Nilichekwa sana Style yangu ya malezi ila leo hii watu wanatamani kuniiga

Nilichekwa sana Style yangu ya malezi ila leo hii watu wanatamani kuniiga

Watoto wa sister yako umetokana nao wapi?

Kakutumia wanae ukae nao?

Kwahiyo yeye kaona kazi ya kulea haiwezi kaamua ku delegate wanae umlelee?

Dada yako is a part of the problem.

Unachoshindwa kuelewa wote mpo kwenye mkanganyiko wa cultures

Wewe ni wa culture tofauti na hao watoto....Hakuna haja ya kuwachukia...na sio kosa lao

Wewe nae nakuona una tatizo la uelewa....unadhani hawa watoto wanafanya makusudi...unatumia lense ya ajabu sana ku view hawa watoto..which according to me na hao watoto you are dead wrong
Cultural collision hiyo inaitwa au mila gongana kiswahili
 
Hapa naona ni clash of cultures

Wanadamu kibao wana dharau na haina uhusiano wa mtu kasoma wapi

Shida ni kwamba nyie ndio mna shida na hawa watoto...shida ni kua wanajua Kingereza zaidi yenu

Yanini mnawazonga?Leave these kids alone...

Akisema anajua Kingereza zaidi ya fulani,mrekebishe...

Huruhusiwi kuchapa watoto wa watu,sijui hayo madaraka umejipa wapi?

Usipende kujipa madaraka ya kuchapa au kudispline watoto wa watu wengine,sio wako,thats the bottomline

Ukorofi kwa watoto ni universal,huyo mtoto ni mtukutuku tu hata kama angekua anasoma Kayumba angekua mkorofi hivyo hivyo ana angekua anajibu watu hovyo hivyo hivyo sema it happens anajua Kingereza mmegeuzia lawama kwenye Kingereza.

Dada yako ni mwanadamu mbali na wewe...usipende kuingilia wanae...sio wao..huna haki ya kuwanyoosha,dada yako ndio kazi yake.....

Una chuki sana na hao watoto I can see in your eyes..leave them alone..they are not yours..wakiharibikiwa ni wao na wazazi wao....stop hizi chuki namna hii
Hahaha mkuu labda nami nikujibu kiustaarabu tu. Kwanza kabisa jua Sina chuki nao ila maisha waliyokulia siyakubali na sitawaacha waendelee na maisha hayo wakiwa chini yangu. Baba yao alishatangulia mbele za haki na mama yao yupo ughaibuni kikazi Sasa no zaidi ya miaka 8. Am totally responsible to these children and the matter of fact I treat them the same way I treat of my own.
Swala la kujua kiingereza hizo ni accusations za walimu kila ninapoitwa shuleni kisa kafanya makosa haya mara muda mwengine mengine kabisa. Sasa ni form Four na mpaka kufikia hapo nimeshamuhamisha shule tatu kwa utovu wa nidhamu, ni bahati hii aliyopo sasa ndio amemaliza form three na sasa ameingia form four. Hivi hao walimu anaowadharau na wenyewe wakaamua wasimpe materials yanayotakiwa au wakamsusa, hiyo NECTA atatoboaje?
Wewe Kama unaona kuna chuki sawa, Kama watoto wako unawalea kimayai as you're living in America, that's ok with you, acha mi nipambane na kuwapa maadili sahihi ya kitanzania
 
Watoto wa sister yako umetokana nao wapi?

Kakutumia wanae ukae nao?

Kwahiyo yeye kaona kazi ya kulea haiwezi kaamua ku delegate wanae umlelee?

Dada yako is a part of the problem.

Unachoshindwa kuelewa wote mpo kwenye mkanganyiko wa cultures

Wewe ni wa culture tofauti na hao watoto....Hakuna haja ya kuwachukia...na sio kosa lao

Wewe nae nakuona una tatizo la uelewa....unadhani hawa watoto wanafanya makusudi...unatumia lense ya ajabu sana ku view hawa watoto..which according to me na hao watoto you are dead wrong
Jibu la maswali yako lipo kwenye post no. 115
 
Safi sana,
Lakini rohoni wanakulaani kinoma.
Wameshaanza kunyooka na wanajichanganya na wenzao Kama kawaida. Sasa si wavivu, kufua wanafua na sometimes wakiwa nyumbani utasikia wa kike mwenyewe anamuomba mfanyakazi amsaidie kufanya kazi ambayo mfanyakazi alikuwa akifanya. Kama ningesema niwaache waishi maisha waliyokuwa wakiishi, haya mabadiriko yangetokea lini?
Kwasasa Ile chuki waliyonayo juu yangu imeshakwisha maana wako free kwangu kunieleza lolote na nawaelekeza na kuwatimizia. Upendo wa familia umerudi, hawana tofauti na wenzao sasa. Nafurahi kuwaona wakijichanganya na wenzao wakicheza kwa furaha au wakiwa wanafundishana huku wakitaniana
 
Sijaimaliza yote lakini mkuu, umekua sasa. Kuna malezi ambayo ni muhimu kwa kila mtu ili kupata jamii inayozingatia miiko na tamaduni za kiafrika.
 
Kuna rafiki yangu alishawahi niambia - kuna umuhimu wa kuinvest kwenye elimu ya watoto wako hata kama ni shule nzuri ukiweza kama Aga Khan etc. hata kwa kujinyima. Nikamuuliza kwa nini...alinielezea vizuri sana.. shule hizi zina watoto wa influencers na tukubali tukatae ni muhimu kuinvest kwenye social networking(ambayo inatofauti kubwa na socializing) maana mtoto wako anaanza kujijengea hazina ya watu muhimu akiwa mdogo. Na kumbuka lasting friendships and connections zinaanzia huko siyo chuo kikuu ambako ni too artificial.
Uko sahihi kabisa dada yangu. Hata exposure ya watoto inakuwa kubwa. Mtoto anaenda o level anakuwa exposed kwenye robotics and programming, wakati akina sisi tunazikuta chuo kikuu tena inanistukiza tu. Kizazi hakibadiriki kwa sababu thinking process yetu yote ni ya shida tupu.
 
Ni changamoto kubwa katika malezi hasa kwa sisi tuliopitia vyuoni na kuna vimishahara au vifaida vya kusongesha life tunajikuta mara nyingi tunalea watoto ndivyo sivyo

1. Mwanzoni mtoto wangu alikuwa anasoma hizi shule za kutoka saa 11 na shuleni wapo wachache darasani hawazidi 20. Pia maendeleo ya social skills sikuyafurahia na hii shule ilichangia katika hili tatizo.

Pesa ya muhula mzima nilikuwa nimeshalipa ila nikamuhamisha shule nyingine ambayo wanawaigi kutoka mchana na darasani wamo kama 57 hivi, nilifanya hivi ili kupanua chances zake za kuwa na marafiki wengi maana kiukweli ile shule ya zamani alikuwa na rafiki moja tu ila kwa sasa ana marafiki wengi, na kitu kingine ike shule ya zamani ilikuwa ni masomo mtundo moja mpaka jioni hii iliminya mda wa wanafunzi kupata mda wa kujuana, hii shuke ya sasa naona wana kmjuoindi cha michezo mara 2 kika wiki, na pia muda wa wanafunzi kujuana zaidi wanapowahi kutoka mchana upo.

Nafurahi sana mwanangu kwa sasa sio mpweke sana kama zamani, shuleni pia iww sehem ya kujenga social skils sio kusoma tu darasani, nami pia kila siki za shule nahakikisha usiku nakaa nae lisaa kumsaidia masomo maana nilipewa syllabus na vitabu wanavyotymia kuwafundishia na wala havinipigi chenga.

2. School bus silipii, sioni umuhimu wake labda mwanafunzi wa mtoto asiezidi miaka mitano na shuke ipo mbali sana, Shule anayosoma mwanangu ukitembea ni mwendo wa dakika 25 tu na wapo wenzake wachache ambao hawalipii school bus wanapitaga njia hii pamoja na wenzao wengi wanaosoma shule ya serikali iliyopo karibu na shule yao, Hii hali nikaona ni kumdumaza tu mtoto hizi school bus, tangu mwaka jana anatwanga mguu na wala sijaona tatizo, Wenzake wengi pia wanaopanda school bus ananiambiaga huwa wanapenda kutembea lakini wazazi hawataki, Kutembea kuna raha yake 😁.

3. Akitoka shuleni inabidi afue nguo zake, kuosha vyombo atavyolia chakula, kusafisha chumba chake, n.k hivi nlimpiga stop house girl kuvifanya kwa mwanangu japo wife alipinga kudai bado wadogo ila nikamwambia silei mayai, baada ya hapo ataweza kucheza na marafiki zake hapa kwangu ama kwao kwa kutoa taarifa mapema tutamkuta nyumba ya rafiki yake yupi, zamani nlikuwa nampiga geti kali ila sikuona faida, kwa sasa amekuwa msaada mkubwa kwa wenzake mageti kali ambao kwamfano nyumba flani mzazi aliniomba mtoto wangu awe anaenda pale kila jumapili maana ni siku ambayo mtoto wake anakuwa hajabanwa na hizi shule wanazotoka saa 11 juoni, hana homework, n.k ila kwake hataki kabisa mtoto wake kutoka nje, ni jambo zuri kuwapa kampani wenzake mi nikamkubalia maana huyo mtoto ndio alikuwa best wake wa shule ya zamani na hata wazazi wake tunajuana nao na ni mfano wa familia bora yenye maadili kwa hio huwa sina shaka, japo nilimuambia mwanangu akijiona hataki au kachoka kwenda awe free kuniambia, haniogopi huwa hasiti kuniambia chochote

4. Zamani nilimwekea Playstation (game ya tv) na katuni nikijidanganya ndio vitampa kampani kama rafiki, kiukweli nilijidanganya, kwanza hii playstation ikaanza kumpa kama uraibu flani wa kuwa teja, yani akisikia playstation anakuwa kama teja hivi, weekend ukifika ndo kabisa anaweza kushinda hapo kwenye screen hadi mnashangaaa. Kiukweli nikaona hizo kampani zake za katuni na magem yatamuharibu na kumfanya afikirie katika ulimwengu ambao haupi kama huo w akwene game na katuni, Ikabidi nimletee mpira awe anacheza cheza nje maana alikuwa anashinda sana ndani, ile game nikaficha nikamdanganya ipo kwa fundi, kidogo kidogo akaanza kuzoea nje, nikamletea na ka mbwa kadogo basi akawa anakapenda sana saizi ni mbwa mkubwa wa ulinzi hapa, furaha yangu ni kumuona akiwa nje, hivi na vile nikaamwamisha shule akaanza kuwa na marafiki kadhaa, nikaacha kulipia schoolbus ili awe ananyoosha vimiguu, n.k basi ndo namimi nafurahi hapo

5. Kuna kipindi flani nilipokuwa naenda kijijini (ni mwendo wa saa moja toka napishi) kwenye vikao hivi na kuwajulia hali ndugu zangu, nilikuwa naenda na huyu mwanagu nae, navyoendelea na shughuli zangu alikuwa anachangamana na wenzake, akiwa huko na wenzake aliweza kufundishwa kujipikia ugali maana kule kijijini kujipikia ni kitu cha lazima kukijua, Hii hali inamwandaa mapema hata atakapoanza maisha yake asiwe mpya kwenye kujilisha, Mke wangu hili jambo mwanzoni alichukizwa nalo sana na kuanza kuniambia mtoto wetu hafai kupika hadi awe mkubwa kwa sasa asome tu lakini kwangu nilipingana nae nikamwambia hakuna tatizo mtoto wetu kujua kupika, ipo siku atahitaji hiki alichojifunza, Hpa fundisho kuu ni kwamba mtoto inabidi ajue kujilisha, Isiwe tu kwa watoto wa kike bali hata wa kume.

6. Michezo - hapa kwanza kabisa nianze na kuelezea kwambaniliwahi kugharamie ajifunze kuogelea, maana kule kijijini nilihofia kuna siku wataenda huko mtoni na majanga yakampata, kwa hio nilichukua hii precaution haraka, Nawaasa sana wazazi mambo kama kuogelea msiyapuuze, ni kitu kinachweza kuokoa maisha ya mwanao au yeye kuokoa maisha ya wengine. Kitu kungine kwa kuchangamana na wezake huku kwetu na shuleni ameweza kuwa mchezaji mzuri tu wa mpira ni kitu kizuri ila pia kijijini kule alifundishwa hizi sarakasi aliteguka mkono mama yake tuligombana sana hii ishu, ila hakuacha aliendelea na kufanikiwa kuweza kuruka hizi sarakasi, Mwaka jana siku ya wazazi wanapofunga shule nilipata kujisikia vizuri nilipomuona mwanagu akiwa anaonyesha ujuzi wake mwele ya umati wa wanafunzi na wazazi tuliofika hapo, Ni jambo lililonifurahisha na hata marafiki zangu na wa mke wangu walipoona zile video tulipewa visifa kidgo, basi hata wife zile hasira zake za mtoto kujifunza sarakasi zikawa zinashuka

7. Kuhusu kumlimbikizia kazi house girl mbazo ni wajibu wa mtoto kuzifanya nimezingatia hili suala japo tumekorofishana sana na mke wangu anaetaka housegirl afanye karibu kila kitu watoto wakae tu, Binafsi nilikataa kabisa huu mpango na mtoto ameshauzoea na umekuwa na tija kwake kujua mapema kwamba maisha ni majukumu, Hata hivyo leo hii au kesho hali yetu inaweza ikawa mbaya watoto wakapata wakati mgumu maana hakutauwa na house girl, Ni kwamba kwa sasa kazi zilizokuwa zinafanywa na house girla anazifanya huyu mwanangu ama awanapeana zamu inapobidi baadhi ya kazi ni : Kabla hajalala inabidi apasi nguo zake, Inabidi atandike kitanda chake kila siku, asafishe chumba chake, akitoka shuleni afue uniform zake, Asubuhi akiamka anafagia uwanja kwa zamu na house girl leo yeye kesho hause gerl, Viombo anavyolia inabidi aoshe yeye, n.k Mwanzoni alikuwa mgumu ila nilimfundisha, na alipokuwa mzembe nilimuonya, na aliporudia uzembe bakora ilitumika.

8. Matumizi ya bakora yanatumika kwa sasa mwanangu napomfundisha kitu flani, akarudia nikamuonya, akarudia tena nikamkaripia ila akiendelea kuna viboko vya mpera, Matumizi ya viboko kwa usahihi ni muhimu sana katika malezi ya watoto, Yapasa atambue kuna madhara ya kutofata anachofundishwa na wazazi wake na kutokiheshimu, Hii pia hata akiwa mkubwa anajitegemea atakuwa anajua kabisa kwamba asipofata hizi sheria jela inamhusu au atafunzwa na walimwengu, Wazazi msipuuzie viboko hivi, kuna maana kubwa sana vimeruhusiwa kutumika hata kwenye biblia na korani na hata kutumuka vizazi hadi vizazi hadi hapa tulipo, haya malezi ya wazungu mnayoyaiga ni kuacha asili yenu, Narudi tena tuvitumie viboko kwa njia sahihi sio kila mda unapiga tu.
Hii muendelezo wa bandiko lako hili ? Mbinu niliyotumia kumlea mwanangu anayesoma private awe mjanja, awe na furaha, na asigeuke kuwa kuku wa kisasa.
 
Asante sana mkuu kwa huu uzi, nimescreenshot baadhi ya sehemu na kumtumia sister yuko ughaibuni na watoto wake wapo hapa nchini. Wakati yupo aliwalea kama mayai, Ila sasa wapo chini ya uangalizi wangu. Sijawahi ona eti Kuna tv ya sitting room alafu unanunua tv nyingine inakaa chumbani kwa mtoto wa kiume kwaajili yakuchezea PlayStation games akiwa likizo toka shuleni😬
Nimefungia laptop zao na PS now ni mwendo kumsaidia mfanyakazi baadhi ya kazi wakiwa likizo. Kuna siku niligombana na sister baada ya kusikia nimemchapa mwanae wa kiume tena vibakora vitatu tu😆. Alininunia the whole week, nikamwambia mimi siwalei Kama wewe ulivyokuwa unawalea bali nitawalea Kama sisi tulivyolelewa na wazazi wetu. Ilimchukua muda kukubaliana nami.
Una hoja hao watoto wanatakiwa kuishi maisha yako sio wewe uishi maisha yao unawapa somo zuri kuwa wajifunze kuwa when you go to Romans you behave like a Roman not like Americans from American Donld Trump Academy!! Big up

Sio litoto linatoka Marekani linaenda kwa bibi yake bukoba kijijini halafu linalilia bibi yake alipikie Pizza eti ndizi halili
 
Huwezi chukua your culture unasukumizia hawa watoto down their throats kwa viboko na lazima

Mnaleta Third World War isiyokua na lazima

Hivyo viboko havisahauliki na siku utakuja kuvilipa wewe mwenyewe

Waache,watajifunza wenyewe....yaani wewe unageuka ni catalyst ya kuwabadili utakavyo wewe

Watu wa ajabu sana nyie...

Huna haki ya kuchukua utamaduni wa mtu aliokua nao na kumpakaza wako asioutaka,sema kwa utashi wake aamue kuuchukua

Mi nadhani mnajifanya nyie ndio alpha and omega wa hawa wanadamu hapa duniani kumbe you guys are just trouble makers na mna your personal troubles within yourselves.

Kinachotakiwa ni wewe kukataa immorals.....Morals ni universal,kama anachofanya ni immoral then you can stop that na akaona hoja yako....

Ila eti anavyo-ongea,uvaaji,physical expression,language,etc unakomaa afate ukitakacho wewe sana sana ninakuona hovyo kabisa,it is unneccessary...

Kama utamaduni wako ni superior atataka na atapenda naturally ku-adopt...Acheni hawa wanadamu nyie
Toto bila viboko litaharibikia ndio aana hadi Mungu akasema usimnyime mtoto viboko

ulaya na Marekani viboko hawataki kwa watoto ndio kunaongoza kwa kuwa na misagaji na mishoga na mijitu ya ndoa za jinsia moja hadi mijaji mibunge serikalini na mikanisani

Tanzania makabila ya pwani na Zanzibar ndiko kuna mishoga na misagaji Mingi sababu viboko mwiko kabila kama mkurya au masai msagaji au shoga utamtoa wapi wanapiga likiaonyesha tu dalili hata ndogo tu ya ujeuri hadi kutishia kuua so litoto linaanza kujua boundaries za ethics mapema na kubehave
 
Ndio maana nasema tusimamie MORALSSSSS!

Ushoga sio morals ni immorals,ni lazima ukatae na wataelewa hoja yako

Kwahoja na kwa force thereafter

Mnashangaza kudhani ushoga ni utamaduni wa wazungu....

Ushoga upo jamii zote across the world and all species karne na karne...Africa mashoga wapo

Issue hapa ni kwamba ushoga ni immorals na watoto innately wanajua na ukisimamia hii hoja by force and everything ni very very understandable

Shida ni nyie kutaka eti mtoto aache utamaduni aliokulia nao kama kuvaa,kuongea,kujieleza,chakula,nk afate vyako kwa lazima...muache bwana

Atajifunza mwenyewe utamaduni of his ancestors akitaka

Mnaongea as if utamaduni wa jamii zingine duniani ni mavi na useless,wakati ni the same au better..afterall who cares unakula chakula gani?

Ule pizza au kande who cares?Acheni hizi dictatorships za ajabu
I smell a rotten rat siongei na shoga au msagaji au mtu wa ndoa ya jinsia moja humu?
 
Mleta mada inaonyesha unakaa eneo la low class kwa Walala hoi ila wewe una kanafuu kidogo ni kama wewe ni katajiri fulani katikati ya maskini kwa ulivyojieleza lakini ungekuwa unakaa high class areas hicho ulichoandika chote ni hopeless mfano hakuna mtoto high class anatembea kwa miguu dakika 25 kwenda shule
Tazama ulichokiandika ndicho hopeless
 
Ni changamoto kubwa katika malezi hasa kwa sisi ambao kuna visenti kidogo huwa tunajikuta tunataka kulea watoto kizungu sana na kuwa na visingizio kama "sitaki mtoto wangu apitie shida nilizopitia" na kujikuta tunalea watoto ndivyo sivyo

1. Mwanzoni mtoto wangu alikuwa anasoma wanatoka saa 11 jioni na shuleni wapo wachache, darasani hawazidi 20. Kwangu kama mzazi nilipoona mtoto wangu navyoenda kumchukua hana marafiki alikua nae moja tu ambae ni jirani na kamzidi darasa, nikajiongeza nikaona hii hali imechochewa na wanafunzi wachache darasani kujumlisha shule kutowapa watoto muda wa kutoka wa kucheza, kujuana, n.k maana pale ilikuwa ni shule ya darasani mtindo moja,

Pesa ya muhula mzima nilikuwa nimeshalipa ila nikamuhamisha shule nyingine ambayo wanawaigi kutoka mchana na darasani wamo kama 60 hivi, shule pia ina ratiba za vipindi wanafunzi kufanya shughuli za kujenga social skills mfano vipindi vya michezo katika ratiba, vipindi vya story telling, vocational skills, n.k Niliona mwanangu akiwa na maendeleo katika social skills alipata marafiki shuleni, zamani alikuwa mkimya sana na mpole ila akaanza kuwa muongeaji na mchangamfu, pia ule mda wanapowahi kutoka mchana unachangia sana kusocialize tofauti na zamani wakitoka saa 11 jioni wanakuwa wamechoka.

Kuhusu ubora wa elimu bado sijaona tofauti katika shule ya zamani na sasa (zote ni za english) nami pia kila siku za shule nahakikisha usiku nakaa nae lisaa kumsaidia masomo maana nilipewa syllabus na vitabu wanavyotymia kuwafundishia na hakuna chochote kinachoweza kunispiga chenga elimu ya shule ya msingi.

2. School bus silipii, sioni umuhimu wake labda mwanafunzi awe mtoto asiezidi miaka mitano au shule ipo mbali sana, Shule anayosoma mwanangu ni mwendo wa dakika 25 tu na wapo wenzake wachache ambao hawalipii school bus wanapitaga njia hii pamoja na wengine wengi wanaosoma shule ya serikali iliyopo karibu na shule yao, School bus niliona ni kumdumaza tu mtoto, anatwanga mguu na wala hakuna tatizo, Wenzake wengi pia wanaopanda school bus ananiambiaga huwa wanatamani sana kutembea ila wazazi hawataki, Kutembea kuna raha yake ya kufanya zoezi, kujimix / kusocialize, n.k.

3. Saizi namruhusu awe anacheza na wenzake nyumbani kwangu au kwa marafiki zake kwa kutoa taarifa mapema tutamkuta nyumba ya rafiki yake yupi, zamani nlikuwa nampiga geti kali na sikuona faida, kwa style hii pia amekuwa msaada mkubwa kwa wenzake wasioruhusiwa kutoka nje maana huu mtaa naoishi wengi hawataki watoto watoke nje, kuna jirani aliniomba mtoto wangu awe anaenda pale kila jumapili maana ni siku ambayo mtoto wake anakuwa hajabanwa na shule , hana homework, n.k ila yeye hataki kabisa mtoto wake kutoka nje, mi nikamkubalia maana yule mtoto ndio alikuwa best wake wa shule ya zamani na hata wazazi wake tunajuana nao na ni mfano wa familia bora yenye maadili kwa hio huwa sina shaka, japo nilimuambia mwanangu akijiona hataki au kachoka kwenda awe free kuniambia, haniogopi huwa hasiti kuniambia chochote

4. Zamani nilimwekea Playstation (game ya tv) na katuni nikijidanganya ndio vitampa kampani kama marafiki, kiukweli nilijidanganya, kwanza hii playstation ikaanza kumpa kama uraibu flani wa kuwa teja, yani aliigeuza game kuwa kama mbadala wa marafiki watu, weekend ikifika ndo kabisa anaweza kushinda hapo kwenye screen hadi mnashangaaa. Kiukweli nikaona hizo kampani zake za katuni na magem yatamuharibu , Ikabidi nimletee mpira awe anacheza cheza nje maana alikuwa anashinda sana ndani, ile game nikaficha nikamdanganya ipo kwa fundi, kidogo kidogo akaanza kuzoea nje, nikamletea na ka mbwa kadogo basi akawa anakapenda sana saizi ni mbwa mkubwa wa ulinzi hapa, furaha yangu ni kumuona akiwa nje, nikaamwamisha shule akaanza kuwa na marafiki kadhaa, nikaacha kulipia schoolbus ili awe ananyoosha vimiguu, n.k basi ndo namimi nafurahi hapo

5. Kuna kipindi flani nilipokuwa naenda kijijini (ni mwendo wa saa moja ) kwenye vikao hivi na kuwajulia hali ndugu zangu, nilikuwa naenda na huyu mwanagu nae, navyoendelea na shughuli zangu alikuwa anachangamana na wenzake, akiwa huko na wenzake aliweza kufundishwa kujipikia ugali maana kule kijijini kujipikia ni kitu cha lazima kukijua, Hii hali inamwandaa mapema hata atakapoanza maisha yake asiwe mpya kwenye kujilisha, Mke wangu hili jambo mwanzoni alichukizwa nalo sana na kuanza kuniambia mtoto wetu hafai kupika hadi awe mkubwa kwa sasa asome tu lakini kwangu nilipingana nae nikamwambia hakuna tatizo mtoto wetu kujua kupika, ipo siku atahitaji hiki alichojifunza, Hapa fundisho kuu ni kwamba mtoto inabidi ajue kujilisha, Isiwe tu kwa watoto wa kike bali hata wa kiume.

6. Michezo - hapa kwanza kabisa nianze na kuelezea kwamba niligharamia ajifunze kuogelea, maana kule kijijini nilihofia kuna siku wataenda huko mtoni akiwa hajui kuogelea, kwa hio nilichukua hii tahadhari haraka, Nawaasa sana wazazi mambo kama kuogelea msiyapuuze, ni kitu kinachoweza kuokoa maisha ya mwanao au yeye kuokoa maisha ya wengine.

Pia kijijini kule alifundishwa hizi sarakasi aliteguka mkono mama yake tuligombana sana hii ishu, ila hakuacha aliendelea na kufanikiwa kuweza kuruka sarakasi za aina nyingi na pia katika shule ya karibu ya serikali aliendeleza kipaji chake hapo kwa kuwa kulikuwa na wanafunzi wengi wanaojua sarakasi, Mwaka jana siku ya wazazi wanapofunga shule nilipata kujisikia vizuri nilipomuona mwanagu akiwa anaonyesha ujuzi wake mbele ya umati wa wanafunzi wenzake na wazazi tuliofika hapo, Ni jambo lililonifurahisha na hata marafiki zangu na wa mke wangu walipoona zile video tulipewa pongezi kidgo, basi hata wife zile hasira zake za mtoto kujifunza sarakasi zikawa zimeisha baada ya kusifiwa na wenzake hahaha.

7. Kuhusu kumlimbikizia kazi house girl mbazo ni wajibu wa mtoto kuzifanya nimezingatia hili suala japo tumekorofishana sana na mke wangu anaetaka housegirl afanye karibu kila kitu mtoto wakae tu, Binafsi nilikataa kabisa huu mpango kumle mtoto mtindo ambao hata mimi wala mke wangu hajalelewa, alianza kutekeleza wajibu kwa mtoto katika kusaidia kazi za nyumbani ni kujua mapema kwamba maisha ni kusaidiana na majukumu, Hata hivyo leo hii au kesho hali yetu inaweza ikawa mbaya watoto wakapata wakati mgumu maana hakutakuwa na house girl, kwa sasa kazi zilizokuwa zinafanywa na house girl anazifanya huyu mwanangu ama wanapeana zamu inapobidi, baadhi ya kazi ni : Kabla hajalala inabidi apasi nguo zake, Inabidi atandike kitanda chake kila siku, asafishe chumba chake, akitoka shuleni afue uniform zake, Asubuhi akiamka anafagia uwanja kwa zamu na house girl , Vyombo anavyolia inabidi aoshe yeye, n.k Mwanzoni alikuwa mgumu ila saizi kazoea, anapozembea namuonya, na inapobidi bakora hazikwepeki.

8. Matumizi ya bakora yanatumika kwa sasa, mwanangu napomfundisha kitu flani au tabia flani aiache, akarudia nikamuonya, akarudia tena nikamkaripia basi kinachofuata kunadawa flani imejaa sana hapa nyumbani kwenye mti wa mpera ni kitendo cha kuichuma tu na kuanza kuitumia, hio dawa si nyingine bali ni viboko, Matumizi ya viboko kwa usahihi ni muhimu sana katika malezi ya watoto, Yapasa atambue kuna madhara ya kutofata kitu sahihi anachofundishwa na wazazi wake na kutokiheshimu, Hii pia inamuandaa hata akiwa mkubwa atakuwa anajua kabisa kwamba asipofata hizi sheria jela inamhusu au atafunzwa na walimwengu, Wazazi msipuuzie viboko hivi, kuna maana kubwa sana vimeruhusiwa kutumika enzi toka enzi na mababu zetu mpaka sasa na hata kwenye biblia na korani, haya malezi ya wazungu mnayoyaiga ni kuikataa asili yenu, Narudi tena tuvitumie viboko kwa njia sahihi sio kila mda unapiga tu.
Mimi sijui hata hao waliokupa ''likes'' wamekupa za ni nini kwani umeelezea mtoto/watoto wa watu wengi wanavyolelewa siku zote tofauti na ulivyokuwa ''mkoloni'' hapo zamani.
 
Mmmm kukaa porin wik nzima?

Tena wakat mwingine wiki 2 zinafika, na huko hakuna nyumba wala kibanda, mnalala kichakani kando kando ya mto na Moto mkuubwaaaaaaaaa!!
 
Mleta mada inaonyesha unakaa eneo la low class kwa Walala hoi ila wewe una kanafuu kidogo ni kama wewe ni katajiri fulani katikati ya maskini kwa ulivyojieleza lakini ungekuwa unakaa high class areas hicho ulichoandika chote ni hopeless mfano hakuna mtoto high class anatembea kwa miguu dakika 25 kwenda shule
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]Nilijua lazima nitakutana na comment kama hii
 
Umefanya sahihi kasoro kumruhusu aende nyumba za watu.

Anaweza kuwa abused huko sexually usijue.

Na mtoto mwenzie au watoto wakubwa wanaokuja nyumba hiyo hata houseboy au housegirl.

Siku hizi kuna shule za serikali English medium, naona kama Better kuliko private English medium.
Hilo anatakiwa alifahamu mapema, hatari ipo hapo.
 
Mleta mada inaonyesha unakaa eneo la low class kwa Walala hoi ila wewe una kanafuu kidogo ni kama wewe ni katajiri fulani katikati ya maskini kwa ulivyojieleza lakini ungekuwa unakaa high class areas hicho ulichoandika chote ni hopeless mfano hakuna mtoto high class anatembea kwa miguu dakika 25 kwenda shule
Maisha ni uchaguzi,,anaweza kuwa low income class,, middle au high lakini ameeleza vizuri alivoamua kuishi,,haha mambo ya classes hayana maana sana,,sababu shabby,,abood,,Omar awadh,,Dangote anaweza kuwaita low income class,,wakati mwingine anaweza kuwa anapata 500k tu kwa mwezi akatafsiriwa na wengine Kama middle au high class,,,ametushirikisha namna anavomlea mwanae hilo tu
 
Maisha ni uchaguzi,,anaweza kuwa low income class,, middle au high lakini ameeleza vizuri alivoamua kuishi,,haha mambo ya classes hayana maana sana,,sababu shabby,,abood,,Omar awadh,,Dangote anaweza kuwaita low income class,,wakati mwingine anaweza kuwa anapata 500k tu kwa mwezi akatafsiriwa na wengine Kama middle au high class,,,ametushirikisha namna anavomlea mwanae hilo tu
Siku zote ishi unavyoona ni sahihi bila kuvunja sheria za nchi wala kukiuka maadili na tamaduni, ukianza kufanya maisha yaendane na fulani ni kiashiria cha wazi kwamba upo weak kwenye maamuzi.

Nimetoka hapa youtube kuangalia mahafali cha chuo fulani huko afrika kusini nimeona mtu anaitwa jina lake kuchukua cheti, kaenda na nguo za kitamaduni na kacheza kwa furaha ngoma ya kitamaduni na hakuna alichokosea.
 
Back
Top Bottom