Nilichojifunza Nanenane: Kufanya Kazi Halmashauri ni kupoteza muda na kukaribisha umasikini tu

Nilichojifunza Nanenane: Kufanya Kazi Halmashauri ni kupoteza muda na kukaribisha umasikini tu

Sasa Mama Samia, kwanini watumishi wa serikali ni sawa na Wana baba mmoja (serikali ya CCM) halafu mishahara tofauti?

#YNWA
Ndugu yangu mwenyekiti wa wakataa ndoa jitahidi sana uje uione pepo (mbingu) maana inasemekana huko pekee ndo kuna usawa. Kwa hapa duniani hakutakaa kuwe sawa.
 
Pia nyie wafanya kazi wa halmashauri huwa ni lazima muwe na kampauko fulani hivi. Iwe kimuonekano, kimitazamo, kiutendaji, hata muwe na hela vipi, mtu akiwaona tu lazima atawajua kuwa hawa ni wa halmashauri. Hata uwe sista du au braza men, lazima tu utajua huyu ni wa halmashauri.

Hata muagize gari pamoja, baada ya wiki utajua tu mwenye hili gari ni staff wa halmashauri.
Nadhani yote hii inatokana na tabia zenu za ufujaji na kuto wajibika kama inavyotarajiwa na kutokuwa innovative na kuwa money oriented na pia utendaji wenu kuwa ni ule wa lazy affairs.

Mtu akiona vitambi, miondoko anajua kuwa hii ni mikato ya OC, recurrent, Gov, in kind n.k
Yote hii ni sababu ya tabia na utendaji wenu kuwa na athari za moja kwa moja kwa raia, lakini hamjali, hivyo mnakua kama wachawi wala nyama za watu, hii inapelekea mnakua kama watu wenye laana ila ni vile hamjijui.
Dah hii imeniuma sanaaaa.
To yeye hebu soma hii.

#YNWA
 
INTRODUCTION:
Kwanza kabisa Mimi Mr. Liverpool ni mtumishi wa umma ndani ya Halmashauri kwa muda wa miaka 11. Miaka 5 nimekuwa Shule na 6 ndio kazini.
Niko kwenye Halmashauri iliyo chaka sanaaa.

SCENARIO
Tokea nifike Nanenane 01/08 Mbeya nimekuwa nikitembelea mabanda ya ofisi nyengine kujifunza.

Nilichojifunza kufanya Kazi Halmashauri iwe Manispaa, Wilaya, Mji mdogo au ""What so ever"" ni kupoteza muda tuu.

Kuna utofauti mkubwa sanaa kati ya Taasisi na Halmashauri.
Japo wote tupo serikali moja ila Taasisi ni watoto pendwa wa serikali.

Nimetembelea mabanda ya Taasisi kama
1. BOT
2. EWURA
3. TRA
4. Zile za kilimo kama PASSS na TANTRADE
5. BRELA
6. N.k

Lakini pia nimetembelea mabanda ya Halmashauri kama
1. Mlele
2. Tanganyika
3. Mbalari
4. Ileje
5. Songwe
6. Mafinga
7. Momba
8. Kalambo
9. Nsimbo
10. Kilolo
11. N.k

Ila nimeona utofauti mkubwa sanaa.....

THE PROBLEM
1. Sehemu za kulalia (Hotel na Lodge)

Kuanzia njia ya Uyole mpaka Kabwe Hadi Mbalizi kuna hoteli nyingi tu, ila kwa posho za Halmashauri huwezi lala hizo Hotel, mule hotelini kumejaa gari za ST... na SU tu. Hakuna SM kabisaaa.
Kuna mshikaji wangu yupo PASS kalala kwenye hoteli ya Laki per night huku Mimi nimelala lodge ya 20,000 per night (kila mtu kala kulingana na urefu wa per diem yake).

2. Muonekano wa mabanda
Hebu tembelea banda la H/W Mlele, Nsimbo, Sumbawanga au Mafinga halafu nenda BRELA, TRA au BOT ndio Utanielewa.

3. Hali wa watumishi
Ukitembelea mabanda ya Taasisi utakuta raia wako charming sanaa, nyuso za furaha na kukukaribisha vizurii.

Ila Halmashauri sasa, Mungu atusaidie, maana raia wamepoteza hope kabisa.

Kwanza wengine posho wamekopwa na wakurugenzi wao..!!!

4. Magari
Hebu angalia ndinga za SU na SM.
Hebu cheki tu external appearance UTANIELEWA.
Hebu chukua V8 ya BOT au Wizara ya Fedha halafu pembeni weka V8 ya Njombe au Kalambo, Utanielewa tu.

CONCLUSION
Halmashauri hakuna maisha na hasa hizi DC ndio Umasikini fullll.

Kijana mtafuta ajira, ukipata ajira SM aisee cha kwanza fikiria kuhama na pambana kuhama.

Kijana mtafuta ajira, njoo SM chukua "cheki namba" halafu sepaa kale maisha Taasisi.

Note:- Kuhama SM sio rahisi ila Inawezekana.

Mimi ni mmoja wapo lazima nihame huku SM, siioni kesho yangu nikiwa hii DC iliyo kijijini hivi.

Yaani Mimi ya Masters yangu siwezi staafia huku kijijini halafu Kuna raia wapo DSM, Mwanza, Mbeya, kifupi wapo mjini wanakula maisha ya Taasisi.

Aisee siwezi kukubali, KUHAMA KWENDA TAASISI NI LAZIMA.
Iwe hata kwa hela ila NITAHAMA TU..!!

NOTE
Mbele ya macho ya serikali ya CCM sisi watumishi ""We are all equal, but some people are more equal""

YNWA
Kweli kabisa mkuu. Kwanza kwenye halmashauri kuna ujinga mwingi sana ambao hauvumiliki hata kidogo
 
Hakuna asiyetaka maisha mazuri.
Juzi nimelalia Mbeya pazuri.
Nikiwa Niko full na Castle lite zangu kichwani nikamropokea mkurugenzi wangu ""Uchaguzi wa 2025 hauwezi kunikuta kwenye halmashauri yako" yaani Mimi na li-masters langu nifie kijijini. HAIWEZEKANIII

Aliniangaliaaa akanijibu "Pombe hizo" [emoji2960][emoji2960][emoji2960][emoji2960]

#YNWA
Mkurugenzi wako uelewa wake mdogo ,ndio maana akakujib hivyo .
Ila Mwanadam akiwa katka mazingira aina tatu uwaga anaongea ukweli
1. Ulevi
2. Utani
3. Hasira
Katka mazingira hayo mtu akikwambia kifanyie kazi.
 
Mimi nilidhani unazungumzia kuwa halmashauri/wilaya/miji midogo zimeshindwa kuonyesha na kuwasilisha yale wanayoyafanya huko makwao,kumbe wewe unalilia hapa kwa ajili ya tumbo lako,unataka ufananane na mtu wa TRA na ukalale hoteli ya nyota tano,kwani ndicho ulichoendea, hebu nawe jilinganisha na wale waliokuja kuonyesha shughuli zao chi ya hizo halmashauri kama nao wanaishi sawa na wewe. halafu nyie mkiwa huko mawilayani kwenu mnajifanya miungu watu, mumejaa urasimu na huduma mbovu kwa watu masikini. Huduma mbovu halafu unataka upate stahiki sawa na taasisi kama Brela,BOAT ,TRA?
""Mimi nilidhani unazungumzia kuwa halmashauri/wilaya/miji midogo zimeshindwa kuonyesha na kuwasilisha yale wanayoyafanya huko makwao,""
JIBU:- Zimeshindwa kuonyesha nini, mbona miradi inajengwa na wananchi wanahudumiwa?

""kumbe wewe unalilia hapa kwa ajili ya tumbo lako""
JIBU:- Bila tumbo lako kuwa sawa hata hii comment ungeandika?

""unataka ufananane na mtu wa TRA na ukalale hoteli ya nyota tano,kwani ndicho ulichoendea""
JIBU:- Nataka maslahi sawa kwa watumishi wotee wa umma.

""hebu nawe jilinganisha na wale waliokuja kuonyesha shughuli zao chi ya hizo halmashauri kama nao wanaishi sawa na wewe""
JIBU:- Tunaongelea serikalini.

""halafu nyie mkiwa huko mawilayani kwenu mnajifanya miungu watu, mumejaa urasimu na huduma mbovu kwa watu masikini. Huduma mbovu halafu unataka upate stahiki sawa na taasisi kama Brela,BOAT ,TRA?""
JIBU:- Huko BOT, BRELA, TRA ndio wanahuduma nzuri mpaka wanastahili mishahara mikubwa zaidi ya local government?

#YNWA
 
Nilienda halmashauri moja hivi asubuhi asubuhi nikakuta wakuu wa idara wana kikao, nikasema ngoja nipate supu kwenye mgahawa uliyopo hapo halmashauri

Nauliza supu nambiwa supu inapatikana mwisho wa mwezi mshahara ukitoka tu zile siku tatu za mwanzoni ndio kuna supu, nikahoji kuna nini wakasema chai ya rangi na mandazi, kuna mihogo ya kuchemsha na karanga, nikawaza sana nikapata jibu kwanini watumishi wa halmashauri wana sonona, majungu makasiriko kwa watumishi waliopo chini yao.
 
Mkurugenzi wako uelewa wake mdogo ,ndio maana akakujib hivyo .
Ila Mwanadam akiwa katka mazingira aina tatu uwaga anaongea ukweli
1. Ulevi
2. Utani
3. Hasira
Katka mazingira hayo mtu akikwambia kifanyie kazi.

In vino veritas
 
Back
Top Bottom