Nilichojifunza kwenye Uchaguzi wa South Africa

More reason kumonitor watu wanaotumia asili yao kupata kura. Kufikia Kenya walipo ni sekunde Moja. Pia dini imeanza kujipenyeza kwenye maamuzi ya kiserikali. Mbegu ndogo inaanza kuota mizizi na kutoa matawi. Kifuatacho ni kiama
 
Lakini Msukuma hana Ujasiri wa Mzulu.Mzulu anajua anafanya nini lakini Msukuma amekalia kula Miwa tu.
 
😂😂 Nimecheka kwa nguvu, nenda kwenye mkutano wa kampeni wa karibia masaa matatu. Masaa mawili ni ya burusani, nusu saa ni ya wapambe kupiga vijembe na kumwaga tambo. 10 ni za mgombea kupiga porojo, na kama kina maswali, basi ni mawili matatu ya watu walipangwa. Kisha 15 za wapambe kuaga.

Siku ya uchaguzi zinaletwa kura za kubumba, huku mtangaza matokeo akiwa ameshapewa maagizo ya nani atangazwe mshindi. Ukitaka kucheka itisha mdahalo, hakuna anayetaka anasema kazi zake zinajieleza. Na hayuko tayari kuhojiwa! Cha ajabu unakuta watu wa aina hiyo wanawekea wananchi maneno mdomoni kuwa wanakubalika!
 
Mwisho wa vyama "VIKONGWE" umekaribia, wajitayarishe kisailolojia soon nao wataitwa vyama vya "UPINZANI"
 
Kweli kabisa mkuu. Sijui Zuma aliwezaje kupenya mpaka kuwa Rais. Maana Hata Mandela wakati anakaribia kustaafu alimfikiria Ramaphosa Kama mrithi wake ukiachilia Mbeki.
 
More reason kumonitor watu wanaotumia asili yao kupata kura. Kufikia Kenya walipo ni sekunde Moja. Pia dini imeanza kujipenyeza kwenye maamuzi ya kiserikali. Mbegu ndogo inaanza kuota mizizi na kutoa matawi. Kifuatacho ni kiama
Yes. Kile kilichotokea mwaka wa 2015 kisijirudie. Kutumia kadi ya kikabila kwenye kuchagua sio afya au kutumia Lugha ya nyumbani kwenye kampeni Tena live kwenye TV.

Hili suala la udini inabidi waliangalie kwa ukatibu Sana. Wakiliachia hivi hivi matokeo yake yatakuwa sio mazuri.
 
Yani ni shida Mkuu. Bado tupo nyuma Sana kwenye chaguzi zetu.
 
Kweli kabisa mkuu. Sijui Zuma aliwezaje kupenya mpaka kuwa Rais. Maana Hata Mandela wakati anakaribia kustaafu alimfikiria Ramaphosa Kama mrithi wake ukiachilia Mbeki.
Zuma ni street fighter but corrupt. Anaweza retail politics lakini Hana strategy ya kuongoza. Kukosa kwake strategy kukawanufaisha waeshia wachache. Halafu tayari ana baggage ya corruption kwenye yale manunuzi ya kijeshi. Ni rahisi kuleverage corruption kupata kitu Kwa mtu maana tayari mna file lake chafu.
 
Tatizo tuna usalama wa Taifa ambao wengi hawana merits za kuwa pale. Ukiangalia NSA au FBI au CIA huingii kama wewe ni bogus. Kwetu kadi ya chama ndo kielelezo namba Moja. Tunahitaji watu wenye uwezo wa kuona Kwa macho matatu. Kama sasa hivi nyuzi za kidini hapa JF zimepamba moto. Kuna wakati mpaka nahofu kwamba pameshageuka kuwa recruiting space Kwa vitu visivyoo faa. We need to be vigilant. They start small. Kama tumeweza kubarn porn Kwa asilimia kubwa basi tunaweza kubarn na hizi extremist views. Kuna indoctrination inaendelea kubwa mno. Tutashtuka tukiwa tumeshachelewa. Time is now. Not yesterday or tomorrow, Now!
 
Kumbe haukujifunza lolote kama hukusema kuwa katiba Yao ni imara na ndiyo nguzo kuu Kwa mustakabali wa afya ya taifa huru la Afrika ya kusini.
 
Taifa lolote lile bila kuwa na katiba imara kamwe haliwezi kuwa na uchaguzi huru na wa haki
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…