Nilidhulumiwa na Polisi(Afisa) kidogo niuawe

Wasalaam

Mwaka 2019 sitausahau kwa tukio hili
Kwa kifupi mimi ni mwenyeji sana wa maeneo ya Kimara Suka na Temboni

Tunafundishwa kusamehe...sasa kuamua kumpotezea mtu kama yule ndio kusamehe au kuna kwenda mbali zaidi?
Kwani huyo askari alikuwa anaishi mbinguni? Ukamwacha tu halafu unatuambia sisi? Jamani hawa askari ni wanadamu kama sisi. Kuna mazingira ambayo wanapigika vizuri tu. Hata kama amestaafu na kuzeeka, mtafute alipo.
 
Maisha yaliniendea poa baada tuu ya kumaliza chuo...lakini hapo katikati ukiwemo 2019 hayakuwa poa kabisa

Siku moja jioni kulikua na mechi sikumbuki alikuwa anacheza man city na nani...nikasema hebu nipite hapa kwenye hii bar niulize mechi ni saa ngapi,karibu tuu mlangoni baada ya kuingia nikaona meza moja amekaa mtu mmoja wa makamo na mwingine alikuwa mzee kabisa mtu mzima...nikawasalimia nikaenda kukaa meza ya pembeni nikaagiza kinywaji

Ghafla yule mtu wa makamo akainuka kwa kufura kanifuata..."wewe unatusalimia unatujua?si ndio wezi ninyi..."katika kushikwa na butwaa nisijue na mimi ni react au vipi mzee akaanza kunisulubia makofi na mateke,alikuwa na vijana wengine meza za pembeni chawa wake wakaanza kunishushia kichapo huku wanasema hawa ni wezi...nilijitetea kwa uchungu nikasema jamani mimi mkazi wa maeneo haya isitoshe ni muumini wa hapa(ki pub kilikuwa karibu na Kanisa Katoliki Mavurunza)
.jamaa wakasema muongo...nikajitetea zaidi kuwa naimba hata kwaya mwiteni muumini yeyote loh watu wakazidi kuwa wengi huku wengine wanasema kaleteni mafuta loh nilianza kukata tamaa

Dakika kama 10 hivi baadhi ya barmaids walianza kunitetea...yule mzee ndio kwanza akapiga simu aletewe mkia wa Taa...mkia wa samaki mmoja hivi kama unavipelepele...dakika chache ukawa umefika...huku wengine wakinipiga na fimbo yeye alikuwa akinisulubia na huu mkia...loh maumivu makali sijawahi kuona...mkia ulinichanachana

Hatimaye baada ya kujitetea na kuona hawanielewi niliwaambia basi niueni hapo nikiwa nimekata tamaa na kumlilia sana Mungu kwa uchungu

Baada ya watu kumbana mzee nimemwibia nini na hakuwa na majibu ...kwa aibu alipiga simu kuuliza kama kuna gari ya polisi ilikuwa Doris maeneo ya Temboni ije kunichukua...ndio nikajua huyu kumbe alikuwa Afisa Mkubwa wa Jeshi la Polisi...baadae akaamua na yule mzee nikafungwa kamba kama mbuzi nikatupwa nyuma kwenye gari yake mpaka Gogoni Police Station...alivyonishusha nilimmshambulia kwa maneno makali sana huku akiwapa oda askari waliokuja kunichukua kuendelea kunipiga...sikusikia maumivu tena
..nilimtamkia maneno yote ya laana

Asubuhi yake niliulizwa na mkuu wa kituo unashtakiwa kwanini na nani nikamjibu simjui muulize askari alienipeleka...nikaandikiwa natuhumiwa kwa uhalifu bila kuutaja uhalifu wenyewe...nilipandishwa mahakamani...asante Mungu nilipata dhamana na hakimu nilivyorudi mara ya pili akafuta kesi

Swali...Hivi vetting ya polisi lazima uwe na roho mbaya ya kishetani au ni kozi mnasoma huko huko?

Huu no uongo huezi ukaanza kupigwa tuh alaf uwe walalamika na kujitetea pambana mpk Kila mtu ajue umeonewa ,maana mwizi akikamatwa hua arushi ngumi zaidi ya kujitetea Kwa maneno
 
Kuna Polisi mmoja hapa WILAYA YA MAGU namtafuta usiku na mchana .Nitakacho mfanyia na wengine majambazi kama yeye watajifunza
 
Umenikumbusha mbali sana.siku moja nipo kazini kwangu mara nikasikia watu wanapita jamaa mmoja (baadae niliambiwa ni afande)anamkimbiza mtu anamwita mwizi Mwizi mwiziii.mara kule mbele wananchi wakibeba mawe,fimbo na kumkamata yule aliyekuwa anakimbizwa na kuanza kumpa kipigo.kucheki hivi nikagundua yule anaepigwa nafahamu tena kijana mzuri tu hapa mtaani msabato kwelikweli.wenzangu wakasema yule alikuwa anamkibiza ni askari polisi.nikapandwa na hasira nikamvagaa yule askari nikamkwida shati kula makofi huku namwambia hivi ndivyo mlivyofundishwa kukamata watu huyu mtu akifa je.huna mbinu zingine za kiaskari ya kumkamata huyu unaemwita mwizi.nilimtoa mangeo na kuanza kutoka damu puani.sasa kuna wananchi wanamfahamu huyo askari tena ana nyota zake wakanisii nimwachie.namuuliza kosa la yule dogo anasema kamwimbia nini komeo la 5000.sasa ndio umwite mtu mwizi akiuwawa? Sasa baada ya kumwachia akapiga simu polisi ije gari mimi nikawa nimesema kidogo mara gari hili hapa wakabebwa watu watatu na yule dogo waliokuwa wanafanya kazi ktk duka.Jamaa akaanza kunitafuta na mimi nikaenda kwa bosi wake mkubwa nikatoa taarifa kile kilichotokea kisha akaniambia niende akampigia simu sijui walimalizaje na wale madogo walitoka
Uongo wa hivi mdanganye mama yako kidogo atakuamini.
 
Mkuu,
Ukiona mtu ana connection ya mapolisi, ujue huyo ni mhalifu anakula nao. Ila ukiwa mtu straight, mapolisi ni watu wabaya sana. Ukiwa na issue unaweza kudhani atakupa msaada kumbe ana-gang na wenzake ili wazidi kukuchapa hela zako.
Kabisa
 
Kwani huyo askari alikuwa anaishi mbinguni? Ukamwacha tu halafu unatuambia sisi? Jamani hawa askari ni wanadamu kama sisi. Kuna mazingira ambayo wanapigika vizuri tu. Hata kama amestaafu na kuzeeka, mtafute alipo.
Hahaha 6yrs imepita sasa
 
Pole sana mkuu jeshi la polisi hapa nchini maadili yao sio mazuri, wanakutafutia kesi hata kosa hauna wale utapeli uko juu sana.
 
Back
Top Bottom