Bush Dokta
JF-Expert Member
- Apr 11, 2023
- 42,525
- 74,605
Kuna Bar Maids wazuri zana. Wanawaka balaaHapo nazan alitaka tu kuonesha umwamba wake hapo baa au Kuna barmaid anamtaman alihisi labda unakula

Mimi polisi mwaka huo huo kijana want alimaliza f4, akawa anaendesha pkpk yangu. Polisi jirani akaniambia kijana wako Hana leseni na Kuna msako anataka kunisaidia apate leseni haraka nimpe 250kWasalaam
Mwaka 2019 sitausahau kwa tukio hili
Kwa kifupi mimi ni mwenyeji sana wa maeneo ya Kimara Suka na Temboni
Maisha yaliniendea poa baada tuu ya kumaliza chuo...lakini hapo katikati ukiwemo 2019 hayakuwa poa kabisa
Siku moja jioni kulikua na mechi sikumbuki alikuwa anacheza man city na nani...nikasema hebu nipite hapa kwenye hii bar niulize mechi ni saa ngapi,karibu tuu mlangoni baada ya kuingia nikaona meza moja amekaa mtu mmoja wa makamo na mwingine alikuwa mzee kabisa mtu mzima...nikawasalimia nikaenda kukaa meza ya pembeni nikaagiza kinywaji
Ghafla yule mtu wa makamo akainuka kwa kufura kanifuata..."wewe unatusalimia unatujua?si ndio wezi ninyi..."katika kushikwa na butwaa nisijue na mimi ni react au vipi mzee akaanza kunisulubia makofi na mateke,alikuwa na vijana wengine meza za pembeni chawa wake wakaanza kunishushia kichapo huku wanasema hawa ni wezi...nilijitetea kwa uchungu nikasema jamani mimi mkazi wa maeneo haya isitoshe ni muumini wa hapa(ki pub kilikuwa karibu na Kanisa Katoliki Mavurunza)
.jamaa wakasema muongo...nikajitetea zaidi kuwa naimba hata kwaya mwiteni muumini yeyote loh watu wakazidi kuwa wengi huku wengine wanasema kaleteni mafuta loh nilianza kukata tamaa
Dakika kama 10 hivi baadhi ya barmaids walianza kunitetea...yule mzee ndio kwanza akapiga simu aletewe mkia wa Taa...mkia wa samaki mmoja hivi kama unavipelepele...dakika chache ukawa umefika...huku wengine wakinipiga na fimbo yeye alikuwa akinisulubia na huu mkia...loh maumivu makali sijawahi kuona...mkia ulinichanachana
Hatimaye baada ya kujitetea na kuona hawanielewi niliwaambia basi niueni hapo nikiwa nimekata tamaa na kumlilia sana Mungu kwa uchungu
Baada ya watu kumbana mzee nimemwibia nini na hakuwa na majibu ...kwa aibu alipiga simu kuuliza kama kuna gari ya polisi ilikuwa Doris maeneo ya Temboni ije kunichukua...ndio nikajua huyu kumbe alikuwa Afisa Mkubwa wa Jeshi la Polisi...baadae akaamua na yule mzee nikafungwa kamba kama mbuzi nikatupwa nyuma kwenye gari yake mpaka Gogoni Police Station...alivyonishusha nilimmshambulia kwa maneno makali sana huku akiwapa oda askari waliokuja kunichukua kuendelea kunipiga...sikusikia maumivu tena
..nilimtamkia maneno yote ya laana
Asubuhi yake niliulizwa na mkuu wa kituo unashtakiwa kwanini na nani nikamjibu simjui muulize askari alienipeleka...nikaandikiwa natuhumiwa kwa uhalifu bila kuutaja uhalifu wenyewe...nilipandishwa mahakamani...asante Mungu nilipata dhamana na hakimu nilivyorudi mara ya pili akafuta kesi
Swali...Hivi vetting ya polisi lazima uwe na roho mbaya ya kishetani au ni kozi mnasoma huko huko?
Tunafundishwa kusamehe...sasa kuamua kumpotezea mtu kama yule ndio kusamehe au kuna kwenda mbali zaidi?
Hapa Bongo Ukipona Mikononi mwa Polisi we nenda katoe sadaka. Ukijidai mjuaji utaisahau familia yako.Ukasamehe kirahisi hivyo?
Kuna kitu unaficha au una shida kubwa sana.
Kwanini usimfungulieashitaka au kumlipia kisasi kwa njia za mitaani.
Kitu gani unahisi nikiweke wazi...sijui kuficha vitu zikiwemo aibu zanguKunakitu unaficha
Uonevu ukizidi tena kwa sababu ya kijinga kama hiyo nipo tayari kufa au kuishia jela.Hapa Bongo Ukipona Mikononi mwa Polisi we nenda katoe sadaka. Ukijidai mjuaji utaisahau familia yako.
Mkuu nampongeza kwa kujikalia kimya akauponya uhai wake
KabisaAlikuwa anatafuta ujiko kwa bar maids....
Kabisa mkuuMuulize mdude wa chadema kuhusu yule askari mafwele ndo utajua hii nchi imejaa vilaza kila sehemu
Elimu ndogo na kupeana kazi kwa vimemo ndo imetufikisha huku
Asee sio watu si inaona wako radhi kuua ili wadhulumu mali ya mtuPole sana! Hawa watu ni watu,ila ukiwakuta na stess zao sio watu ni zaidi ya majitu!
Hii ningepotezea ila siyo kitendo alichafanyiwa mleta mada.Mimi polisi mwaka huo huo kijana want alimaliza f4, akawa anaendesha pkpk yangu. Polisi jirani akaniambia kijana wako Hana leseni na Kuna msako anataka kunisaidia apate leseni haraka nimpe 250k
Nikatoa kumbe wamechukua hela kwa vijana karibia 30, Sasa ikawa ukiuliza hiyo hela ni balaa.
Wanamvizia kijana wako wanamkamata, mzazi ukienda unaswekwa ndani hamna dhamana.
Utatoa rushwa Hadi ukome ndo utoke!
Hivyo ambao hawakuwekwa mahabusu wakakimbia kudai zile pesa.
Hawa jamaa wanamafunzo mengi ya kupora raia.
Wengi ni wahuni TU na roho mbaya zao wanaishia maisha ya hovyo sana!Wasalaam