Nilichojifunza kwenye Uchaguzi wa South Africa

watu wanataka maendeleo hawataki harakati
Kweli kabisa. Kwa Sasa watu wanataka sera ya maendeleo hasa ya kiuchumi mambo ya propaganda na harakati hawayataki. Natamani upinzani wa Tanzania wajifunze kwenye hili.
 
Nilichojifunza kuhusu Africa Kusini kwenye uchaguzi wao , ni yafuatayo:

1. Kwenye uchaguzi wao wameaangalia sera zaidi, sio vyama vya siasa au utumbuizaji wa wasanii kwenye majukwaa ya kampeni. Kwa mfano chama Cha Julius Malema kimeshindwa kuungwa mkono kwa pale alipoleta sera ya kufungua mipaka (Open Border Policy) wasouth wakaachana naye. Sasa hivi chama chake kimeporomoka mpaka nafasi ya nne kwa kujikusanyia asilimia 9 ya kura.

2. Uchaguzi upo wazi. Waandishi wa habari wanaruhusiwa kuhudhuria tukio la kuhesabu kura. Hili limetia moyo Sana. Hata kituo Chao kikuu Cha kujumuisha kura Kiko friendly hakuna mapolisi Wala Usalama kuzuia watu. Matokeo yote yatapatikana kwenye dashboard na kila wakala mkuu wa chama anakuwa na eneo lake la kupokea matokeo kutoka kwa mawakala wake na anaweza kuthibitisha ukweli wake kwa kuangalia matokeo kwenye dashboard.

3. Utendaji wa serikali ndio utategemea mafanikio ya uchaguzi unaofuata. Chama tawala kinapofanya madudu ndio jinsi kinavyojipunguzia uwezekano wa kuendelea kukaa madarakani. Kwenye huu muhula ulioisha ANC imefanya vibaya sana kiutawala, Ajira imekuwa changamoto, umeme, maji na pia Hali ya kiuchumi sio nzuri. Hivyo waafrica Kusini wameamua kupima utendaji wa ANC kwa kura walizoipa.

4. Wasouth wameanza kujifikiria kukipa nafasi chama cha DA ambacho kina chimbuko la wazunguWasouth wanadhani DA inaweza kuirudisha Afrika Kusini kwenye mstari. Maana weusi wenzao akina Zuma ni rushwa tu na Gupta's wake, huku Ramaphosa akifukia mabilioni ya Fedha kwenye mashimo nyumbani kwake mpaka kupeleka wafanyakazi wake wa nyumbani kuanza kufukua na kudokoa hizo pesa.

5. Pia nimejifunza ya kwamba kuwa chama Cha ukombozi sio ticket ya kufanya ufisadi na ujinga mwingine.
ANC walitumia kadi ya kuwa chama Cha ukombozi kufanya madudu na kutojihusisha na mambo ya wananchi, Leo hiyo kadi haifanyi kazi kabisa. Wapiga kura hawajali Nini Wala Nini.

6. Mwisho, uchaguzi wa South Africa u aimejikita kwenye uchumi zaidi. Ni chama gani kitatoa ahueni ya uchumi ndicho kinasikilizwa na sio vinginevyo.

Ni hayo tu kwa Sasa,

By the Econonist.
Zuma si alikuwa kwenye hiyo serikali ana kipi cha maana cha ofer halafu mtu mwenye tuhuma za rushwa anapataje tena wabunge wengi hapo naona shida kweli
 
Mkuu, wewe unajua Jina langu kunizidi?. Ni Econonist na sio Economist. Kafuatilie kazi ya Econonist ni Nini? Tuwe watu wa tafiti na sio kujifungia kwenye tunayoyajua tu na kulazimishana no please.
Mkuu, nimejaribu kugugo jina lako sijapata majibu, nipo tayari kupata maarifa mapya toka kwako

Sent from my SM-G998U using JamiiForums mobile app
 
Kweli kabisa. Kwa Sasa watu wanataka sera ya maendeleo hasa ya kiuchumi mambo ya propaganda na harakati hawayataki. Natamani upinzani wa Tanzania wajifunze kwenye hili.
huku kwetu harakati lazima ziwepo maana sisi bado tunapambana na katiba yetu ya kiduanzi inayokibeba chama tawala katiba ikikaa poa na tukawa demokrasia ya ukweli naamin tutakuja kufika huko kwa wastaarabu
 
Malema alikuwa anapinga Xenophobia ndio maana amekimbiwa na wapigakura wengi lakini kwangu namuona ndio amekomaa Kisiasa na ni PanAfricanist.

Kumbuka South Africa kuna wahamiaji wengi kutoka Ulaya Mashariki lakini Xenophobia inawaathiri zaidi wahamiaji kutoka Nchi za Kiafrika.
Malema ana sera nyingi za ki-Mugabe amabazo Waafrika Kusini wengi wameona madhara yake kwa jinsi ambavyo Wazimbabwe wamekuwa wakimbizi wa kisiasa na uchumi Afrika Kusini.
 
Mkuu, umechambua vema.

Pia kwa kuongezea ni kwamba ANC kwa miaka 30 kimeshindwa kuwaokoa kimaisha wana am hi wengi ambao ni waafrika. Suala la ajira limekuwa ni gumu kulitatua wakati Afrika Kusini ni nchi tajiri huku kusini mwa jangwa la sahara.

Kukiwa na tatizo la ajira na idadi hiyo ikiongezeka kwaleta uhalifu, chuki kwa wageni na mambo mengi yasofaa.

Pili ANC imegubikwa na vitendo vya Rushwa na Ufisadi kama ulivyosema na hiyo husababisha hata kusahau majukumu yake kama vile kushindwa kuhakikisha kuna umeme wa kutosha.

Afrika Kusini imekuwa ikikumbwa na tatizo la umeme kukatika na kuna wakati usiwepo kabisa jambo linoashiria kwamba serikali ya ANC imewasahau wananchi walk wengi ambao ni waafrika.

Jambo jingine kubwa na muhimu sana lilojionyesha wazi katika uchaguzi huo ni kwamba upinzani wa kweli hutoka ndani ya chama tawala. Haya maneno aliwahi kuyasema hayati baba wa taifa Mwalimu Nyerere kwamba kwa hapa kwetu Tanzania, upinzani wa kweli utatoka ndani ya CCM.

ANC kumuondoa Jacob Zuma kuliwezesha yeye kuvutwa na chama cha MK.

Tukumbuke chama hiki kimedumu miezi sita tu tangu kianze kampeni zake na leo hii kimepunguza idadi kubwa ya wabunge wa ANC bungeni.

Si CCM ambayo mtu akiwa na mawazo tofauti basi huandamwa wee hadi vikao vya Chamwino.

CCM iliwahi kuambiwa na marehemu Horace Kolimba kuwa imepoteza dira na mwelekeo na ikamfanyia kikao Chamwino, leo hii Luhaga Mpina anakosoa lakini ashambuliwa asiseme.

Hili laonyesha unafiki wa hali ya juu kwasababu huwezi kusema upinzani wa kweli watoka ndani ya CCM kisha wale wanokinzana na sera zilizopo wanyamazishwe.

Hivyo basi, katika nchi kama hii yenye uwingi wa wapiga kura werevu wenye uwezo wa kuchambua mambo kimantiki bila kuendekeza uchawa, wao wameamua kuvisogeza vyama vingine hasa DA ili kuwapa ovyo ANC na hii mbinu hutumika kuleta bunge liitwalo Hung Parliament.

Hiyo ndo njia sahihi kwenda mbele ili kuleta maendeleo kwa kila mwananchi maana ANC walikuwa na program waloiita economical black empowerment ambayo iliingia uchawa, nepotism na madudu mengine yaso na maana na ikasahaulika.
 
Inaweza kuwa. Ila nilifanya intentionally na sio misspelling. Ingawa watu wengi wanalazimisha iwe Economist.
Uko sahihi mkuu! Nashangaa sikuliona hilo. Hiyo ni ID yako na siyo kama wengi tulivyokuwa tukifikiria.
 
Nilichojifunza kuhusu Africa Kusini kwenye uchaguzi wao , ni yafuatayo:

1. Kwenye uchaguzi wao wameaangalia sera zaidi, sio vyama vya siasa au utumbuizaji wa wasanii kwenye majukwaa ya kampeni. Kwa mfano chama Cha Julius Malema kimeshindwa kuungwa mkono kwa pale alipoleta sera ya kufungua mipaka (Open Border Policy) wasouth wakaachana naye. Sasa hivi chama chake kimeporomoka mpaka nafasi ya nne kwa kujikusanyia asilimia 9 ya kura.

2. Uchaguzi upo wazi. Waandishi wa habari wanaruhusiwa kuhudhuria tukio la kuhesabu kura. Hili limetia moyo Sana. Hata kituo Chao kikuu Cha kujumuisha kura Kiko friendly hakuna mapolisi Wala Usalama kuzuia watu. Matokeo yote yatapatikana kwenye dashboard na kila wakala mkuu wa chama anakuwa na eneo lake la kupokea matokeo kutoka kwa mawakala wake na anaweza kuthibitisha ukweli wake kwa kuangalia matokeo kwenye dashboard.

3. Utendaji wa serikali ndio utategemea mafanikio ya uchaguzi unaofuata. Chama tawala kinapofanya madudu ndio jinsi kinavyojipunguzia uwezekano wa kuendelea kukaa madarakani. Kwenye huu muhula ulioisha ANC imefanya vibaya sana kiutawala, Ajira imekuwa changamoto, umeme, maji na pia Hali ya kiuchumi sio nzuri. Hivyo waafrica Kusini wameamua kupima utendaji wa ANC kwa kura walizoipa.

4. Wasouth wameanza kujifikiria kukipa nafasi chama cha DA ambacho kina chimbuko la wazunguWasouth wanadhani DA inaweza kuirudisha Afrika Kusini kwenye mstari. Maana weusi wenzao akina Zuma ni rushwa tu na Gupta's wake, huku Ramaphosa akifukia mabilioni ya Fedha kwenye mashimo nyumbani kwake mpaka kupeleka wafanyakazi wake wa nyumbani kuanza kufukua na kudokoa hizo pesa.

5. Pia nimejifunza ya kwamba kuwa chama Cha ukombozi sio ticket ya kufanya ufisadi na ujinga mwingine.
ANC walitumia kadi ya kuwa chama Cha ukombozi kufanya madudu na kutojihusisha na mambo ya wananchi, Leo hiyo kadi haifanyi kazi kabisa. Wapiga kura hawajali Nini Wala Nini.

6. Mwisho, uchaguzi wa South Africa umejikita kwenye uchumi zaidi. Ni chama gani kitatoa ahueni ya uchumi ndicho kinasikilizwa na sio vinginevyo.

Ni hayo tu kwa Sasa,

By the Econonist.
I beg to differ from your point.
 
Pia Rais aliyeko madarakani alikubali sauti za WATU siyo huku kwetu ungeshsngaa wanapindua meza
 
Ndugu Economist matokeo ya kujifunza kwako kunaweza vipi kuwaamsha wadanganyika waliolala,ili watoke walipo kwamia?
 
econonist
Ni moja ya mabandiko mazuri wiki hii, natamani kungekuwa na mijadala ya namna hii. Kudos

1. ANC kama ilivyo CCM wanasafiria nyota ya Ukombozi. Kwa South Africa (SA) ANC inajivunia kuondoa apartheid (ubaguzi wa rangi). Nusu ya Wapiga kura wamezaliwa miaka ya 1995 wengi hawakumona Mandela akiwa jela achilia mbali akitoka Jela. Hiki ni kizazi cha Gen X and Gen Z

Unemployment rate ni takribani 29% kukiwa na matatizo ya kijamii ikiwemo Uhalifu uliokithiri n.k.
Ukiwaeleza Gen Z and Gen X kuhusu ubaguzi hilo si tatizo kwao, tatizo ni unemployment and their future katika nchi iliyokuwa karibu na ''first world''.

2. Ushahidi kwamba Gen Z and Gen X hawajali ubaguzi ni pale walipopigia chama cha Wazungu. Kwao sera za uchumi ni muhimu kuliko majigambo ya kuondoa apartheid. Vijana hao wanaona ''future' yao kiuchumi ni muhimu kuliko kuwagawa kwa makundia na hapa ndipo EFF ya malema inapoingia

3. EFF wana sera ya kuwawezesha Watu weusi. Watu wa SA wanasema tatizo si rangi kama ilivyokuwa kwa wazungu, tatizo ni uchumi. Wamewapiga chini EFF kwasababu hawana sera za kuinua hali za watu bali wanatumia rangi kama sera, kosa lile lile la makaburu

Funzo, watu wa SA wana mtazamo mkubwa sana wa masuala ya nchi yao kuliko Watanzania.

Tunaweza kusema katika nchi za SADC na EAC Tanzania ndio nchi yenye watu wasioweza kupambanua maisha yao na siasa , wasioweza kupambanua siasa na uchumi na wanaoishi kwa mazoea na si mipango! Sorry

JokaKuu
 
Back
Top Bottom