Nilichoshuhudia ni aibu, viongozi BAVICHA ni weupe kichwani, CHADEMA mna kazi sana ya kuwafundisha kujenga hoja na kufanya utafiti

Mkuu sitaki kupinga yote uliyosema, je hao unaotaka waulizwe maswali magumu wana uwezo wa kuyajibu? Maana umesema Abdul Nondo wangalau aliulizwa swali la msingi, je alijibiwa?
Alijibiwa majibu hayakuwa ya kuridhisha lakini aliweza ku expose weakness, na ni jambo muhimu hili, ku expose weakness ambayo serikali haiwezi kujitetea kunapandisha credit ya chama na kuipunguzia serikali

Sio kila anayewakosoa ni adui wakuu..dah
 
Hili mi limenifanya niwaone hawana maana. Wao hoja yoyote ambayo inaenda tofauti wao, wanaishambulia kwa matusi
 
Alijibiwa majibu hayakuwa ya kuridhisha lakini aliweza ku expose weakness, na ni jambo muhimu hili, ku expose weakness ambayo serikali haiwezi kujitetea kunapandisha credit ya chama na kuipunguzia serikali

Sio kila anayewakosoa ni adui wakuu..dah

Mkuu mbona hujiamini, sijapinga ukosoaji wako, numekusaidia tu kuweka vizuri huo ukosoaji wako.
 
Niweke wazi kwanza sina chama nimekuwa nikipiga spana pande zote, na unaweza kucheki profile yangu kuthibitisha hilo.

So napenda hoja yangu isijadiliwe kishabiki bali objectively

Ni kuhusu vijana wa Chadema, hawa wapo wengi sana mtandaoni kuliko vijana wa vyama vingine, ACT, CUF, CCM n.k hapa Chadema niwapongeze kwa kuwa na base kubwa mtandaoni

Lakini tatizo kubwa la hawa vijana ni kuwa hawawezi kujenga hoja zaidi ya mashambulizi ya dhihaka na matusi, hoja zipo kidogo sana.

Nitatoa mifano michache, juzi kulikuwa na taarifa kuwa umeme umepandishwa bei, waliokuwa wakisambaza habari hizi ni vijana wa Chadema akina Martin, Mdude, Pambalu n.k kucheki kwenye simu yangu nikaona haujapanda bei, lakini sikuridhika maana umeme unauzwa kwa bei tofauti kwa miji tofauti nikasema labda utakuwa umepanda mikoa mingine maana jamaa walikuwa wakilaani kwa nguvu na kujiamini sana.

Sasa Bungeni likaulizwa hilo swali na Makamba akajibu umeme haujapanda na hauwezi kupandishwa kimyakimya na waliotangaza wachukuliwe hatua.

Kule Twitter nikaona pia Nape kaandika kuwa waliosambaza hizo taarifa wachukuliwe hatua.

Sasa nilitegemea vijana wa Chadema ambao ndio walikuwa mstari wa mbele kusambaza taarifa zile wangetoa maelezo kuwa Serikali imedanganya na kuleta ushahidi.

Mfano waambatanishe na msg zs LUKU kuwa umeme wilaya fulani ulikuwa ukinunua wa 10k unapata unit 40 lakini sasa ukinunua unapata unit 20 na screen shot za msg ili kumuumbua Makamba, au labda kama ulipandishwa kisha baada ya kelele za watu ukashushwa basi pia watoe hayo maelezo pamoja na evidence.

Lakini hawakufanya chochote kama hicho, badala yake wakawa wanamshambulia Makamba na Nape kuwa wasiwatishe wao hawatishiki, mara walipiga magoti kwa Magufuli na blah blah kibao.

Sasa najiuliza hiki ni chama kinachotegemea watu wenye akili watakaa wawasikilize na kuwachukulia serious kweli? Maana wanafanya vitu kihuni sana.

Tundu Lissu pamoja na yeye kuwa na lugha za dhihaka, lakini anajenga hoja vizuri na kuweka na facts mara nyingi, sasa hawa vijana kwa nini asiwafundishe?

Jana pia kulikuwa na mjadala Clubhouse ambapo msemaji wa Serikali Gerson Msigwa alikuwa akiulizwa maswali, aliulizwa maswali na watu wengi sasa kuna vijana wa Chadema kuna Mwaipaya, Pambalu na yule Rose Mayemba nao wakapewa nafasi waulize, nilitegemea kwa kuwa wao ni viongozi kwenye siasa wangembana Msigwa kwa maswali magumu na yaliyofanywa utafiti, ila dah ilikuwa ni aibu, jamaa kwanza hawajui hata kujenga hoja ya swali, kwenda wanazunguuka hadi kero, na maswali yenyewe ni famba tupu, mfano yule Pambalu aliuliza "Msigwa tujibu ndio au hapana, Samia yupo nyuma ya kinachoendelea Loliondo?"

Mwaipaya nae hivyo hivyo, kulikuwa na yule dogo wa ACT anaitwa Abdul Nondo kidogo huyu alikuwa na swali la maana, maana alimuuliza Msigwa kuhusu serikali kukiuka amri ya mahakama kuhusu mgogoro wa Loliondo, kuna kesi iliyofunguliwa na watu wa loliondo ambapo serikali iliamriwa isifanye chochote mpaka kesi itolewe hukumu. Msigwa hakuweza kujibu hili.

Halafu kingine ni hawa vijana ambao ndio viongozi wa vijana wengine kukosa busara kama watoto, unakuta hawajaridhika labda na jibu badala ya kuonyesha maturity wanaanza kuropoka hovyo bila mpangilio. Dah!
Basi CCM kuna upungufu mkubwa sana wa vijana wanaojielewa na kama taifa tuna tatizo kubwa sana la vijana wajenga hoja maana wapo vijana kama watano kwenye unaibu waziri toka CDM na kuna DC,RC,DAS,RAS wengi ambao walipotoka CDM tuu,wakapewa nafasi hizo.
Mihemko ya kimtandao ni tofauti na ya kitendaji.
Kuna mtu kama K. Kihongosi ambaye kwa mihemko yake aliyokuwa nayo, mtu mwenye akili timamu kama zangu siwezi kufikiri hata siku moja kama anaweza kuwa hata VEO,lakini eti leo ndiye boss wa UVCCM.
Kuna vyama havina progamu ya kuwatengeneza vijana kuwa viongozi bora wa kesho (hasa CCM hawana hili) zaidi ya kutengeneza vijana wa kukilinda chama, maslahi ya chama na maslahi ya wachache.
All in all, hakuna mpango wa kitaifa wa kutengeneza viongozi wa kesho.
 
Tamko la chama gani
Wewe unazungumzia vijana wa chama gani?
Hivi ni kweli wanaoumizwa na upandaji holela wa gharama za maisha ni CDM pekee?
Wafuasi wa vyama vingine na wasio na vyama wao hawaguswi na kuumizwa!!?
Kama wanaguswa,wao hawapaswi kulalamikia hali hiyo!!??
 
No, hilo nimelisema kwa kuwa Chadema wengi mna sifa ya kutukana watu wenye mawazo tofauti na nyie

Utukanwe na nani boss, au unataka kujichukulia umaarufu kuwa huwa unatukanwa? Au nyie ni wale bendera fuata upepo, ukisikia watu wanasema kitu na ww unapitia humohumo ili uende na fashion? Nijuavyo mimk ukija na hoja ya msingi inajibiwa vizuri na ushahidi wa hilo upo, ukija na hoja ya kuzingua unazunguliwa, maana huku mitandaoni sio vikao vya kanisa. Simple as that.
 
Katiba mpya ni ya muhimu sana sana kwa WATANZANIA sio kwa Chadema,ACT au CCM.

Amini nawaambia wanasiasa ni wale wale wanatoka kwenye jamii yetu. Tusitarajie tafauti kubwa kati ya walioko sasa madarakani na walio upinzani. ACT au Chadema wakiingia bila katiba imara, vilio ni vilevile.

Wapo watu walikua upinzani wamerudi ccm na madaraka wakapewa. kafulilaa , katambii, mtatiruu, silindee, waitaraa, je mnaona tofauti yeyote?

Wengine akademia wakala shavu serikalini bashiroho, mwakymbe (digirii 4), Kaboody, slowslow, Spika Tulea . Je mmeona tafauti

Katiba ya wananchi walau itasaidia kupunguza madaraka ya walamba asali/wanasiasa na kuhimiza uwajibikaji
 
Niweke wazi kwanza sina chama nimekuwa nikipiga spana pande zote, na unaweza kucheki profile yangu kuthibitisha hilo.

So napenda hoja yangu isijadiliwe kishabiki bali objectively

Ni kuhusu vijana wa Chadema, hawa wapo wengi sana mtandaoni kuliko vijana wa vyama vingine, ACT, CUF, CCM n.k hapa Chadema niwapongeze kwa kuwa na base kubwa mtandaoni

Lakini tatizo kubwa la hawa vijana ni kuwa hawawezi kujenga hoja zaidi ya mashambulizi ya dhihaka na matusi, hoja zipo kidogo sana.

Nitatoa mifano michache, juzi kulikuwa na taarifa kuwa umeme umepandishwa bei, waliokuwa wakisambaza habari hizi ni vijana wa Chadema akina Martin, Mdude, Pambalu n.k kucheki kwenye simu yangu nikaona haujapanda bei, lakini sikuridhika maana umeme unauzwa kwa bei tofauti kwa miji tofauti nikasema labda utakuwa umepanda mikoa mingine maana jamaa walikuwa wakilaani kwa nguvu na kujiamini sana.

Sasa Bungeni likaulizwa hilo swali na Makamba akajibu umeme haujapanda na hauwezi kupandishwa kimyakimya na waliotangaza wachukuliwe hatua.

Kule Twitter nikaona pia Nape kaandika kuwa waliosambaza hizo taarifa wachukuliwe hatua.

Sasa nilitegemea vijana wa Chadema ambao ndio walikuwa mstari wa mbele kusambaza taarifa zile wangetoa maelezo kuwa Serikali imedanganya na kuleta ushahidi.

Mfano waambatanishe na msg zs LUKU kuwa umeme wilaya fulani ulikuwa ukinunua wa 10k unapata unit 40 lakini sasa ukinunua unapata unit 20 na screen shot za msg ili kumuumbua Makamba, au labda kama ulipandishwa kisha baada ya kelele za watu ukashushwa basi pia watoe hayo maelezo pamoja na evidence.

Lakini hawakufanya chochote kama hicho, badala yake wakawa wanamshambulia Makamba na Nape kuwa wasiwatishe wao hawatishiki, mara walipiga magoti kwa Magufuli na blah blah kibao.

Sasa najiuliza hiki ni chama kinachotegemea watu wenye akili watakaa wawasikilize na kuwachukulia serious kweli? Maana wanafanya vitu kihuni sana.

Tundu Lissu pamoja na yeye kuwa na lugha za dhihaka, lakini anajenga hoja vizuri na kuweka na facts mara nyingi, sasa hawa vijana kwa nini asiwafundishe?

Jana pia kulikuwa na mjadala Clubhouse ambapo msemaji wa Serikali Gerson Msigwa alikuwa akiulizwa maswali, aliulizwa maswali na watu wengi sasa kuna vijana wa Chadema kuna Mwaipaya, Pambalu na yule Rose Mayemba nao wakapewa nafasi waulize, nilitegemea kwa kuwa wao ni viongozi kwenye siasa wangembana Msigwa kwa maswali magumu na yaliyofanywa utafiti, ila dah ilikuwa ni aibu, jamaa kwanza hawajui hata kujenga hoja ya swali, kwenda wanazunguuka hadi kero, na maswali yenyewe ni famba tupu, mfano yule Pambalu aliuliza "Msigwa tujibu ndio au hapana, Samia yupo nyuma ya kinachoendelea Loliondo?"

Mwaipaya nae hivyo hivyo, kulikuwa na yule dogo wa ACT anaitwa Abdul Nondo kidogo huyu alikuwa na swali la maana, maana alimuuliza Msigwa kuhusu serikali kukiuka amri ya mahakama kuhusu mgogoro wa Loliondo, kuna kesi iliyofunguliwa na watu wa loliondo ambapo serikali iliamriwa isifanye chochote mpaka kesi itolewe hukumu. Msigwa hakuweza kujibu hili.

Halafu kingine ni hawa vijana ambao ndio viongozi wa vijana wengine kukosa busara kama watoto, unakuta hawajaridhika labda na jibu badala ya kuonyesha maturity wanaanza kuropoka hovyo bila mpangilio. Dah!
Unataka watu wawe OBJECTIVE kwenye HOJA Yako?

Jibu ni Rahisi. Unga mkono juhudi na mapambano tupate KATIBA mpya.

Suala la weledi na ELIMU ni la kimfumo, vijana waongelewe Kwa ujumla wao bila kujali vyama nk.

Darasa la nane la zamani enzi za Nyerere mhitimu alikuwa karibu kuwa sawa na anaetoka university ya sasa, tumerudi nyuma.

Tukijadili Kwa muktadha wa vijana waliopo CCM, wao ni level ya chini kabisa sababu RUSHWA imetamalaki upatikanaji wao. Hadi wanateuliwa kutuongoza wakiwa VILAZA.

Tukiweka Ushabiki Pembeni CHADEMA Ina watu wengi cream walioachwa na mfumo mbovu wa RUSHWA.

Mf Mnyiiika mmoja unaweza chukua vijana vijana 100 pale Lumumba na wasimuweze Kwa hoja. Amen
 
Mkuu uko sahihi kabisa kuwa hata wazee wa CDM wote hamna kitu, na udhaifu wao umeuweka wazi. Tuje CCM kwenye wasomi. Wakati wa JK, CCM wote kuanzia wasomi hadi wasiosoma, wazee kwa vijana walisema umeme wa gas ndio habari ya mjini, na umeme wa maji tatizo ni mabadiliko ya tabia nchi. Na mapambio yote yakaimbwa, hadi wananchi wa Mtwara waliogoma gas kupisha mradi, yakawakuta yanayowakuta Wamasai wa ngorongoro leo.

Alipokuja Magufuli habari ya umeme wa gas ikawekwa kwapani, wimbo ikawa ni bwawa la JHNNP ndio mkombozi wetu, lile kundi lote la CCM hakuna aliyesema porojo ya mabadiliko ya tabia nchi wala nini! 6.5t ikawekezwa kwenye umeme wa maji wenye mabadiliko ya tabia nchi, wakaipotezea gas kwa kauli rahisi kuwa gas sio yetu imeuzwa! Mpaka leo hawajaweka wazi nani Kauza gas na kwanani.

Hebu tusaidie hapo kwenye hayo makundi mawili, ni kundi lipi ujinga wake uko wazi kuliko kundi jingine?
Hilo swali ndiyo yale unachukua pepa unaanza nalo na point zote zinapotea,umetisha
 
Wewe unazungumzia vijana wa chama gani?
Hivi ni kweli wanaoumizwa na upandaji holela wa gharama za maisha ni CDM pekee?
Wafuasi wa vyama vingine na wasio na vyama wao hawaguswi na kuumizwa!!?
Kama wanaguswa,wao hawapaswi kulalamikia hali hiyo!!??
Nimezungzia kitu specific hapo, umeme kupanda bei, ambacho kilisemwà na Bavicha wakashindwa kuthibitisha baada ya serikali kukanusha
 
Utukanwe na nani boss, au unataka kujichukulia umaarufu kuwa huwa unatukanwa? Au nyie ni wale bendera fuata upepo, ukisikia watu wanasema kitu na ww unapitia humohumo ili uende na fashion? Nijuavyo mimk ukija na hoja ya msingi inajibiwa vizuri na ushahidi wa hilo upo, ukija na hoja ya kuzingua unazunguliwa, maana huku mitandaoni sio vikao vya kanisa. Simple as that.
Nitafute umaarufu wakati situmii hata jina wala picha yangu? Matusi ni jadi ya vijana wengi wa Chadema nimelisema kwa kuwa hata kwenye hii thread wametukana badala ya kujibu hoja
 
Mkuu matusi ni kwa vijana wa vyama vyote, labda kama macho yako umeweka filter. Isitoshe nimekuambia humu mitandaoni sio kama kwenye vikao vya kanisa, hivyo dhihaka, matusi na kejeli ni sehemu ya changamoto za mitandaoni, huwezi kukwepa, labda ungesema hayo matusi umetukanwa na virified I'd ya CDM.
 
Back
Top Bottom