Uonevu ukizidi tena kwa sababu ya kijinga kama hiyo nipo tayari kufa au kuishia jela.
Nitaenda wizarani hadi Ikulu au nitalipa kisasi au nitatafuta uchawi unapatikana wapi duniani.
Ningemtafuta huyo askari akiwa peke yake na kwa kumshitukiza.
Huyo labda alisalimia kihuni au alifanya kosa fulani dogo.
Angeomba radhi kwamba alilewa ninge msamehe haraka tu.
Mkuu kuna watu wana hulka mbaya sana kwenye maisha.
Nimewahi kutana na jambo kama hilo la dhihaka.
Kuna Mzee mmoja alikuwa na Binti mgonjwa(Moyo)
Tukiwa kikundi tumsindikiza tunatoka shule(Form 4)
Binti alizidiwa njiania katika harakati za kumpeleka Hospital tukafanikiwa,mmoja wetu alikuwa anaijua ile familia pale mjini.Akawahi kupeleka taarifa ofisini kwa Mama yake Binti.
Wakati tupo hapo Hos wenye Binti yao wakaja pamoja na Baba,sisi tulikuwa hapo pia.
Mama yake alituongelesha vizuri,mzee pasipo hiyana alisema hawa wanafunzi wavuta bangi ndio wamemsaidia binti yangu?Hawa wahuni ndio watakuwa wamempa binti yangu shida,
Hebu tumwamishe binti yetu hapa haraka tumepeleke kwingine nisije ua mtu hapa.
Tuliondoka pale Hospital mdogo mdogo masela na wadada tuliokuwa nao.
Ikapita muda sana nipo Home naona Mama wa yule Binti akaja Home kwetu na Matunda,Mayai na Kuku.Akazungumza na Bi mkubwa juu ya lile tukio,alifanya hivyo kwa baadhi ya familia majirani katika lie kundi.
Ikapita miaka 2,mambo ya Jumuiya haya.Nakutana na yule Mzee aliongea lakini sikumuelewa na alijua hilo.
Bahati mbaya zaidi kuna ndugu yetu kaoa huko😀😀😀😀😀kama ajali kazini.
Alimwambia Kaka aliyeoa ,kuna ndugu yako anamsimamo mkali sana najisikia kujutia kauli yangu juu yake kipindi flani.
Tumekua nilienda msalimia mana ni mgonjwa mgonjwa,Mzee uwe na amani ilikuwa hako yako kama Mzazi kutusema nyakati zile.