Nilichoshuhudia ni aibu, viongozi BAVICHA ni weupe kichwani, CHADEMA mna kazi sana ya kuwafundisha kujenga hoja na kufanya utafiti

Mkuu sitaki kupinga yote uliyosema, je hao unaotaka waulizwe maswali magumu wana uwezo wa kuyajibu? Maana umesema Abdul Nondo wangalau aliulizwa swali la msingi, je alijibiwa?
Alijibiwa majibu hayakuwa ya kuridhisha lakini aliweza ku expose weakness, na ni jambo muhimu hili, ku expose weakness ambayo serikali haiwezi kujitetea kunapandisha credit ya chama na kuipunguzia serikali

Sio kila anayewakosoa ni adui wakuu..dah
 
Hili mi limenifanya niwaone hawana maana. Wao hoja yoyote ambayo inaenda tofauti wao, wanaishambulia kwa matusi
 
Alijibiwa majibu hayakuwa ya kuridhisha lakini aliweza ku expose weakness, na ni jambo muhimu hili, ku expose weakness ambayo serikali haiwezi kujitetea kunapandisha credit ya chama na kuipunguzia serikali

Sio kila anayewakosoa ni adui wakuu..dah

Mkuu mbona hujiamini, sijapinga ukosoaji wako, numekusaidia tu kuweka vizuri huo ukosoaji wako.
 
Basi CCM kuna upungufu mkubwa sana wa vijana wanaojielewa na kama taifa tuna tatizo kubwa sana la vijana wajenga hoja maana wapo vijana kama watano kwenye unaibu waziri toka CDM na kuna DC,RC,DAS,RAS wengi ambao walipotoka CDM tuu,wakapewa nafasi hizo.
Mihemko ya kimtandao ni tofauti na ya kitendaji.
Kuna mtu kama K. Kihongosi ambaye kwa mihemko yake aliyokuwa nayo, mtu mwenye akili timamu kama zangu siwezi kufikiri hata siku moja kama anaweza kuwa hata VEO,lakini eti leo ndiye boss wa UVCCM.
Kuna vyama havina progamu ya kuwatengeneza vijana kuwa viongozi bora wa kesho (hasa CCM hawana hili) zaidi ya kutengeneza vijana wa kukilinda chama, maslahi ya chama na maslahi ya wachache.
All in all, hakuna mpango wa kitaifa wa kutengeneza viongozi wa kesho.
 
Tamko la chama gani
Wewe unazungumzia vijana wa chama gani?
Hivi ni kweli wanaoumizwa na upandaji holela wa gharama za maisha ni CDM pekee?
Wafuasi wa vyama vingine na wasio na vyama wao hawaguswi na kuumizwa!!?
Kama wanaguswa,wao hawapaswi kulalamikia hali hiyo!!??
 
No, hilo nimelisema kwa kuwa Chadema wengi mna sifa ya kutukana watu wenye mawazo tofauti na nyie

Utukanwe na nani boss, au unataka kujichukulia umaarufu kuwa huwa unatukanwa? Au nyie ni wale bendera fuata upepo, ukisikia watu wanasema kitu na ww unapitia humohumo ili uende na fashion? Nijuavyo mimk ukija na hoja ya msingi inajibiwa vizuri na ushahidi wa hilo upo, ukija na hoja ya kuzingua unazunguliwa, maana huku mitandaoni sio vikao vya kanisa. Simple as that.
 
Katiba mpya ni ya muhimu sana sana kwa WATANZANIA sio kwa Chadema,ACT au CCM.

Amini nawaambia wanasiasa ni wale wale wanatoka kwenye jamii yetu. Tusitarajie tafauti kubwa kati ya walioko sasa madarakani na walio upinzani. ACT au Chadema wakiingia bila katiba imara, vilio ni vilevile.

Wapo watu walikua upinzani wamerudi ccm na madaraka wakapewa. kafulilaa , katambii, mtatiruu, silindee, waitaraa, je mnaona tofauti yeyote?

Wengine akademia wakala shavu serikalini bashiroho, mwakymbe (digirii 4), Kaboody, slowslow, Spika Tulea . Je mmeona tafauti

Katiba ya wananchi walau itasaidia kupunguza madaraka ya walamba asali/wanasiasa na kuhimiza uwajibikaji
 
Unataka watu wawe OBJECTIVE kwenye HOJA Yako?

Jibu ni Rahisi. Unga mkono juhudi na mapambano tupate KATIBA mpya.

Suala la weledi na ELIMU ni la kimfumo, vijana waongelewe Kwa ujumla wao bila kujali vyama nk.

Darasa la nane la zamani enzi za Nyerere mhitimu alikuwa karibu kuwa sawa na anaetoka university ya sasa, tumerudi nyuma.

Tukijadili Kwa muktadha wa vijana waliopo CCM, wao ni level ya chini kabisa sababu RUSHWA imetamalaki upatikanaji wao. Hadi wanateuliwa kutuongoza wakiwa VILAZA.

Tukiweka Ushabiki Pembeni CHADEMA Ina watu wengi cream walioachwa na mfumo mbovu wa RUSHWA.

Mf Mnyiiika mmoja unaweza chukua vijana vijana 100 pale Lumumba na wasimuweze Kwa hoja. Amen
 
Hilo swali ndiyo yale unachukua pepa unaanza nalo na point zote zinapotea,umetisha
 
Wewe unazungumzia vijana wa chama gani?
Hivi ni kweli wanaoumizwa na upandaji holela wa gharama za maisha ni CDM pekee?
Wafuasi wa vyama vingine na wasio na vyama wao hawaguswi na kuumizwa!!?
Kama wanaguswa,wao hawapaswi kulalamikia hali hiyo!!??
Nimezungzia kitu specific hapo, umeme kupanda bei, ambacho kilisemwà na Bavicha wakashindwa kuthibitisha baada ya serikali kukanusha
 
Nitafute umaarufu wakati situmii hata jina wala picha yangu? Matusi ni jadi ya vijana wengi wa Chadema nimelisema kwa kuwa hata kwenye hii thread wametukana badala ya kujibu hoja
 
Nitafute umaarufu wakati situmii hata jina wala picha yangu? Matusi ni jadi ya vijana wengi wa Chadema nimelisema kwa kuwa hata kwenye hii thread wametukana badala ya kujibu hoja

Mkuu matusi ni kwa vijana wa vyama vyote, labda kama macho yako umeweka filter. Isitoshe nimekuambia humu mitandaoni sio kama kwenye vikao vya kanisa, hivyo dhihaka, matusi na kejeli ni sehemu ya changamoto za mitandaoni, huwezi kukwepa, labda ungesema hayo matusi umetukanwa na virified I'd ya CDM.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…