econonist
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 20,189
- 29,663
Nilichojifunza kuhusu Africa Kusini kwenye uchaguzi wao , ni yafuatayo:
1. Kwenye uchaguzi wao wameaangalia sera zaidi, sio vyama vya siasa au utumbuizaji wa wasanii kwenye majukwaa ya kampeni. Kwa mfano chama Cha Julius Malema kimeshindwa kuungwa mkono kwa pale alipoleta sera ya kufungua mipaka (Open Border Policy) wasouth wakaachana naye. Sasa hivi chama chake kimeporomoka mpaka nafasi ya nne kwa kujikusanyia asilimia 9 ya kura.
2. Uchaguzi upo wazi. Waandishi wa habari wanaruhusiwa kuhudhuria tukio la kuhesabu kura. Hili limetia moyo Sana. Hata kituo Chao kikuu Cha kujumuisha kura Kiko friendly hakuna mapolisi Wala Usalama kuzuia watu. Matokeo yote yatapatikana kwenye dashboard na kila wakala mkuu wa chama anakuwa na eneo lake la kupokea matokeo kutoka kwa mawakala wake na anaweza kuthibitisha ukweli wake kwa kuangalia matokeo kwenye dashboard.
3. Utendaji wa serikali ndio utategemea mafanikio ya uchaguzi unaofuata. Chama tawala kinapofanya madudu ndio jinsi kinavyojipunguzia uwezekano wa kuendelea kukaa madarakani. Kwenye huu muhula ulioisha ANC imefanya vibaya sana kiutawala, Ajira imekuwa changamoto, umeme, maji na pia Hali ya kiuchumi sio nzuri. Hivyo waafrica Kusini wameamua kupima utendaji wa ANC kwa kura walizoipa.
4. Wasouth wameanza kujifikiria kukipa nafasi chama cha DA ambacho kina chimbuko la wazunguWasouth wanadhani DA inaweza kuirudisha Afrika Kusini kwenye mstari. Maana weusi wenzao akina Zuma ni rushwa tu na Gupta's wake, huku Ramaphosa akifukia mabilioni ya Fedha kwenye mashimo nyumbani kwake mpaka kupeleka wafanyakazi wake wa nyumbani kuanza kufukua na kudokoa hizo pesa.
5. Pia nimejifunza ya kwamba kuwa chama Cha ukombozi sio ticket ya kufanya ufisadi na ujinga mwingine.
ANC walitumia kadi ya kuwa chama Cha ukombozi kufanya madudu na kutojihusisha na mambo ya wananchi, Leo hiyo kadi haifanyi kazi kabisa. Wapiga kura hawajali Nini Wala Nini.
6. Mwisho, uchaguzi wa South Africa umejikita kwenye uchumi zaidi. Ni chama gani kitatoa ahueni ya uchumi ndicho kinasikilizwa na sio vinginevyo.
Ni hayo tu kwa Sasa,
By the Econonist.