Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kwani hizo english medium nyingi zina kuwa kuanzia chekechea na primary school, asilimia kubwa wakienda sekondari huwa wanarudi hizi shule za serikali.Hizo shule za English Medium wanampa mtoto maarifa gani ya kumsaidia huko duniani akija kuanza kuishi?
Naona kama unazidi kupoteq njia...🤣Ur still a learner mkuu.
Nani alie kudanganya kwambia kulipa mamilioni English Mediums ndio kuwajibika kwa watoto wako? Nani huyo tumtafute tukamchape?
Elewa neno " kumchapa"
Ebu jaribu kuangaza macho tena uone kama kuna sehem nimeandika kwamba wanangu wapo English mediums....🤨Hizo shule za English Medium wanampa mtoto maarifa gani ya kumsaidia huko duniani akija kuanza kuishi?
Elimu bora ni nini?Naona kama unazidi kupoteq njia...🤣
I'm talking about millions, hapa nimesema ubora wa elimu, kuwajibika kwa ubaba wangu pamoja na maarifa wanayo yapata kutoka kule ninapo wapeleka kusoma.
Ikiwa utaanza kuthaminisha pesa, trust me.... hapo lazima utapotea njia kwasabau mimi nikisema sinapesa zaidi ya elfu tano mfukoni, kunamwingine atasema hana pesa kabisa kwasabau akiba yake imebaki 10 millions bank...😊
Mwisho nisema kwamba badi ni wajibu wa mzazi/baba kumuandaa mwanae ajekua nani huko baadae.
Hahahahahmalengo yangu watoto niwapeleke popote ili wajue kwanza kusoma na kuandika na kuongea vizuri na kuhesabu. Kiswahili na kiingerezs katika grobal standards.
Wakifanikiwa hapo mengine waniachie mimi ntajua pa kiwapeleka.
Faida ya english medium inampa mtoto marafiki wa maana, sio kama za kayumba!
Ni kwamba hawa watu wa mtaani kwetu wananiiga au na wao uchumi umewapiga kama Mimi.
Ni hivi niliwahi kuandika Uzi hapa nikisema nimeamua kuwatoa watoto wangu English Medium na kuwaleta Kayumba baada ya uchumi wangu kuzorota. Then nikaja nikaanzisha Uzi kuhusu FAIDA binafsi nilizo zipata baada ya kuwahimishia watoto wangu Kayumba.
Leo nimeenda shuleni kulikuwa na kikao cha wazazi. I was surprised KUKUTANA na watu zaidi ya kumi ambao na wao watoto wao walikuwa wanasoma English Medium na sasa wamewahamishia Kayumba.. Nilishindwa kupata jibu je ni kwamba hawa jamaa wana niiga Mimi au na wao uchumi umewapiga kama Mimi?
Kati yao kumi ni mmoja ndio Nina uhakika kwa asilimia mia kwamba amewahamishia watoto wake Kayumba kwa sababu ya kunigeza Mimi au at least kuwa inspired na Mimi.
Niliambiwa na mtu kwamba huyu jamaa aliwahi kusikika bar akiwaambia watu anawarudisha watoto wake Kayumba kwa sababu uchumi umekuwa mgumu. Akasema " Kama ( jina langu) nimewarudisha watoto wangu Kayumba yeye ni nani asiwarudishe?
Ni hivi hapo mtaani kwetu ( uswahilini) Mimi ninachukuliwa kama kijana mwenye uwezo kifedha.
Ila ukweli ninaujua Mimi mwenyewe ninapitia kipindi kigumu kiuchumi.. Ndio maana niliamua kuwarudisha watoto wangu shule ya Kayumba.
Mimi kuwarudisha watoto wangu Kayumba ilikuwa ni habari iliyo enea mtaa mzima..
Najua baadhi ya watu watakuwa wamefurahi kwa sababu kwao hilo linamaanisha anguko langu..
Hata hivyo leo nimekuja kugundua kwamba, Kumbe ni watu wengi tu hapo mtaani ambao walikuwa wanasomesha watoto wao English Medium walikuwa wanaumia kimya kimya ila walikuwa hawajui cha kufanya kwa sababu walikuwa wana ogopa macho na maneno ya watu ndio maana wengi wao walikuwa wanaishi kwa stress ilimradi ionekane watoto wao wanasoma English Mediums.
Nilipo watoa watoto wangu English Medium.na kuwaleta Kayumba, wazazi wengi wamefuata njia, now wanawatoa watoto wao English Mediums na kuwaleta Kayumba..
Nilicho kigundua kuhusu watanzania wengi ni kwamba wengi wanafanya mambo kwa ajili ya kujionyesha kwa watu. Kwa ajili ya approval and validation from other people.
Kwako ewe Mtanzania. Fanya kitu ambacho kipo ndani ya uwezo wako. Ishi maisha yako halisi usiishi kuwa impress watu.
Kingereza chenyewe ni Cha Kuunga unga Bora Katumba.Hapana hajacopy wala kupaste Uzi wangu ila maudhui yake yanafanana na maudhui ya Uzi nilio wahi kuutoa. Mimi nipo against na shule za English Medium za waswahili na ambazo hazipo chini ya taasisi. To me ili niweze kuiita English Medium, at least ada yake iwe milioni kumi kwa mwaka. Chini ya hapo najua ni ubabaishaji tu. Hiyo milioni 1 na nusu au mbili au 3 au 4 kwa mwaka bora nikalewe bar kuliko kumpeleke Mr. MUGETTA akalewe...
English Mediums za m.1 point tano , 2,3ms kwa mwaka ni Kayumba ambazo zinafundisha kwa KIINGEREZA period
Duh we hatari kweli mkuu umebadilisha tena gia anganiEbu jaribu kuangaza macho tena uone kama kuna sehem nimeandika kwamba wanangu wapo English mediums....🤨
Nakini pia, wanaume ama wababa hatujawahi kukosa kisinguzio mara tu tunapo ishiwa noti..😊
NakaziaKila mtu afanye analoona linafaa, lakini hata umsomeshe shule ya milioni 10 kwa mwaka kama mtoto huyo yupo hapa Tanzania wewe mzazi huna unalolifanya unajigeuzageuza tu ili uliwe vizuri... akimaliza hizo shule za milioni 10 kama hana hata mtaji wa kuanzisha kampuni yake wewe mzazi utakuwa na fahari ipi mbele yake unapomwona mwanao anazunguka na vibahasha na kugombania interviews za kihayawani?...
Kuna mahali nimewakataza watu kuwapeleka watoto wao English Mediums?Deal na Maisha yako, achana na ya watu, ukiweza mpeleka mtoto shule ya English kwa primary ni muhimu maana anapata msingi wa lugha kuendelea huko mbele hata akienda za kawaida.
Ila kama hauna uwezo Mungu anasaidia....
Kamwe usimsomeshe mtoto kinyonge sababu unataka kujenga, msomeshe kinyonge sababu huna hela.
Kujenga utajenga tu, ila umri na elimu ya mtoto havingoji......
Achana na maisha ya watu....
Hakuna mtu anaweza igiza umaskini.
Kabisa mkuuKingereza chenyewe ni Cha Kuunga unga Bora Katumba.
Kama una pesa peleka Nchi jirani au top schools za bei kubwa hapo utakuta walimu Wageni kutoka Nchi ambazo watu wanajua lugha.
Kuna mahali nimewakataza watu kuwapeleka watoto wao English Mediums?
Kabisa mkuu halafu sijui kwanini watu huwaga hawalioni hilo? Tatizo letu watanzania huwaga hatuna mipango ya muda mrefu..Kila mtu afanye analoona linafaa, lakini hata umsomeshe shule ya milioni 10 kwa mwaka kama mtoto huyo yupo hapa Tanzania wewe mzazi huna unalolifanya unajigeuzageuza tu ili uliwe vizuri... akimaliza hizo shule za milioni 10 kama hana hata mtaji wa kuanzisha kampuni yake wewe mzazi utakuwa na fahari ipi mbele yake unapomwona mwanao anazunguka na vibahasha na kugombania interviews za kihayawani?...
Nimewataja kwa sababu story yangu inawahitajiKuna mahali umeongelea maisha ya jirani zako wakati hayakuhusu.