Nilichokigundua kuhusu watanzania, mara baada ya kuwatoa watoto wangu English Medium na kuwaleta Kayumba

Nilichokigundua kuhusu watanzania, mara baada ya kuwatoa watoto wangu English Medium na kuwaleta Kayumba

Nikumpeleka mwanao shule ambayo atakua anaenda na kidumu cha maji, ufagio, jembe, fyekeo na mgongoni akiwa amebeba begi la madaftari..😊
Wakati huo baba ukiwa unaendesha BMW x 1, unakula suit daily, unapumua kwenye ofisi yenye fully kiyoyozi na baada ya kutoka job unapitia Pizzeria unakata 1 plate ya 21 thousands kisha unashushia na ballantain ya 60 thousands...😊

Kayumba za siku hizi hawabebi vidumu zina visima vya maji safi.

Kwa mijini kama Dar Shule za serikali zinatazamwa sana nowdays
 
Kayumba za siku hizi hawabebi vidumu zina visima vya maji safi.

Kwa mijini kama Dar Shule za serikali zinatazamwa sana nowdays
Sawa mkuu, kwakua watanzania wote wanaishi daslam nisawa...😊
 
Rudisha mtoto english medium, acha ukoloni. Kapambane, ukiwapeleka huko wapeleke, usione wenzako tunawapeleka ukajua ni hela, kuna elimu nzuri huko, na maandalizi mema, tafuta shule nzuri peleka mtoto. Huko kayumba wapeleke ila usijitetee mbele ya kadamnasi sijui tunawapeleka for kujitapa tu. Madogo wanakula skuli zuri huko.
 
[emoji3][emoji3] kwamba hata laki 2 hana
Amini nakuambia mkuu,jamii forum ilikuwa wakati ule sio hii ya leo ambayo imekosa mvuto kwa thread za kutunga na za kipuuzi kiasi kwamba hata ukiangalia michango yao utagundua kwasasa taifa limekumbwa na vijana wa ovyo
 
Kila mtu afanye analoona linafaa, lakini hata umsomeshe shule ya milioni 10 kwa mwaka kama mtoto huyo yupo hapa Tanzania wewe mzazi huna unalolifanya unajigeuzageuza tu ili uliwe vizuri... akimaliza hizo shule za milioni 10 kama hana hata mtaji wa kuanzisha kampuni yake wewe mzazi utakuwa na fahari ipi mbele yake unapomwona mwanao anazunguka na vibahasha na kugombania interviews za kihayawani?...
Inafikirishaa ilaa hata Ukimpa hizo mil 10 wakati huo hazitamfikisha popotee cha zaidi muwekeee akibaaa bank akisoma akifika mbali na hana pa kuanzia bhasi unaweza msupport japo ni ngumu mtu kuweza kumsomesha mwanae shule za Mil 10 alafu kesho mtoto akawa hana pakushika kabisa means mzee awe kafilisika hata vile visenti alivyomuwekea kwenye Acc havitakuwepo tena..
 
Ni kwamba hawa watu wa mtaani kwetu wananiiga au na wao uchumi umewapiga kama Mimi.

Ni hivi niliwahi kuandika Uzi hapa nikisema nimeamua kuwatoa watoto wangu English Medium na kuwaleta Kayumba baada ya uchumi wangu kuzorota. Then nikaja nikaanzisha Uzi kuhusu FAIDA binafsi nilizo zipata baada ya kuwahimishia watoto wangu Kayumba.

Leo nimeenda shuleni kulikuwa na kikao cha wazazi. I was surprised KUKUTANA na watu zaidi ya kumi ambao na wao watoto wao walikuwa wanasoma English Medium na sasa wamewahamishia Kayumba.. Nilishindwa kupata jibu je ni kwamba hawa jamaa wana niiga Mimi au na wao uchumi umewapiga kama Mimi?

Kati yao kumi ni mmoja ndio Nina uhakika kwa asilimia mia kwamba amewahamishia watoto wake Kayumba kwa sababu ya kunigeza Mimi au at least kuwa inspired na Mimi.

Niliambiwa na mtu kwamba huyu jamaa aliwahi kusikika bar akiwaambia watu anawarudisha watoto wake Kayumba kwa sababu uchumi umekuwa mgumu. Akasema " Kama ( jina langu) nimewarudisha watoto wangu Kayumba yeye ni nani asiwarudishe?

Ni hivi hapo mtaani kwetu ( uswahilini) Mimi ninachukuliwa kama kijana mwenye uwezo kifedha.

Ila ukweli ninaujua Mimi mwenyewe ninapitia kipindi kigumu kiuchumi.. Ndio maana niliamua kuwarudisha watoto wangu shule ya Kayumba.

Mimi kuwarudisha watoto wangu Kayumba ilikuwa ni habari iliyo enea mtaa mzima..

Najua baadhi ya watu watakuwa wamefurahi kwa sababu kwao hilo linamaanisha anguko langu..

Hata hivyo leo nimekuja kugundua kwamba, Kumbe ni watu wengi tu hapo mtaani ambao walikuwa wanasomesha watoto wao English Medium walikuwa wanaumia kimya kimya ila walikuwa hawajui cha kufanya kwa sababu walikuwa wana ogopa macho na maneno ya watu ndio maana wengi wao walikuwa wanaishi kwa stress ilimradi ionekane watoto wao wanasoma English Mediums.

Nilipo watoa watoto wangu English Medium.na kuwaleta Kayumba, wazazi wengi wamefuata njia, now wanawatoa watoto wao English Mediums na kuwaleta Kayumba..

Nilicho kigundua kuhusu watanzania wengi ni kwamba wengi wanafanya mambo kwa ajili ya kujionyesha kwa watu. Kwa ajili ya approval and validation from other people.

Kwako ewe Mtanzania. Fanya kitu ambacho kipo ndani ya uwezo wako. Ishi maisha yako halisi usiishi kuwa impress watu.
They are being more driven by emotions rather than mind.
 
Rudisha mtoto english medium, acha ukoloni. Kapambane, ukiwapeleka huko wapeleke, usione wenzako tunawapeleka ukajua ni hela, kuna elimu nzuri huko, na maandalizi mema, tafuta shule nzuri peleka mtoto. Huko kayumba wapeleke ila usijitetee mbele ya kadamnasi sijui tunawapeleka for kujitapa tu. Madogo wanakula skuli zuri huko.
Elimu bora ni nini?
 
Nikumpeleka mwanao shule ambayo atakua anaenda na kidumu cha maji, ufagio, jembe, fyekeo na mgongoni akiwa amebeba begi la madaftari..😊
Wakati huo baba ukiwa unaendesha BMW x 1, unakula suit daily, unapumua kwenye ofisi yenye fully kiyoyozi na baada ya kutoka job unapitia Pizzeria unakata 1 plate ya 21 thousands kisha unashushia na ballantain ya 60 thousands...😊
Safi sana mkuu, umegundua huna jibu umeona upotezee kimasihara.


Rudisha "watoto wako " Kayumba.

Anyways nimeandika " watoto wako " kwa sababu najua hata wewe hauna uhakika.kama.ni watoto wako.

Sasa nasema " Rudisha watoto wa mke wako wako Kayumba"
Utakuja kunishukuru sana.
 
NI kweli mkuu.Kayumba kuanzia darasa la tano utawakuta wanawapokea wahamiaji kutoka English schools.
Na wazazi wengi wakijitahidi Hadi std 7 ujue sekondari NI kayumba.
Tena wanatoa shukrani kwa watoto kuchaguliwa kayumba.wanasema kuwa Bora wapumue.na wamekoma kusomesha English medium
Mi mwenyewe nimekoma. 🤣🤣🤣
 
Ukifanya mambo yako kisa jamii inakuangliaje, unakua bado hujakua kifikra. Bado una utoto kichwani, wanasema matumizi yasizidi mapato.
 
Yupo jirani yng mmoja ana maisha magumu Sana,,
Ila mtu wa mashauzi sn,,

Jamaa anai mwanae yupo english medium.
Kuna kipindi ada inasumbuwa na mtoto anafukuzwa shule,,
Basi jamaa anaamuwa kumfungia mtoto hata mwezi mzima asitoke ndani asubuhi,, during school hours.0600 - 1500hrs jioni anamfungulia mlango akacheze nje...
Mradi mtoto aonekane amekwenda shule.


Shida yote ya nn?
 
Back
Top Bottom