Nilichojifunza kusafiria Pikipiki safari ndefu

Mimi nawaona tu mnavyozifaragua hizo pikipiki. Kwakweli huu mnaouita usafiri kwangu haujawahi kuwa na maana yoyote. Sina mbwembwe nao wala shobo. Navyokwambia hata kuendesha sijui kabisa.

Wewe unasafiri zaidi ya KM 800🤔🤔
 
Pikipiki,baiskeli ni vyombo vya safari fupi tu hapo ulipo.sio safari.
Panda bus,endesha gari ,panda ndege au treni.
Mnapenda sana kumlaumu Mungu mkiwa mnazikwa wakati ujinga mmefanya wenyewe.
Nenda na hiyo pikipiki Dodoma tu hapo tena tuletee mrejesho.
 
Hapo tuuu🤣🤣🤣
 
kwakweli sijutii kabisa kusafiria Pikipiki nilikuwa naogopa sana kutumia pikipiki zenye cc mdogo ila sio hatari kama Wanavyo dai...nili enjoy sana safari za pikipiki.​
Nakuunga mkono, kuna watumiaji wa piki piki wako makundi matano 5.
1. Kundi la kwanza ni The Poor & the destitutes.
Hili ndilo kundi kubwa la watumiaji wa usafiri wa pikipiki kufuatia hali ya umasikini, watu wengi haswa vijijini wanaishi kwenye lindi la umasikini uliotopea ambapo hawana usafiri mwingine wowote tegemeo zaidi usafiri wa
pikipiki。 Hawa ni wale wote wanao lazimika kutumia usafiri wa pikipiki kama usafiri tegemewa kwa kila kitu, wanatumia pikipiki kusafiri mbali kwa sababu ya shida tuu, dharura na hakuna usafiri mwingine affordable.

2. The Mishe Mishe Men. Kuna watu wa mishe mishe za mambo yao fulani fulani za kukwepa mandata mabararani, hivyo hutumia piki piki kupitia njia za panya road ili wasidakwe!.
3. The Hurry Men. Kuna watumiaji wa pikipiki hutumia usafiri wa pikipiki ili kuwahi sehemu, usually maeneo ya mijini yenye foleni kila kona, usafiri wa pikipiki ndio usafiri pekee wa kuwahi.
4. The Ordinary Preferencial
Kuna watu usafiri wa pikipiki kwao ni usafiri wa preference, by choice, kuna usafiri mwingine mwingi, public transport, daladala, uba na bolt, taxi, magari, mabasi, treni na ndege lakini wanachagua kutumia usafiri wa pikipiki just for preference.
5. The Hobby Group both the rich and the ordinary.
Hili ni kundi la watumiaji wa piki piki kwa hobby, usually wanaendesha wenyewe, hawa wanatumia pikipiki as hobby, hawa wanakwenda na pikipiki popote kwasababu wanapenda and it is fun kwao. Ukifanya kitu unachokipenda na una enjoy, huchoki, na mapenzi yakizidi unakuwa blinded unacheza michezo ya hatari na bike bila kugopa!.

Kundi hili lina bike loves wa kawaida wanaotumia pikipiki za kawaida na the rich and the famous ambao wanatumia big bikes,baadhi ya hizi big bikes ni more expensive kuliko magari!。 Hili ndilo kundi langu.

Nilikuwa namiliki pikipiki 5 kwa matumizi mbalimbali.
1. Batavus ya 50 cc ya kuendea dukani hapo jirani.
2. Honda VT 250cc ya kuendea kazini daily
3. Beta 350 off road ya kuchezea michezo ya pikipiki pale Kawe kila Jumapili.
4. Buel 1,200 cc for fun ride, hii ni racing bike, the only one in Tanzania by then, niliinulia US and it costed me a hell!.
5. Harley Davidson 1.800 cc custom made for long safari.
Hii Harley bongo mswahili nilikuwa ni mimi tuu!,wengine wote wenye harley wote ni wazungu!. Hii ndio ilinifanya vibaya na ikaripotiwa humu Pascal Mayalla apata ajali..... na nilipopona nikatoa shukrani humu Waraka wa Pascal Mayalla - Asanteni Sana!

P
 
Mkuu hivi haya madude kwa hapa bongo kuna mafundi wake?
 
Mkuu hizi mbili za mwisho Bado unazo...nije ni test ka feeling ka kudrove motorbike cc 1200 to 1800 sio poa​
 
Nimesafiri pia na boxer bmx domo la mamba 150 this week kutoka mafinga to dsm
 
Mie Juma mosi iliyopita nimetoka Dodoma saa 7 na SunLG kitako cha mbuzi hadi Kondoa 160KM kwa rami,nikatoka kondoa to Kateshi 95 KM rough road nilifika saa 7 usiku hiko Kateshi.Mafuta nilitumia 30K.

Kesho yake nikatoka Kateshi saa 4 asubuhi-Singida Mjini 90KM kwa mafuta ya 10K,nikampuzika kidogo kisha nikaanza safari ya Singida -Dodoma 240KM kwa mafuta ya 20K.

So,kwa ujumla safari nzima nilitembea 590KM kwa mafuta ya 60K,ambapo nilitumia masaa 13.

KAKA KAMA WEWE ULITOKA DAR TO SHY 990KM kwa masaa 12 hongera.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…