Nilichojifunza Nanenane: Kufanya Kazi Halmashauri ni kupoteza muda na kukaribisha umasikini tu

Nilichojifunza Nanenane: Kufanya Kazi Halmashauri ni kupoteza muda na kukaribisha umasikini tu

Kwanini usijiajiri mkuu? Naamini mishahara kwa watumishi wa umma imepishana kidogo kwa kada husika,labda uwe mwanasiasa ndio utapiga pesa.

Lakini katika ajira za kutumikia umma wote tupo katika mtumbwi mmoja
Siyo kweli.
Kuna tofauti kubwa sana kati ya Halmashauri na Mashirika ya Umma au zile wanaita 'Mamlaka ya ....'
 
kila siku nasisitiza kufanya kazi halmashauri sijui serikali ya wapi, kwa ujumla utumishi wa umma wa kibongo ni kama kalaana flani hivi , kama vipi piga tukio huko kijijini usepe, hamna maana wana wanakula bata town wewe unakaa kileji na elimu yako piga bunda mzee baba utakuja kunishukuru baadaye.
Tupe rada ya tukio haf tunasepaje wasiojulikana wapo kila kona TZ si watanidaka na kunifilisi vihela nilivyoiba.
 
Kuonana na mtu yoyote wa JF kwa kweli hili swali LIMENISHINDA.

Kuna siku nilipost kuhusu biashara ya vinywaji "Nina miaka 7 Niko kwenye biashara ya vinywaji"
Watu wengi tu walinifata PM kuomba namba ya simu ili wajifunze hii biashara, ila SIWEZI KWA KWELI.

Cha MUHIMU ni tuchat tu na tumalizane hukohuko PM.

#YNWA
Create new account kwa ajili ya positive issues ili uwe connected.
2019 niliona tangazo la shamba jamaa kaweka no. zake nilimtafuta mpaka tukaliona shamba. Kwa hio JF sio tu kwamba ina watu wabaya au matapeli.
Wapo watu wanahitaji huduma yako, kama huna baya humu vipi uogope watu.
Umeanzisha genge la uhalifu humu?
Wengi humu wana acc 2.
Hili jukwaa unaweza kulitumia hata kibiashara kama huyo dalali wa mashamba.
Ifike mahala tuwe positive ili kutumia watu kuuuza huduma au kupata huduma.
 
Kwanini usijiajiri mkuu? Naamini mishahara kwa watumishi wa umma imepishana kidogo kwa kada husika,labda uwe mwanasiasa ndio utapiga pesa.

Lakini katika ajira za kutumikia umma wote tupo katika mtumbwi mmoja
Sio kweli.
HR mwenye bachelor aliyeanza Kazi Leo akiwa Halmashauri ni TGS D = 745K akianza BRELA 1.8mil

Mwalimu mwenye bachelor akianza Kazi Kufundisha Shule za Halmashauri TGST D = 745K na akiwa Tutor assistant chuoni ni zaidiii.

Serikali kwenye mishahara HAINA USAWA KABISAAA.

#YNWA
 
Poleni sana watumishi. Ila msisahau kuwa binadamu hatuko sawa. Wengi tuliopo nje ya ajira rasmi za kuajiriwa tunawaonea wivu nyie. Cha muhimu ni kila mmoja kutumia vizuri alichonacho mkononi ili kimtoe kwenye hali ngumu ya kiuchumi kwenda kwenye haliz nzuri.
 
Poleni sana watumishi. Ila msisahau kuwa binadamu hatuko sawa. Wengi tuliopo nje ya ajira rasmi za kuajiriwa tunawaonea wivu nyie. Cha muhimu ni kila mmoja kutumia vizuri alichonacho mkononi ili kimtoe kwenye hali ngumu ya kiuchumi kwenda kwenye haliz nzuri.
Sasa Mama Samia, kwanini watumishi wa serikali ni sawa na Wana baba mmoja (serikali ya CCM) halafu mishahara tofauti?

#YNWA
 
INTRODUCTION:
Kwanza kabisa Mimi Mr. Liverpool ni mtumishi wa umma ndani ya Halmashauri kwa muda wa miaka 11. Miaka 5 nimekuwa Shule na 6 ndio kazini.
Niko kwenye Halmashauri iliyo chaka sanaaa.

SCENARIO
Tokea nifike Nanenane 01/08 Mbeya nimekuwa nikitembelea mabanda ya ofisi nyengine kujifunza.

Nilichojifunza kufanya Kazi Halmashauri iwe Manispaa, Wilaya, Mji mdogo au ""What so ever"" ni kupoteza muda tuu.

Kuna utofauti mkubwa sanaa kati ya Taasisi na Halmashauri.
Japo wote tupo serikali moja ila Taasisi ni watoto pendwa wa serikali.

Nimetembelea mabanda ya Taasisi kama
1. BOT
2. EWURA
3. TRA
4. Zile za kilimo kama PASSS na TANTRADE
5. BRELA
6. N.k

Lakini pia nimetembelea mabanda ya Halmashauri kama
1. Mlele
2. Tanganyika
3. Mbalari
4. Ileje
5. Songwe
6. Mafinga
7. Momba
8. Kalambo
9. Nsimbo
10. Kilolo
11. N.k

Ila nimeona utofauti mkubwa sanaa.....

THE PROBLEM
1. Sehemu za kulalia (Hotel na Lodge)

Kuanzia njia ya Uyole mpaka Kabwe Hadi Mbalizi kuna hoteli nyingi tu, ila kwa posho za Halmashauri huwezi lala hizo Hotel, mule hotelini kumejaa gari za ST... na SU tu. Hakuna SM kabisaaa.
Kuna mshikaji wangu yupo PASS kalala kwenye hoteli ya Laki per night huku Mimi nimelala lodge ya 20,000 per night (kila mtu kala kulingana na urefu wa per diem yake).

2. Muonekano wa mabanda
Hebu tembelea banda la H/W Mlele, Nsimbo, Sumbawanga au Mafinga halafu nenda BRELA, TRA au BOT ndio Utanielewa.

3. Hali wa watumishi
Ukitembelea mabanda ya Taasisi utakuta raia wako charming sanaa, nyuso za furaha na kukukaribisha vizurii.

Ila Halmashauri sasa, Mungu atusaidie, maana raia wamepoteza hope kabisa.

Kwanza wengine posho wamekopwa na wakurugenzi wao..!!!

4. Magari
Hebu angalia ndinga za SU na SM.
Hebu cheki tu external appearance UTANIELEWA.
Hebu chukua V8 ya BOT au Wizara ya Fedha halafu pembeni weka V8 ya Njombe au Kalambo, Utanielewa tu.

CONCLUSION
Halmashauri hakuna maisha na hasa hizi DC ndio Umasikini fullll.

Kijana mtafuta ajira, ukipata ajira SM aisee cha kwanza fikiria kuhama na pambana kuhama.

Kijana mtafuta ajira, njoo SM chukua "cheki namba" halafu sepaa kale maisha Taasisi.

Note:- Kuhama SM sio rahisi ila Inawezekana.

Mimi ni mmoja wapo lazima nihame huku SM, siioni kesho yangu nikiwa hii DC iliyo kijijini hivi.

Yaani Mimi ya Masters yangu siwezi staafia huku kijijini halafu Kuna raia wapo DSM, Mwanza, Mbeya, kifupi wapo mjini wanakula maisha ya Taasisi.

Aisee siwezi kukubali, KUHAMA KWENDA TAASISI NI LAZIMA.
Iwe hata kwa hela ila NITAHAMA TU..!!

NOTE
Mbele ya macho ya serikali ya CCM sisi watumishi ""We are all equal, but some people are more equal""

YNWA
Mimi nilidhani unazungumzia kuwa halmashauri/wilaya/miji midogo zimeshindwa kuonyesha na kuwasilisha yale wanayoyafanya huko makwao,kumbe wewe unalilia hapa kwa ajili ya tumbo lako,unataka ufananane na mtu wa TRA na ukalale hoteli ya nyota tano,kwani ndicho ulichoendea, hebu nawe jilinganisha na wale waliokuja kuonyesha shughuli zao chi ya hizo halmashauri kama nao wanaishi sawa na wewe. halafu nyie mkiwa huko mawilayani kwenu mnajifanya miungu watu, mumejaa urasimu na huduma mbovu kwa watu masikini. Huduma mbovu halafu unataka upate stahiki sawa na taasisi kama Brela,BOAT ,TRA?
 
Tena walimu ndokabisa utafikiri escape from sobibor
[emoji16][emoji16], wanajichekesha wakiona Dem, unawazingua nipe Ela ya chai hata buku hawatoi hii hapa kwenye chupa, kada nyingine ukiwazingua zinatoka tu.
 
Back
Top Bottom