Nilichojifunza Nanenane: Kufanya Kazi Halmashauri ni kupoteza muda na kukaribisha umasikini tu

Sasa Mama Samia, kwanini watumishi wa serikali ni sawa na Wana baba mmoja (serikali ya CCM) halafu mishahara tofauti?

#YNWA
Ndugu yangu mwenyekiti wa wakataa ndoa jitahidi sana uje uione pepo (mbingu) maana inasemekana huko pekee ndo kuna usawa. Kwa hapa duniani hakutakaa kuwe sawa.
 
Dah hii imeniuma sanaaaa.
To yeye hebu soma hii.

#YNWA
 
Kweli kabisa mkuu. Kwanza kwenye halmashauri kuna ujinga mwingi sana ambao hauvumiliki hata kidogo
 
Mkurugenzi wako uelewa wake mdogo ,ndio maana akakujib hivyo .
Ila Mwanadam akiwa katka mazingira aina tatu uwaga anaongea ukweli
1. Ulevi
2. Utani
3. Hasira
Katka mazingira hayo mtu akikwambia kifanyie kazi.
 
""Mimi nilidhani unazungumzia kuwa halmashauri/wilaya/miji midogo zimeshindwa kuonyesha na kuwasilisha yale wanayoyafanya huko makwao,""
JIBU:- Zimeshindwa kuonyesha nini, mbona miradi inajengwa na wananchi wanahudumiwa?

""kumbe wewe unalilia hapa kwa ajili ya tumbo lako""
JIBU:- Bila tumbo lako kuwa sawa hata hii comment ungeandika?

""unataka ufananane na mtu wa TRA na ukalale hoteli ya nyota tano,kwani ndicho ulichoendea""
JIBU:- Nataka maslahi sawa kwa watumishi wotee wa umma.

""hebu nawe jilinganisha na wale waliokuja kuonyesha shughuli zao chi ya hizo halmashauri kama nao wanaishi sawa na wewe""
JIBU:- Tunaongelea serikalini.

""halafu nyie mkiwa huko mawilayani kwenu mnajifanya miungu watu, mumejaa urasimu na huduma mbovu kwa watu masikini. Huduma mbovu halafu unataka upate stahiki sawa na taasisi kama Brela,BOAT ,TRA?""
JIBU:- Huko BOT, BRELA, TRA ndio wanahuduma nzuri mpaka wanastahili mishahara mikubwa zaidi ya local government?

#YNWA
 
Nilienda halmashauri moja hivi asubuhi asubuhi nikakuta wakuu wa idara wana kikao, nikasema ngoja nipate supu kwenye mgahawa uliyopo hapo halmashauri

Nauliza supu nambiwa supu inapatikana mwisho wa mwezi mshahara ukitoka tu zile siku tatu za mwanzoni ndio kuna supu, nikahoji kuna nini wakasema chai ya rangi na mandazi, kuna mihogo ya kuchemsha na karanga, nikawaza sana nikapata jibu kwanini watumishi wa halmashauri wana sonona, majungu makasiriko kwa watumishi waliopo chini yao.
 
Huu uzi umenichekesha sana comment za watu πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ mnawawafanya job seekers waogope kwenda halmashauri ndo mana kuna watu wamepangiwa kazi halmashauri huko misungwi, ukerewe hawajaenda kuripoti πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Mkurugenzi wako uelewa wake mdogo ,ndio maana akakujib hivyo .
Ila Mwanadam akiwa katka mazingira aina tatu uwaga anaongea ukweli
1. Ulevi
2. Utani
3. Hasira
Katka mazingira hayo mtu akikwambia kifanyie kazi.

In vino veritas
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…