Nilichojifunza Uchaguzi wa Kenya: Tuwape nafasi Matajiri na Watafutaji

Siasa za Kenya sizitofautishi sana na siasa za Marekani! Wao wanaamini sana katika kumpa nafasi mtu anayeonesha ana uwezo wa kutafuta pesa na kupambana kupata pesa! Ndo mana inawezekana hata kiuchumi wako vizuri kuzidi sisi ingawa na sie tunajikongoja kuwafikia

Wakenya sio waumini sana wa ngonjera za sijui nichagueni mimi sio mwizi, mimi sio fisadi kwa sababu wanajua watu wanaopenda kujivika hizo sifa sio watu wenye akili za kimaendeleo na hawawezi kuhimiza vizuri maendeleo yao!

Kutoka kwa Jomo Kenyata mpaka kwa Daniel Arap Moi, kuja kwa Kibaki mpaka kwa Uhuru Kenyata na sasa naona Hustler William Ruto anaenda kubeba ndoo.

Wote ni watu wenye ukwasi ambao wako proud na ukwasi wao na wanatumia ukwasi wao kama njia ya ku motivate watu wengine kuwa na ukwasi.

Tanzania tujifunze hili kutoka Kenya mambo ya mtu kujisifia umaskini na kujiona ndo ticket k ya kuwa kiongozi tuachane nayo.

Kuanzia saivi tuanze kuangalia maisha ya mtu kama anajiweza kiuchumi vizuri, ana mali anazoziendesha vizuri, ana nyumba nzuri na ya kisasa na ana biashara nzuri ambayo ana imanage vizuri kama kigezo cha kumpa mtu uongozi.

Suala la kuteua sijui mtu hohehae asiye na mbele wala nyuma huku tukitegemea apandishe uchumi wetu liwe mwisho kuanzia leo.
Mkuu with due respect
Leo unenibadlisha sana fikra zangu,
nilitegemea kwa ufisadi anaohusishwa nao Ruto wakenya wangempiga chini mapema ,
Hustlers wanaweza kuwa ndio chaguo sahibi kwa maendeleo
 
Una hoja, ila huku haiwezekani, watu wanachukia walionacho, nimeshafanya uchunguzi mitandaoni, zaidi ya 70% ya watanzania hawapendi mwenzao aishi vizuri
Mindset za aina hii zinaendeshwa na sera za kijamaa
 
Kenya ni Mabepari Hilo Haina ubishi.

Hata Marekani na ulaya ni Mabepari, hawana tatizo na TAJIRI kugombea ikiwa tu, atakuwa Hana DOA ktk utajiri wake, awe clean kulipa MAPATO na KODI.

Huku kwetu hatujui ikiwa tu WAJAMAA au Mabepari.

Matajiri wa huku ni WAKWEPA Kodi, wanatumia pesa walizopata kupitia kukwepa Kodi kununua wapiga kura.

Hivyo ktk muktadha huo lazima matajiri wachukiwe sababu utajiri wao Si halali, mfano wanaotupandishia Bei za mafuta ktk biashara zao za mafuta ndo wabunge wetu na mawaziri.

Ni kheri achaguliwe msomi, asiye na kitu awe kiongozi, KATIBA mpya na Sheria nzuri zimdhibiti.

Ameeeen
Msomi asiye na kitu ni hatari sana kwenye siasa za kijamaa,
Ndo anajifunza wizi na unafiki kwa level ya juu kabisa
 
Siasa za Kenya sizitofautishi sana na siasa za Marekani! Wao wanaamini sana katika kumpa nafasi mtu anayeonesha ana uwezo wa kutafuta pesa na kupambana kupata pesa! Ndo mana inawezekana hata kiuchumi wako vizuri kuzidi sisi ingawa na sie tunajikongoja kuwafikia

Wakenya sio waumini sana wa ngonjera za sijui nichagueni mimi sio mwizi, mimi sio fisadi kwa sababu wanajua watu wanaopenda kujivika hizo sifa sio watu wenye akili za kimaendeleo na hawawezi kuhimiza vizuri maendeleo yao!

Kutoka kwa Jomo Kenyata mpaka kwa Daniel Arap Moi, kuja kwa Kibaki mpaka kwa Uhuru Kenyata na sasa naona Hustler William Ruto anaenda kubeba ndoo.

Wote ni watu wenye ukwasi ambao wako proud na ukwasi wao na wanatumia ukwasi wao kama njia ya ku motivate watu wengine kuwa na ukwasi.

Tanzania tujifunze hili kutoka Kenya mambo ya mtu kujisifia umaskini na kujiona ndo ticket k ya kuwa kiongozi tuachane nayo.

Kuanzia saivi tuanze kuangalia maisha ya mtu kama anajiweza kiuchumi vizuri, ana mali anazoziendesha vizuri, ana nyumba nzuri na ya kisasa na ana biashara nzuri ambayo ana imanage vizuri kama kigezo cha kumpa mtu uongozi.

Suala la kuteua sijui mtu hohehae asiye na mbele wala nyuma huku tukitegemea apandishe uchumi wetu liwe mwisho kuanzia leo.
Maskini huwa tuna roho za visasi sn
 
Den Xiaoping alipelekwa kusoma ulaya akakaa na matajiri akajifunza kwa matajiri wanavyoenenda na kufanya. Ndo mana aliporudi China alirudi na mindset ya kitajiri kuwa it doesn't matter if a cat is white or black as long as it catches a mice it's a good cat!

Tanzania hakunq maskini mwenye akili za kitajiri
Wewe jamaa ni mtu wa ajabu sana hata haukumbuki ulichoandika mwanzo.
 
Sasa chini ya mfumo wa Mao huyo Den Xiaoping angepata wapi utajiri?

Mabadiliko aliyoyaweza kuyafanya ni kutokana na kupata nafasi ya kusoma kwa matajiri ndo akapata akili za kitajiri na kuifanya China kufanya mabadiliko na kuwa matajiri

Hivi unafahamu hata China uongozi watu wanapataka kwa kutumia vigezo gani?
 
Sasa chini ya mfumo wa Mao huyo Den Xiaoping angepata wapi utajiri?

Mabadiliko aliyoyaweza kuyafanya ni kutokana na kupata nafasi ya kusoma kwa matajiri ndo akapata akili za kitajiri na kuifanya China kufanya mabadiliko na kuwa matajiri
Hivi unafahamu hata sababu ya Deng Xiaoping kuvutiwa na CPC tokea huko Ufaransa alipokuwepo na kuja kujiunga nao 1922 akiwa na miaka 18 tu, Kwa nini ajiunge nao CPC [ Chama cha kikomunisti cha China cha watu wa hali ya chini ] na sio Kuomitang [ cha cha kibepari cha matajiri]?
 
Msomi asiye na kitu ni hatari sana kwenye siasa za kijamaa,
Ndo anajifunza wizi na unafiki kwa level ya juu kabisa
Tunaandika KATIBA mpya Ili msomi asiye na kitu apewe uongozi kama ana sifa.

Mifumo imdhibiti asiibe, Aishi Kwa JASHO lake.

Ameeeen.
 
Mnyonge atakufikisha wapi wewe?

Ukianza kumuelezea namna ya kuboresha mazingira ya uwekezaji na biashara atakuona muhujumu uchumi tu maana anakuwa hajawai hata kufanya biashara au kuwekeza mtaji sehemu na kutengeneza faida

Kuna shida katika understanding yako. Hakunaga greed ya kuunufaisha umma. Kuna greed ya “kujinufaisha wewe na familia yako”!

Trump (Rais billionaire wa kwanza wa Marekani) ameunufaishaje umma wa Marekani, kwa mfano?
 
Trump organization imeajiri watu 22,450. Ajira hizo ni changamoto kwenye uchumi wa Marekani

Iliajiri kwasababu Trump (billionaire) alichaguliwa kuwa Rais wa Marekani?

Wamarekani hawatajirikii madarakani tofauti na wa kwetu. Miye nilikujibu tuu swali lako Trump amenufaishaje umma wa Marekani. Alipokuwa Rais aliweka sera za kuinua uchumi vizuri sana ambao umma ulinufaika nao.
 
Walionufaika na urais wa Trump ni yeye mwenyewe na washirika wake, through self-dealings and trickle-down economic policies. Hata juhudi zake za kutaka kupindua matokeo ya 2020 presidential election ili aendelee kubaki zilikuwa zinasukumwa na maslahi binafsi hayo hayo.
 
Halafu inaonekana mleta mada hujui architecture ya siasa za Kenya. Siasa za Kenya ni za makundi sio za vyama vya siasa. Hakuna chama cha siasa cha kusema kimempitisha mgombea, ni mgombea na marafiki zake wanaanzisha chama, anajiita party leader then anakuwa mgombea moja kwa moja.
Party leader, umenikumbusha EICITIII Wazalendo cha jamaa
 
Back
Top Bottom