Nilidhulumiwa na Polisi(Afisa) kidogo niuawe

Hawa watu bwana mi hata ndugu yangu akipata hiyo kazi undugu unakufa, na najitahidi sana kuishi maisha yasiyoweza kunikutanisha nao ila ndo kama hivyo bahati mbaya hutokea... I still remember vividly one of 'em once put a gun on mi head, a fkng loaded gun, ni Mungu tu kwamba yale yaliisha.
Mzee wangu aliweka msimamo asitokee mtoto wake kufanya kazi hii...aliibiwa gunia zaidi ya 150 halafu wakawa wanamuomba rushwa
 
Nina kisasi kibaya sana ambacho kinakaa rohoni miaka mingi ikiwa nimedhuliwa jambo ambalo linaonekana...

Yangenikuta mimi ki ukweli ningechukua hata miaka mi tano ila jambo lingemkuta naamini ni mara tano yake.. Hapo asingejua ni nani wala hata kunifikiria ni mimi kwani miaka ingekuwa ishapita sana na nimefanya utafiti wa hali ya juu.
Miaka imepita nadhani lau naweza kumhadithia mtu yeyote
 
Wanakuwaga na mashetani tu na huvuta bangi; au unakuta wamekuwa na kuzulumu Roho za watu, hayo ndo matokeo yake!
Polisi nenda kafuatilie taratibu za kupata vibali au kuripoti upotevu wa vitu kama taratibu zinavyodai na sio kujihusianisha nao
 
Ukasamehe kirahisi hivyo?
Kuna kitu unaficha au una shida kubwa sana.
Kwanini usimfungulie mashitaka au kulipa kisasi kwa njia za mitaani.
Umfungulie mashitaka polisi katika mahakama zetu hizi hizi?kumbuka muda huo sikuwa na chochote hali ngumu na huyu Afisa sijui ni Inspekta nani huko ...kwenye mfumo wa haki ningetoboa?

Mimi ni mkristo sina ujasiri wa kumfanyia mnyama mtu mathalani kwa njia hizo za mtaani...dhamiri yangu ni hai
 
Mimi polisi mwaka huo huo kijana want alimaliza f4, akawa anaendesha pkpk yangu. Polisi jirani akaniambia kijana wako Hana leseni na Kuna msako anataka kunisaidia apate leseni haraka nimpe 250k
Nikatoa kumbe wamechukua hela kwa vijana karibia 30, Sasa ikawa ukiuliza hiyo hela ni balaa.
Wanamvizia kijana wako wanamkamata, mzazi ukienda unaswekwa ndani hamna dhamana.
Utatoa rushwa Hadi ukome ndo utoke!
Hivyo ambao hawakuwekwa mahabusu wakakimbia kudai zile pesa.
Hawa jamaa wanamafunzo mengi ya kupora raia.
Wana laana kubwa
 
When you’re outside make sure umevaa vizuri, umenyoa vizuri pia muonekano mzuri na usafi utakuepusha na mambo ya kifala kama hayo…

Ukiwa rafu unafanania kusingiziwa majanga lastly tengenezeni muscles kidogo jamani muwe na mionekano na nguvu za kufanya adui ajifikirie mara mbili kuku-attack maana akikosea kidogo umevunja kiuno

When you’re outside make sure umevaa vizuri, umenyoa vizuri pia muonekano mzuri na usafi utakuepusha na mambo ya kifala kama hayo…

Ukiwa rafu unafanania kusingiziwa majanga lastly tengenezeni muscles kidogo jamani muwe na mionekano na nguvu za kufanya adui ajifikirie mara mbili kuku-attack maana akikosea kidogo umevunja kiuno.
Muonekano wangu mkuu very innocent
 
Wasalaam

Mwaka 2019 sitausahau kwa tukio hili
Kwa kifupi mimi ni mwenyeji sana wa maeneo ya Kimara Suka na Temboni

Maisha yaliniendea poa baada tuu ya kumaliza chuo...lakini hapo katikati ukiwemo 2019 hayakuwa poa kabisa

Siku moja jioni kulikua na mechi sikumbuki alikuwa anacheza man city na nani...nikasema hebu nipite hapa kwenye hii bar niulize mechi ni saa ngapi,karibu tuu mlangoni baada ya kuingia nikaona meza moja amekaa mtu mmoja wa makamo na mwingine alikuwa mzee kabisa mtu mzima...nikawasalimia nikaenda kukaa meza ya pembeni nikaagiza kinywaji

Ghafla yule mtu wa makamo akainuka kwa kufura kanifuata..."wewe unatusalimia unatujua?si ndio wezi ninyi..."katika kushikwa na butwaa nisijue na mimi ni react au vipi mzee akaanza kunisulubia makofi na mateke,alikuwa na vijana wengine meza za pembeni chawa wake wakaanza kunishushia kichapo huku wanasema hawa ni wezi...nilijitetea kwa uchungu nikasema jamani mimi mkazi wa maeneo haya isitoshe ni muumini wa hapa(ki pub kilikuwa karibu na Kanisa Katoliki Mavurunza)
.jamaa wakasema muongo...nikajitetea zaidi kuwa naimba hata kwaya mwiteni muumini yeyote loh watu wakazidi kuwa wengi huku wengine wanasema kaleteni mafuta loh nilianza kukata tamaa

Dakika kama 10 hivi baadhi ya barmaids walianza kunitetea...yule mzee ndio kwanza akapiga simu aletewe mkia wa Taa...mkia wa samaki mmoja hivi kama unavipelepele...dakika chache ukawa umefika...huku wengine wakinipiga na fimbo yeye alikuwa akinisulubia na huu mkia...loh maumivu makali sijawahi kuona...mkia ulinichanachana

Hatimaye baada ya kujitetea na kuona hawanielewi niliwaambia basi niueni hapo nikiwa nimekata tamaa na kumlilia sana Mungu kwa uchungu

Baada ya watu kumbana mzee nimemwibia nini na hakuwa na majibu ...kwa aibu alipiga simu kuuliza kama kuna gari ya polisi ilikuwa Doris maeneo ya Temboni ije kunichukua...ndio nikajua huyu kumbe alikuwa Afisa Mkubwa wa Jeshi la Polisi...baadae akaamua na yule mzee nikafungwa kamba kama mbuzi nikatupwa nyuma kwenye gari yake mpaka Gogoni Police Station...alivyonishusha nilimmshambulia kwa maneno makali sana huku akiwapa oda askari waliokuja kunichukua kuendelea kunipiga...sikusikia maumivu tena
..nilimtamkia maneno yote ya laana

Asubuhi yake niliulizwa na mkuu wa kituo unashtakiwa kwanini na nani nikamjibu simjui muulize askari alienipeleka...nikaandikiwa natuhumiwa kwa uhalifu bila kuutaja uhalifu wenyewe...nilipandishwa mahakamani...asante Mungu nilipata dhamana na hakimu nilivyorudi mara ya pili akafuta kesi

Swali...Hivi vetting ya polisi lazima uwe na roho mbaya ya kishetani au ni kozi mnasoma huko huko?

Tunafundishwa kusamehe...sasa kuamua kumpotezea mtu kama yule ndio kusamehe au kuna kwenda mbali zaidi?
Umechelewa sana aisee, tungepiga pesa ndefu sana, pensheni ya huyo askari yote ingehamia kwako, na bado angeuza na mali zake nyingine ili kukufidia.

Siku nyingine ukipigwa na kushikiliwa isivyo halali, hakikisha ndani ya miaka 3 uwe umefungua kesi ya madai kwa kufungwa au kushikiliwa isivyo halali, utadai fidia kiasi chochote utakacho.
 
Muonekano wako ulikuwaje, nywele, nguo, utembeaji?

Sema kiukweli polisi ni watu wabaya sana. 2016 pale external nilikamatwa na askari wa barabarani, haha yule jamaa tuliwashana hadi kwa mkuu wa kituo, mkuu wa kituo akanyoosha mikono juu...
Very innocent
 
Umechelewa sana aisee, tungepiga pesa ndefu sana, pensheni ya huyo askari yote ingahamia kwako, na bado angeuza na mali zake nyingine ili kukufidia.

Siku nyingine ukipigwa na kushikiliwa isivyo halali, hakikisha ndani ya miaka 3 uwe umefungua kesi ya madai kwa kufungwa au kushikiliwa isivyo halali, utadai fidia kiasi chochote utakacho.
Sawa mkuu
 
Very innocent
Mkuu,
Ukiona mtu ana connection ya mapolisi, ujue huyo ni mhalifu anakula nao. Ila ukiwa mtu straight, mapolisi ni watu wabaya sana. Ukiwa na issue unaweza kudhani atakupa msaada kumbe ana-gang na wenzake ili wazidi kukuchapa hela zako.
 
Wasalaam

Mwaka 2019 sitausahau kwa tukio hili
Kwa kifupi mimi ni mwenyeji sana wa maeneo ya Kimara Suka na Temboni

Maisha yaliniendea poa baada tuu ya kumaliza chuo...lakini hapo katikati ukiwemo 2019 hayakuwa poa kabisa

Siku moja jioni kulikua na mechi sikumbuki alikuwa anacheza man city na nani...nikasema hebu nipite hapa kwenye hii bar niulize mechi ni saa ngapi,karibu tuu mlangoni baada ya kuingia nikaona meza moja amekaa mtu mmoja wa makamo na mwingine alikuwa mzee kabisa mtu mzima...nikawasalimia nikaenda kukaa meza ya pembeni nikaagiza kinywaji

Ghafla yule mtu wa makamo akainuka kwa kufura kanifuata..."wewe unatusalimia unatujua?si ndio wezi ninyi..."katika kushikwa na butwaa nisijue na mimi ni react au vipi mzee akaanza kunisulubia makofi na mateke,alikuwa na vijana wengine meza za pembeni chawa wake wakaanza kunishushia kichapo huku wanasema hawa ni wezi...nilijitetea kwa uchungu nikasema jamani mimi mkazi wa maeneo haya isitoshe ni muumini wa hapa(ki pub kilikuwa karibu na Kanisa Katoliki Mavurunza)
.jamaa wakasema muongo...nikajitetea zaidi kuwa naimba hata kwaya mwiteni muumini yeyote loh watu wakazidi kuwa wengi huku wengine wanasema kaleteni mafuta loh nilianza kukata tamaa

Dakika kama 10 hivi baadhi ya barmaids walianza kunitetea...yule mzee ndio kwanza akapiga simu aletewe mkia wa Taa...mkia wa samaki mmoja hivi kama unavipelepele...dakika chache ukawa umefika...huku wengine wakinipiga na fimbo yeye alikuwa akinisulubia na huu mkia...loh maumivu makali sijawahi kuona...mkia ulinichanachana

Hatimaye baada ya kujitetea na kuona hawanielewi niliwaambia basi niueni hapo nikiwa nimekata tamaa na kumlilia sana Mungu kwa uchungu

Baada ya watu kumbana mzee nimemwibia nini na hakuwa na majibu ...kwa aibu alipiga simu kuuliza kama kuna gari ya polisi ilikuwa Doris maeneo ya Temboni ije kunichukua...ndio nikajua huyu kumbe alikuwa Afisa Mkubwa wa Jeshi la Polisi...baadae akaamua na yule mzee nikafungwa kamba kama mbuzi nikatupwa nyuma kwenye gari yake mpaka Gogoni Police Station...alivyonishusha nilimmshambulia kwa maneno makali sana huku akiwapa oda askari waliokuja kunichukua kuendelea kunipiga...sikusikia maumivu tena
..nilimtamkia maneno yote ya laana

Asubuhi yake niliulizwa na mkuu wa kituo unashtakiwa kwanini na nani nikamjibu simjui muulize askari alienipeleka...nikaandikiwa natuhumiwa kwa uhalifu bila kuutaja uhalifu wenyewe...nilipandishwa mahakamani...asante Mungu nilipata dhamana na hakimu nilivyorudi mara ya pili akafuta kesi

Swali...Hivi vetting ya polisi lazima uwe na roho mbaya ya kishetani au ni kozi mnasoma huko huko?

Tunafundishwa kusamehe...sasa kuamua kumpotezea mtu kama yule ndio kusamehe au kuna kwenda mbali zaidi?
Nenda tume ya haki za binaadamu ukamrepoti huyo polisi
 
Hawa watu bwana mi hata ndugu yangu akipata hiyo kazi undugu unakufa, na najitahidi sana kuishi maisha yasiyoweza kunikutanisha nao ila ndo kama hivyo bahati mbaya hutokea... I still remember vividly one of 'em once put a gun on mi head, a fkng loaded gun, ni Mungu tu kwamba yale yaliisha.
Sio wote wana roho mbaya ..kuna wengine wapo vzuri tu
 
Pole ila Kuna kitu kinamiss kwenye hii simulizi.
 
kweli vitoto vya elfumbili ni vya ajabu sana,...yaani unapigwa bila kosa tena unapigwa na kizee?....itoshe kusema wewe ni fala🚮🚮
 
Back
Top Bottom