Jamaa_Mbishi
JF-Expert Member
- Jun 15, 2013
- 9,626
- 6,731
Amani ya Mungu iwe nanyi wapendwa, naomba ushauri.
Ni mume niliempenda nilemuheshimu na kumfanyia kila kitu anachostahili mwanaume kufanyiwa kumfariji wakati wa magumu na kuwa nae wakati wa furaha, naye mwenyewe aliyakubali yote niliyokua nafanya.
Sasa juzi kachelewa kurudi nyumbani na sikumuuliza sababu akasema anaomba ale chakula ndipo aoge, nikapakua tukala kisha nikamuandaa akaoge ndipo nilipokuta kwenye nguo za ndani uchafu wa kutoka kujamiana na mwanamke.Nilipomuuliza akajibu fikiria utakachoamua kufikiri.
Naomben ushauri kwani hapa nasikia mwili wote unauma, kichwa kinataka kupasuka.
Usikurupuke kuhisi amechapa nje ya ndoa, kumbuka kuna wanaume wengine ni dhaifu, akiona mwanamke au hata kuku wanajamiana anachanganikiwa na kuwaza vya hajabu kisha kulowesha chupi. Wengi wanashindwa kusema ukweli baada ya kushitukiwa na wake zao matokeo yake wanakuja na maneno ya kejeli kama hayo aliyosema mumeo kwako. Ila pole lakini..