Nilichokikuta ukweni imebidi nimsamehe mume wangu

Ndugu nilishakaa nae nikamwambia kila mwisho wa mwezi anipe laki 2 tu nami niongeze za kwangu angalau kila mwezi tunafanya kitu,,, akakubalu ila nimiez 5 tangu tukubaliane hivyo hajafanya kitu kama icho
Jaribu kukaa nae umshauri tena akikataa achana nae utakuwa hujapata mume mwenye akili atakuwa bwege tu huyo AU

Tafuta watu wanaoheshimiana nae sana mfano rafiki zake au mzee mwenye busara umueleze na mkae pamoja awashauri
 
mwambie apunguze hela ya kuwatumia kwa miezi minne alafu uchanganye na yakwako ili mpate mtaji wa biashara mtakayoweka kuifanya, alafu kipato cha hiyo biashara ni kwaajili ya maendeleo yenu tu. sometimes inabidi uwe kauzu zaidi ya dagaa.
 
Mtengenezee mazingira ya kuacha kupeleka hela kwao si kumwambia akupe hela wewe!!! Ukifanya hivyo maanake atatuma tu na utakuwa hujatatua tatizo mwambie awaambie kuwa saizi hata kazi katumbuliwa
 
Kwa haraka haraka huyo jamaa yako ni mpumbafu kiwango cha lami
 
AKIFA NANI ATANUNULIA NGUO HAO NDUGU?

HEBU AFE KIROHO KWAO KWANZA.

KWA MAPATO YENU MIEZI SITA ARUSHA MNAJENGA NA MIEZI SITA MINGINE GARI

KISHA MUWAPE MTAJI WAFANYE KAZI.
 
Ushauri wangu mm ni kama ifuatavyo..
1. Wewe kama mkewe au mke mtarajiwe vyovyote vile yafaa umtie moyo, ushauri na pia unyesha furaha kwake kwa kadiri ya uwezo wako hali hii itampa ujasiri na kuamini bado yuko katika njia sahihi..
2. Mshauri amchague mmoja wa hao ndugu zake amuwezeshe mtaji au kama anaconnection amchomekee kazi sehemu yoyote ile.. hii itampunguzia mzigo wa kusaidia nyumbani akiwa peke yake.. ukoo wao sasa utakuwa na watu wawili muhimu na hivyo yeye kujikuta akipunguza gharama za kuwahudumia kwa angalau nusu yake..
3. Aangalie mahitaji muhimu zaidi ya huko kijijini mara nyingi ni maji hivyo kama anaweza achimbe kisima ili kuwarahisishia uhitaji huo kama ujuavyo water is the povert trap..
4. Mumeo ajifunze kitu kimoja muhimu.. Kutoa sana kwa ndugu ndio umasikini wake..
Kwa ufupi tu lkn...
 
Hameni mtaa mbali kama ni karibu na home au kama ni mbali lakin ndugu wanapajua hamien mtaa mwingine badilishen Namba za Simu kwishaa
 
si vizuri kuhukumu kwa makabila lakini kwa hili kama uko vizuri unaweza kutuambia anatoka mkoa gani tu halafu mengine tutajaza wenyewe katika kukushauri na kujishauri wenyewe kwa kuwa ushauri utakaotolewa utatufaa sote kukabiri changamoto za familia.
 
Nianze na msemo wa kiswahili unaosema kuwa "Ni kosa la kiufundi kuwa na huruma ya mshumaa ktk maisha". Mshumaa unatusaidia kutoa mwanga lakini wenyewe unateketea.

Kifupi ni kwamba anatakiwa kuwa na malengo ya msingi kuhusu ustawi wa familia yenu (Mke, Mme na Watoto) kwanza ("familia kwanza") kisha ndugu badae.

Na kwamba, kusaidia ni jambo jema sana ila kusizidi uwezo ulionao/kipato chako. Ili umdu kusaidia kwa kiwango cha kawaida lazima ufahamu aina na kariba za misaada unayotoa ni kwa ajili ya nini/kutatua changamoto gani/ipi na kwa nani??.

Si kila msaada ukiombwa usaidie unazama mfokoni kusaidia kisa una mshahara. Mfano kutoa msaada wa kununua nguo kwa ndugu, yaani kila ndugu unataka avae vizuri wakati ote. Kwa lugha nyingine wewe ndiyo mwenye jukumu hilo. Wakati huyo unayemsaidia kumnunulia nguo kila wakati ana nguvu na akili timamu. Misaada ktk shida/changamoto za namna hiyo hupwasi kuiendekeza hata kidogo.

Zipo shida/changamoto za kusaidia mfano kusomesha, matibabu, kunua chakula wakati wa njaa hasa kama Wazazi/Walezi wako hawana uwezo wa kuzalisha tena. Vinginevyo waweza kuwa unawasaidia pale inapobidi au unatoa kama zawadi kwao.

Na kwamba unapotoa msaada wa kusomesha ndugu kwa mfano, maana yake unatengeneza mazingira ya kupunguza utoaji wa misaada isiyokuwa na tija hasa wakati ujao maana unamfanya mlengwa aweze kujitegema mwenyewe kwa 100%.

Lakini pia, ili kumudu utoaji wa misaada kwa kiwango kama anachotoa Mme wako na kufanya maendeleo, lazima uwe na vyanzo vya uchumi zaidi ya kimoja. Vingenevyo maendelea kwenu itakuwa mwiko kwakweli.

Nimalizie kwa misemo ya kiswahili chetu kizuri:-

1. Wema usizidi uwezo.
2. Tenda wema nenda zako.
3. Kutoa ni moyo usambe si utajiri.
4. Huwezi kwenda kuzima moto kwa jirani wakati kwako kunaungua.

"Life+time"....
 
Kwer Mkuu hiyo laki 3,ni mtaji safi sana kila siku anabet timu 3..mpaka mwisho wa mwezi ni milionea..
NB:Onyo beting ni hatari kwa kipato chako.
Sasa anayebeti na huja mume wanatofauti gani??
 
Achane naye mtafute mwingine uanze naye maisha.
 
Ni vile hujui wengi wa zaman wamesoma kwa michango ya ndugu na jamaa unaweza kuta dadazake walipigana kufa na kupona asome leo useme asiwahudumie kweli mkuu.
 
Huyo mwanaume hajui kwamba maisha yake na familia yake yanamhusu yeye?
 
Akituliza akili Mtapata maendeleo,Kama ana stable income achugua mkopo hata wa mil 16 kisha afungue biashara inayoeleweka ambayo kashaifanyia tafiti za kutosha,akupe usimamie wewe!
 
Kuhudumia ndugu zako Ni msaada wa kifamilia.
Ila kuhudumia kwa kuwanunulia nguo za kuvaa Ni ujinga.
Hasa wadada ambao kila fasheni wanataka wapite nayo.
Angekuwa anasomesha watoto wa hao ndugu zake ningemuelewa.
Tena usikute Wana waume zao.
Dada umeolewa na mvulana.
Mwanaume hawezi kubali kufanya Mambo ya hivyo.
Mtu pekee ninayemuhudumia kwa mavazi na chakula Ni mzazi.
Wengine Ni optional.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…