguu dakika 25 kwenda shule
Uko sahihi nina jirani nilikuwa nakaa alikuwa na binti mmoja tu akampeleka international school ada mamilioni nikauliza kwa nini na yeye mbona anaishi mtaani maisha ya kawaida akasema wanataka mwanae mbeleni aolewe na watoto wa matajiri sio vidume vya mtaani ni kweli alifanikiwa mwanae kaolewa uswisi na mswisi waliyesoma wote international school kule kuna watoto wa decision makers kwenye society hata mtoto Mara ingine kukosa kazi sio rahisi unakuta ni rafiki wa mtoto wa bakhreesa , mtoto wa bosi fulani nk tofauti na mtaani hao watoto wa decision makers hawapatikani shule za kawaida ndio maana wazazi wengine hujinyima sana ili watoto wao wasogee jaribu wakae na kufanya urafiki na watoto wa decision makers kwenye societyKuna rafiki yangu alishawahi niambia - kuna umuhimu wa kuinvest kwenye elimu ya watoto wako hata kama ni shule nzuri ukiweza kama Aga Khan etc. hata kwa kujinyima. Nikamuuliza kwa nini...alinielezea vizuri sana.. shule hizi zina watoto wa influencers na tukubali tukatae ni muhimu kuinvest kwenye social networking(ambayo inatofauti kubwa na socializing) maana mtoto wako anaanza kujijengea hazina ya watu muhimu akiwa mdogo. Na kumbuka lasting friendships and connections zinaanzia huko siyo chuo kikuu ambako ni too artificial.
Ndio yeye ni low class inawezekana wewe high class unakojoa soda na kunya keki hongera mkuu.
Mmm kuna ukweli fulani mfano Dar unakuta mbezi beach au msasani au Masaki kote huko kuna watu wana mabanda ya kufuga kuku,ngombe na nguruwe kwenye makazi na watu wana magenge ya kuuza mboga na karanga za shilingi 100Kwanza hapa Tanzania kuna eneo lolote la kuitwa high class? 😂
Aibu nimeona. MimiUko sahihi nina jirani nilikuwa nakaa alikuwa na binti mmoja tu akampeleka international school ada mamilioni nikauliza kwa nini na yeye mbona anaishi mtaani maisha ya kawaida akasema wanataka mwanae mbeleni aolewe na watoto wa matajiri sio vidume vya mtaani ni kweli alifanikiwa mwanae kaolewa uswisi na mswisi waliyesoma wote international school kule kuna watoto wa decision makers kwenye society hata mtoto Mara ingine kukosa kazi sio rahisi unakuta ni rafiki wa mtoto wa bakhreesa , mtoto wa bosi fulani nk tofauti na mtaani hao watoto wa decision makers hawapatikani shule za kawaida
Kua careful sana na jamii inayokuzunguka
Usije uka trust jamii inayokuzunguka
Wewe ndio una best interest na mtoto wako kuliko anybody else
Hiyo jamii inayokuzunguka sio kwamba inakupenda sana na hao watoto wako zaidi yao wao binafsi
Na pia hizo vurugu za kusema namlundika mtoto wangu na watoto wa watu wengine ajifunze kitu,usije fanya kwa kuforce au ujanja ujanja
Familia au majirani wanatembeleana formally,siku maalumu kwa mwaliko maalumu,sio unavamia nyumba za watu na mtoto wako sio unamkurupua avamie nyumba za watu
Watoto wakutane sehem maalumu za mikusanyiko kama playground,kwenye sports,street plays,riding,etc
Hii tabia mbovu ya kuvamia vamia majumba ya watu kutaka ukoo ili mtoto wako ajuane na watu ni nonsense....
Mfundishe mtoto wako to treat all people with respect atapata marafiki tu...
Mambo mengine ya kuvamia jamii na kutaka ukoo kwa kuforce au ku plan ni nonsense maana watoto wako watakuja kuishi kwa upungufu maana maisha yao yote watakua wana fight kutafuta acceptance kwenye jamii,which is a source of all evils!
Tatizo lenu mnadhani SHIDA mlizopata nyie mnataka na watoto wenu wazipate as if hizo shida zilikusaidia.SHIDA hazisaidii ndio maana zikaitwa SHIDA to begin with.
Concept ya kuhamisha SHIDA ulizopata kipindi unakua kama kutembea bila viatu na kukaa darasa lenye watoto 60 desk moja wanakaa watoto 12,mtu anakua na muandiko mbovu mpaka anakuja kua Engineer muandiko ni mbovu au mgongo umepinda mpaka ukubwani nyie mnadhani ni faida
Nonsense
Huu mtaala wa primary umemshinda dada angu kwa watoto wake wawili mpaka wanafika form two mdogo na form four mkubwa wa kiume. Dogo la kiume ni jeuri na dharau nyingi mpaka kufikia hatua ya kuwaambia walimu kuwa hawajui kiingereza sahihi kisa yeye na dada ake wamesoma international primary school baada ya kufauru Std. Seven na kupangiwa shule za serikali.Ningeshangaa kama huo mtaala wa primary ungekupig chenga.
Asante sana mkuu kwa huu uzi, nimescreenshot baadhi ya sehemu na kumtumia sister yuko ughaibuni na watoto wake wapo hapa nchini. Wakati yupo aliwalea kama mayai, Ila sasa wapo chini ya uangalizi wangu. Sijawahi ona eti Kuna tv ya sitting room alafu unanunua tv nyingine inakaa chumbani kwa mtoto wa kiume kwaajili yakuchezea PlayStation games akiwa likizo toka shuleni😬Ni changamoto kubwa katika malezi hasa kwa sisi tuliopitia vyuoni na kuna vimishahara au vifaida vya kusongesha life tunajikuta mara nyingi tunalea watoto ndivyo sivyo
1. Mwanzoni mtoto wangu alikuwa anasoma hizi shule za kutoka saa 11 na shuleni wapo wachache darasani hawazidi 20. Pia maendeleo ya social skills sikuyafurahia na hii shule ilichangia katika hili tatizo.
Pesa ya muhula mzima nilikuwa nimeshalipa ila nikamuhamisha shule nyingine ambayo wanawaigi kutoka mchana na darasani wamo kama 57 hivi, nilifanya hivi ili kupanua chances zake za kuwa na marafiki wengi maana kiukweli ile shule ya zamani alikuwa na rafiki moja tu ila kwa sasa ana marafiki wengi, na kitu kingine ike shule ya zamani ilikuwa ni masomo mtundo moja mpaka jioni hii iliminya mda wa wanafunzi kupata mda wa kujuana, hii shuke ya sasa naona wana kmjuoindi cha michezo mara 2 kika wiki, na pia muda wa wanafunzi kujuana zaidi wanapowahi kutoka mchana upo.
Nafurahi sana mwanangu kwa sasa sio mpweke sana kama zamani, shuleni pia iww sehem ya kujenga social skils sio kusoma tu darasani, nami pia kila siki za shule nahakikisha usiku nakaa nae lisaa kumsaidia masomo maana nilipewa syllabus na vitabu wanavyotymia kuwafundishia na wala havinipigi chenga.
2. School bus silipii, sioni umuhimu wake labda mwanafunzi wa mtoto asiezidi miaka mitano na shuke ipo mbali sana, Shule anayosoma mwanangu ukitembea ni mwendo wa dakika 25 tu na wapo wenzake wachache ambao hawalipii school bus wanapitaga njia hii pamoja na wenzao wengi wanaosoma shule ya serikali iliyopo karibu na shule yao, Hii hali nikaona ni kumdumaza tu mtoto hizi school bus, tangu mwaka jana anatwanga mguu na wala sijaona tatizo, Wenzake wengi pia wanaopanda school bus ananiambiaga huwa wanapenda kutembea lakini wazazi hawataki, Kutembea kuna raha yake 😁.
3. Akitoka shuleni inabidi afue nguo zake, kuosha vyombo atavyolia chakula, kusafisha chumba chake, n.k hivi nlimpiga stop house girl kuvifanya kwa mwanangu japo wife alipinga kudai bado wadogo ila nikamwambia silei mayai, baada ya hapo ataweza kucheza na marafiki zake hapa kwangu ama kwao kwa kutoa taarifa mapema tutamkuta nyumba ya rafiki yake yupi, zamani nlikuwa nampiga geti kali ila sikuona faida, kwa sasa amekuwa msaada mkubwa kwa wenzake mageti kali ambao kwamfano nyumba flani mzazi aliniomba mtoto wangu awe anaenda pale kila jumapili maana ni siku ambayo mtoto wake anakuwa hajabanwa na hizi shule wanazotoka saa 11 juoni, hana homework, n.k ila kwake hataki kabisa mtoto wake kutoka nje, ni jambo zuri kuwapa kampani wenzake mi nikamkubalia maana huyo mtoto ndio alikuwa best wake wa shule ya zamani na hata wazazi wake tunajuana nao na ni mfano wa familia bora yenye maadili kwa hio huwa sina shaka, japo nilimuambia mwanangu akijiona hataki au kachoka kwenda awe free kuniambia, haniogopi huwa hasiti kuniambia chochote
4. Zamani nilimwekea Playstation (game ya tv) na katuni nikijidanganya ndio vitampa kampani kama rafiki, kiukweli nilijidanganya, kwanza hii playstation ikaanza kumpa kama uraibu flani wa kuwa teja, yani akisikia playstation anakuwa kama teja hivi, weekend ukifika ndo kabisa anaweza kushinda hapo kwenye screen hadi mnashangaaa. Kiukweli nikaona hizo kampani zake za katuni na magem yatamuharibu na kumfanya afikirie katika ulimwengu ambao haupi kama huo w akwene game na katuni, Ikabidi nimletee mpira awe anacheza cheza nje maana alikuwa anashinda sana ndani, ile game nikaficha nikamdanganya ipo kwa fundi, kidogo kidogo akaanza kuzoea nje, nikamletea na ka mbwa kadogo basi akawa anakapenda sana saizi ni mbwa mkubwa wa ulinzi hapa, furaha yangu ni kumuona akiwa nje, hivi na vile nikaamwamisha shule akaanza kuwa na marafiki kadhaa, nikaacha kulipia schoolbus ili awe ananyoosha vimiguu, n.k basi ndo namimi nafurahi hapo
5. Kuna kipindi flani nilipokuwa naenda kijijini (ni mwendo wa saa moja toka napishi) kwenye vikao hivi na kuwajulia hali ndugu zangu, nilikuwa naenda na huyu mwanagu nae, navyoendelea na shughuli zangu alikuwa anachangamana na wenzake, akiwa huko na wenzake aliweza kufundishwa kujipikia ugali maana kule kijijini kujipikia ni kitu cha lazima kukijua, Hii hali inamwandaa mapema hata atakapoanza maisha yake asiwe mpya kwenye kujilisha, Mke wangu hili jambo mwanzoni alichukizwa nalo sana na kuanza kuniambia mtoto wetu hafai kupika hadi awe mkubwa kwa sasa asome tu lakini kwangu nilipingana nae nikamwambia hakuna tatizo mtoto wetu kujua kupika, ipo siku atahitaji hiki alichojifunza, Hpa fundisho kuu ni kwamba mtoto inabidi ajue kujilisha, Isiwe tu kwa watoto wa kike bali hata wa kume.
6. Michezo - hapa kwanza kabisa nianze na kuelezea kwambaniliwahi kugharamie ajifunze kuogelea, maana kule kijijini nilihofia kuna siku wataenda huko mtoni na majanga yakampata, kwa hio nilichukua hii precaution haraka, Nawaasa sana wazazi mambo kama kuogelea msiyapuuze, ni kitu kinachweza kuokoa maisha ya mwanao au yeye kuokoa maisha ya wengine. Kitu kungine kwa kuchangamana na wezake huku kwetu na shuleni ameweza kuwa mchezaji mzuri tu wa mpira ni kitu kizuri ila pia kijijini kule alifundishwa hizi sarakasi aliteguka mkono mama yake tuligombana sana hii ishu, ila hakuacha aliendelea na kufanikiwa kuweza kuruka hizi sarakasi, Mwaka jana siku ya wazazi wanapofunga shule nilipata kujisikia vizuri nilipomuona mwanagu akiwa anaonyesha ujuzi wake mwele ya umati wa wanafunzi na wazazi tuliofika hapo, Ni jambo lililonifurahisha na hata marafiki zangu na wa mke wangu walipoona zile video tulipewa visifa kidgo, basi hata wife zile hasira zake za mtoto kujifunza sarakasi zikawa zinashuka
7. Kuhusu kumlimbikizia kazi house girl mbazo ni wajibu wa mtoto kuzifanya nimezingatia hili suala japo tumekorofishana sana na mke wangu anaetaka housegirl afanye karibu kila kitu watoto wakae tu, Binafsi nilikataa kabisa huu mpango na mtoto ameshauzoea na umekuwa na tija kwake kujua mapema kwamba maisha ni majukumu, Hata hivyo leo hii au kesho hali yetu inaweza ikawa mbaya watoto wakapata wakati mgumu maana hakutauwa na house girl, Ni kwamba kwa sasa kazi zilizokuwa zinafanywa na house girla anazifanya huyu mwanangu ama awanapeana zamu inapobidi baadhi ya kazi ni : Kabla hajalala inabidi apasi nguo zake, Inabidi atandike kitanda chake kila siku, asafishe chumba chake, akitoka shuleni afue uniform zake, Asubuhi akiamka anafagia uwanja kwa zamu na house girl leo yeye kesho hause gerl, Viombo anavyolia inabidi aoshe yeye, n.k Mwanzoni alikuwa mgumu ila nilimfundisha, na alipokuwa mzembe nilimuonya, na aliporudia uzembe bakora ilitumika.
8. Matumizi ya bakora yanatumika kwa sasa mwanangu napomfundisha kitu flani, akarudia nikamuonya, akarudia tena nikamkaripia ila akiendelea kuna viboko vya mpera, Matumizi ya viboko kwa usahihi ni muhimu sana katika malezi ya watoto, Yapasa atambue kuna madhara ya kutofata anachofundishwa na wazazi wake na kutokiheshimu, Hii pia hata akiwa mkubwa anajitegemea atakuwa anajua kabisa kwamba asipofata hizi sheria jela inamhusu au atafunzwa na walimwengu, Wazazi msipuuzie viboko hivi, kuna maana kubwa sana vimeruhusiwa kutumika hata kwenye biblia na korani na hata kutumuka vizazi hadi vizazi hadi hapa tulipo, haya malezi ya wazungu mnayoyaiga ni kuacha asili yenu, Narudi tena tuvitumie viboko kwa njia sahihi sio kila mda unapiga tu.
Ingekuwa Ulaya au Marekani polisi wangekubeba kule viboko na vibao marufuku kwa mke au mtotoKuna siku akiwa likizo alileta za kuleta nikamchapa bakora, baada ya hapo akaenda kunishtaki polisi kuwa eti mjomba kanichapa so waje kunikamata hapo akiwa form two😆. Polisi wakamwambia haya tangulia nyumbani sisi tunakuja.
Na sister yuko Finland sasa asitake watoto wake niwalee katika mazingira hayo. Kwanza ameshaanza kunielewa maana kazi wanafanya ila stage ya kuwapiga tangia nilipomchapa bakora akiwa form two huyu mkubwa wa kiume imewajengea hofu juu yangu kwahiyo nikiagiza kitu wanatekeleza ingawa sometimes naona kabisa wanafanya kwa shingo upande. Ni aibu mtoto wa kikeyupo form three now hata kusonga ugali hajui na kuandaa chakula mezani anaona ni usumbufu. Muda wote wakiwa home wanataka wakae mbele ya tv, wataangalia hapo mpaka jioni. Sasa maisha hayo sisi wenyewe hatujakulia, kwanini tuwaharibu Hawa watoto? Baadae mama yao asipokuwepo au uwezo alionao sasa ukapungua itakuwaje?Ingekuwa Ulaya au Marekani polisi wangekubeba kule viboko marufuku
Kule mtoto au mke kumtuma kitu mfano afue au kuosha vyombo kama wewe kidume unatakiwa kusema Sorry my sweet honey I beg can you wash vyombo tulivyolia chakula? Vinginevyo haoshi
Ma Mura wa Kikurya mupoooo?
Safi sana,Huu mtaala wa primary umemshinda dada angu kwa watoto wake wawili mpaka wanafika form two mdogo na form four mkubwa wa kiume. Dogo la kiume ni jeuri na dharau nyingi mpaka kufikia hatua ya kuwaambia walimu kuwa hawajui kiingereza sahihi kisa yeye na dada ake wamesoma international primary school baada ya kufauru Std. Seven na kupangiwa shule za serikali.
Kuna siku akiwa likizo alileta za kuleta nikamchapa bakora, baada ya hapo akaenda kunishtaki polisi kuwa eti mjomba kanichapa so waje kunikamata hapo akiwa form two😆. Polisi wakamwambia haya tangulia nyumbani sisi tunakuja.
Sasa wanaelekea elekea maana kila wakiwa nyumbani likizo lazima niwatembelee nakuwalizimisha wafanye baadhi ya kazi na si kumuachia mfanyakazi wa ndani kila kitu mpaka kufua nguo za hili dume. Wananichukia sana nikienda pale lakini hawana jinsi kwasababu kwasasa wako chini ya uangalizi wangu maana dada hayupo nchini kikazi.
Na watanyooka tu