Nilichekwa sana Style yangu ya malezi ila leo hii watu wanatamani kuniiga

Nilichekwa sana Style yangu ya malezi ila leo hii watu wanatamani kuniiga

Mleta mada inaonyesha unakaa eneo la low class kwa Walala hoi ila wewe una kanafuu kidogo ni kama wewe ni katajiri fulani katikati ya maskini kwa ulivyojieleza lakini ungekuwa unakaa high class areas hicho ulichoandika chote ni hopeless mfano hakuna mtoto high class anatembea kwa miguu dakika 25 kwenda shule
Wewe useless kabisa
 
Ukiishi eneo la high class ambao kila mtoto anapelekwa shule na school bus au na gari ya wazazi wa kwako ukimtembeza kwa miguu kwenda shule atajiskia kunyanyasika na kuona mzazi hampendi wala kumjali atajisikia vibaya mno lakini kama yako uswahilini low class ambao asilimia kubwa wanaenda kwa mguu shule ataona sawa tu
unafikir ufahar unavyoaanaga wale watoto wenenepeana vile unafikri ni nzur kwa afya mtoto mpaka anashindwa kuhema.kuna ubaya gan mtoto akitembea.mh alikua anatembea km8 kwenda na kurud kongwa primary huko
 
Tuliozaliwa kijijini na Kisha kuja mjini ukubwani aloo tunayajua maisha kinoma.

Utotoni Kwanza full kucheza porini michezo ya kujificha, kombolela, rede, kuruka kamba, kuwinda ndege, kuwinda nyani, kuchoma misitu Moto (utukutu), kutafuta uyoga, kugema ulimbo wankutegea ndege, kutega kware na tetere kwa mitego.

Kuchonga PIA, kuchonga ngorogojo (sijui Ni kkswahili sahihi??) Kuchonga magari ya udongo na magunzi.

Kuchunga mbuzi porini masafa ya mbaaaaali huko milimani na mabondeni mnakutana kundi kubwa na wachungaji mnafurahi pamoja. Kuogelea mtoni na mabwawani, kuvua samaki kwa ndoano mtoni.

Kwenda kuvua samaki kwa nyavu mnakaa porini huko wiki nzima. Kufanya vibarua vya kulima maporini hukoo mnakuwa mnalala huko kama wiki nzima. Kuwinda nyani, sungura, swala n.k kwa mbwa!!

Daaah let me go to the village next year!!!!!!
hamna mishe zifanya hapo.nimetengeza sana magar ya udongo badae nikaanza kutafuta bering mnapigilia kwenye ubao mnaltelezea okota saana mabomba ya sindano zs hospital zilizotumika
 
Tangu mwaka jana anatwanga mguu na wala sijaona tatizo, Wenzake wengi pia wanaopanda school bus ananiambiaga huwa wanapenda kutembea lakini wazazi hawataki, Kutembea kuna raha yake
 
unafikir ufahar unavyoaanaga wale watoto wenenepeana vile unafikri ni nzur kwa afya mtoto mpaka anashindwa kuhema.kuna ubaya gan mtoto akitembea.mh alikua anatembea km8 kwenda na kurud kongwa primary huko
Mtoto kukondeana nako sio afya njema
 
Ukiishi eneo la high class ambao kila mtoto anapelekwa shule na school bus au na gari ya wazazi wa kwako ukimtembeza kwa miguu kwenda shule atajiskia kunyanyasika na kuona mzazi hampendi wala kumjali atajisikia vibaya mno lakini kama yako uswahilini low class ambao asilimia kubwa wanaenda kwa mguu shule ataona sawa tu
Tatizo lako unaongelea maisha ambayo hujawahi hata kuyaishi mkuu, unaongelea tu vitu utafkiri upo kijiweni, Kwa taarifa yako hata kule arusha njiro kwa matajiri kuna watoto wanatembea hadi shuleni au kupanda daladala, Malezi tunatofautiana mkuu, Huku nakoishi asilimia 80 watoto wanapanda school bus hii 20 tuliyobaki sio kwamba pesa ya achoolbus haipo!! la hasha!! ipo ila tunatofautiana malezi, mzazi mwengine anaona school bus inamfaa mtoto wake wengine tunaona ngoja atembee, Nikupe mfano mwengine nenda Mbeya maeneo ya kishua kama Uzunguni kwa wazito kuna watoto wanatembea vizuri tu mpaka shuleni na wazazi wao pesa zimejaa, Tatizo inawezekana huna hata mtoto kwahio hujui unachokiongea, unayoa stori za vijiweni unaweka humu jukwaa la great thinkers.
 
Saf sana umeweza kumuandaa mtoto vzr ila muache awe na skills ya life ajifunze kutengeneza tiyara(kit) atengeneze magari awinde ndege nk
 
Mleta mada inaonyesha unakaa eneo la low class kwa Walala hoi ila wewe una kanafuu kidogo ni kama wewe ni katajiri fulani katikati ya maskini kwa ulivyojieleza lakini ungekuwa unakaa high class areas hicho ulichoandika chote ni hopeless mfano hakuna mtoto high class anatembea kwa miguu dakika 25 kwenda shule
Inaonekana huwezi kabisa kujisimamia na kujiamini kufanya kile unachokiona bora kwako. Wewe ni dizaini ya watu wanaofanya vitu kwa kupelekwa pelekwa tuu ilimradi usionekane upo tofauti. Be a man
 
safi kabisa.sisi kuna ps 4 hapa home.mdg wetu kamaliza diploma ya ualim ila jaman akijifungia humo chumban anaweza akaanza game saa 12 asbh anatoka jion yaan hata kula hali.hana socialize tionkabisaaaa
Mkuu nilifatilia hii ishuu google, huu ni ugonjwa unaitwa gaming addiction na umegharaimu maisha ya vijana wengi kuwa wazembe, kufeli shuleni, kuacha kusocialize maana wanajifungia sana, n.k

Na huko nje kuna rehab kabisa za hawa waathirika.

Cha kufanya chukueni hio game muifiche awe anacheza saa moja tu kwa siku inatosha, atafute kazi lasivyo mtampoteza huyo kijana.
 
Nice

swalehe kaosha ukuta leo anajikuta kichaa yeye na pacha ake Grace
 
Mkuu bila shaka unatokea DODOMA mpk SADA unazijua ahahaha ,basi haya NGWELU ,NGUKWE , MPELEMEHE piaa ahahaha ,akajifunze na kuwinda MBAWALA,FUNO na HARUZI ,bila kusahau kusenya KUNI ,mkuu nimecheza sna porini kuwinda Maeneo.ya Mpwapwa huko .Pamoja sana.
 
Ugumu wa maisha ukitumiwa vizuri unasaidia sana mbeleni.

Kuna ndugu watatoka vijijini wanasoma Dar wanajifunza maisha. Baada ya muda wanaenda mbali zaidi ya watu wengi waliowakaribisha, waliozaliwa Dar.

Mara nyingi hua naona watoto wanaokua na akili za maisha ni wale haswa waliokulia kijijini na kusoma huko angalau mpaka std 7. Huyu akija kutoka huko akaja mjini humuambii kitu maisha anakua anayajua hasa.

Hawa wanaoenda mara moja moja kipindi cha krismasi sawa sio mbaya sana ila ukute na yeye mtoto ana akili kichwani. Wengine wakifika vijijini ndio anaanza kujikuta supastaa kila kitu anajua yeye na maneno mengi kama chiriku. Akiamka asubuhi anaoga na kuvaa raba anaanza kuzunguka zunguka tu kama mtalii.

Olu in olu ni vizuri mzazi kumu ekspozi mtoto kwenye hali tofauti tofauti za maisha.
 
Mkuu bila shaka unatokea DODOMA mpk SADA unazijua ahahaha ,basi haya NGWELU ,NGUKWE , MPELEMEHE piaa ahahaha ,akajifunze na kuwinda MBAWALA,FUNO na HARUZI ,bila kusahau kusenya KUNI ,mkuu nimecheza sna porini kuwinda Maeneo.ya Mpwapwa huko .Pamoja sana.
Hahahaha Yes ni kweli,Mm ni wa kanda ya kati,matunda hayo huyakosi aisee,
Zile root ya kujua hiyo miti ya matunda ilipo,inastawisha afya ya akili sana.
 
Mtoto hata hajakua unaanza kujisifia. Kuna waliokuwa na maadili mema, walipofika chuo wakaanza umalaya, ulevi na kubwia unga.

Subiri akue kwanza.
 
Safi sana bro..naunga mkono..hata mim wanangu ntapeleka style hyo

Sisi tuliolelewa kimayai tunaziona athar zake ukubwani...mim mmoja wao
 
hamna mishe zifanya hapo.nimetengeza sana magar ya udongo badae nikaanza kutafuta bering mnapigilia kwenye ubao mnaltelezea okota saana mabomba ya sindano zs hospital zilizotumika
Hahahaha watoto wa sikuizi wanakosa sana haya maajabu.
Hapo kuzurula hosptal na kuokota sindano.
Nakumbuka jion moja tukaenda kuzurula maeneo ya kituo cha afya, timu ya vijana si chini ya saba na mbwa watatu.
Kando kando tunapitachocho hapa na hapa
Tukaona mbwa anakuja na kitu kama linyama hivi,sasa wakati anatusogelea kuna midewife mmoja (hakua zamu ila anakaa kota)akamuona mbwa yule akatuambia tumuamuru yule mbwa aache au tumnyang'anye hilo linyama na tulifukie haraka.
Hatukua wabishi tukafanya hivyo.
Kesho yake shule tukaitwa na mwalimu akatuonya kutembelea mazingira hatarishi huko hosptali tuache.
Akatuuliza mnajua yule mbwa jana alibeba nini,tukamwambwia hatujui.
Akasema ni kondo.
Mbwa alifukua mahali lilipotupwa na kufukuwa kondo la uzazi.

Hata sikuelewa kondo ni nini nilikuja kuelewa nipo darasa la sita,kwenye somo la sayansi.

Tuashateleza sana kwny mizambarao..
Tumekwea hadi mipapai...😂😂😂
 
Mtoto hata hajakua unaanza kujisifia. Kuna waliokuwa na maadili mema, walipofika chuo wakaanza umalaya, ulevi na kubwia unga.

Subiri akue kwanza.
Hicho ulichokiongelea ni kitu kingine kabisa, wapo waliowahi kusoma seminari tangu shule ya msingi mpaka form 6 na walikuwa na tabia nzuri tu ila chuoni walipofika walibadilika kabisa, Kwa hio kitu unachozungumzia kipo nje ya maada.

Anyway kila mtu na malezi yake,
 
Mara nyingi hua naona watoto wanaokua na akili za maisha ni wale haswa waliokulia kijijini na kusoma huko angalau mpaka std 7. Huyu akija kutoka huko akaja mjini humuambii kitu maisha anakua anayajua hasa.

Hawa wanaoenda mara moja moja kipindi cha krismasi sawa sio mbaya sana ila ukute na yeye mtoto ana akili kichwani. Wengine wakifika vijijini ndio anaanza kujikuta supastaa kila kitu anajua yeye na maneno mengi kama chiriku. Akiamka asubuhi anaoga na kuvaa raba anaanza kuzunguka zunguka tu kama mtalii.

Olu in olu ni vizuri mzazi kumu ekspozi mtoto kwenye hali tofauti tofauti za maisha.

Kabisa sababu maisha hayatabiriki. Mzazi anaweza kufa, kufukuzwa kazi, biashara kuyumba, magonjwa, uzee.

Mtoto inabidi awe tayari kwa yote just in case.
 
Hilo swala la kutembea miguu kuna raha yake nalikubali kabisa 100%...nakumbuka kipindi npo o level niliwahi nunuliwa baiskel na mshua lakini nilkuwa naiacha home ili mradi tu nitembee na wenzangu tupige story njian
 
Kwamba na watoto wengine wanasema wanapenda kutembea kwa miguu kuliko school bus na wewe umeamini??

6988dc76-4d89-459c-87ad-6b3f51990ecc.jpg
 
Back
Top Bottom