Hakuna mchaw mwenye uwezo huoUonevu ukizidi tena kwa sababu ya kijinga kama hiyo nipo tayari kufa au kuishia jela.
Nitaenda wizarani hadi Ikulu au nitalipa kisasi au nitatafuta uchawi unapatikana wapi duniani.
Ningemtafuta huyo askari akiwa peke yake na kwa kumshitukiza.
Huyo labda alisalimia kihuni au alifanya kosa fulani dogo.
Angeomba radhi kwamba alilewa ninge msamehe haraka tu.
Tungemalizana kihuni kimafia mtaani.Hakuna mchaw mwenye uwezo huo
Mkuu kuna watu wana hulka mbaya sana kwenye maisha.Uonevu ukizidi tena kwa sababu ya kijinga kama hiyo nipo tayari kufa au kuishia jela.
Nitaenda wizarani hadi Ikulu au nitalipa kisasi au nitatafuta uchawi unapatikana wapi duniani.
Ningemtafuta huyo askari akiwa peke yake na kwa kumshitukiza.
Huyo labda alisalimia kihuni au alifanya kosa fulani dogo.
Angeomba radhi kwamba alilewa ninge msamehe haraka tu.
Baadhi yao ni wezi majambazi na matapeliMimi polisi mwaka huo huo kijana want alimaliza f4, akawa anaendesha pkpk yangu. Polisi jirani akaniambia kijana wako Hana leseni na Kuna msako anataka kunisaidia apate leseni haraka nimpe 250k
Nikatoa kumbe wamechukua hela kwa vijana karibia 30, Sasa ikawa ukiuliza hiyo hela ni balaa.
Wanamvizia kijana wako wanamkamata, mzazi ukienda unaswekwa ndani hamna dhamana.
Utatoa rushwa Hadi ukome ndo utoke!
Hivyo ambao hawakuwekwa mahabusu wakakimbia kudai zile pesa.
Hawa jamaa wanamafunzo mengi ya kupora raia.
Sema wengi wao ndio wako hivyo. Aise hiyo taasisi ni aibu sana hata wao wenyewe hawako proud nayo.Baadhi yao ni wezi majambazi na matapeli
ChaiUmenikumbusha mbali sana.siku moja nipo kazini kwangu mara nikasikia watu wanapita jamaa mmoja (baadae niliambiwa ni afande)anamkimbiza mtu anamwita mwizi Mwizi mwiziii.mara kule mbele wananchi wakibeba mawe,fimbo na kumkamata yule aliyekuwa anakimbizwa na kuanza kumpa kipigo.kucheki hivi nikagundua yule anaepigwa nafahamu tena kijana mzuri tu hapa mtaani msabato kwelikweli.wenzangu wakasema yule alikuwa anamkibiza ni askari polisi.nikapandwa na hasira nikamvagaa yule askari nikamkwida shati kula makofi huku namwambia hivi ndivyo mlivyofundishwa kukamata watu huyu mtu akifa je.huna mbinu zingine za kiaskari ya kumkamata huyu unaemwita mwizi.nilimtoa mangeo na kuanza kutoka damu puani.sasa kuna wananchi wanamfahamu huyo askari tena ana nyota zake wakanisii nimwachie.namuuliza kosa la yule dogo anasema kamwimbia nini komeo la 5000.sasa ndio umwite mtu mwizi akiuwawa? Sasa baada ya kumwachia akapiga simu polisi ije gari mimi nikawa nimesema kidogo mara gari hili hapa wakabebwa watu watatu na yule dogo waliokuwa wanafanya kazi ktk duka.Jamaa akaanza kunitafuta na mimi nikaenda kwa bosi wake mkubwa nikatoa taarifa kile kilichotokea kisha akaniambia niende akampigia simu sijui walimalizaje na wale madogo walitoka
Elezea vizuri Mzee....kuna kitu umeficha.Wasalaam
Mwaka 2019 sitausahau kwa tukio hili
Kwa kifupi mimi ni mwenyeji sana wa maeneo ya Kimara Suka na Temboni
Maisha yaliniendea poa baada tuu ya kumaliza chuo...lakini hapo katikati ukiwemo 2019 hayakuwa poa kabisa
Siku moja jioni kulikua na mechi sikumbuki alikuwa anacheza man city na nani...nikasema hebu nipite hapa kwenye hii bar niulize mechi ni saa ngapi,karibu tuu mlangoni baada ya kuingia nikaona meza moja amekaa mtu mmoja wa makamo na mwingine alikuwa mzee kabisa mtu mzima...nikawasalimia nikaenda kukaa meza ya pembeni nikaagiza kinywaji
Ghafla yule mtu wa makamo akainuka kwa kufura kanifuata..."wewe unatusalimia unatujua?si ndio wezi ninyi..."katika kushikwa na butwaa nisijue na mimi ni react au vipi mzee akaanza kunisulubia makofi na mateke,alikuwa na vijana wengine meza za pembeni chawa wake wakaanza kunishushia kichapo huku wanasema hawa ni wezi...nilijitetea kwa uchungu nikasema jamani mimi mkazi wa maeneo haya isitoshe ni muumini wa hapa(ki pub kilikuwa karibu na Kanisa Katoliki Mavurunza)
.jamaa wakasema muongo...nikajitetea zaidi kuwa naimba hata kwaya mwiteni muumini yeyote loh watu wakazidi kuwa wengi huku wengine wanasema kaleteni mafuta loh nilianza kukata tamaa
Dakika kama 10 hivi baadhi ya barmaids walianza kunitetea...yule mzee ndio kwanza akapiga simu aletewe mkia wa Taa...mkia wa samaki mmoja hivi kama unavipelepele...dakika chache ukawa umefika...huku wengine wakinipiga na fimbo yeye alikuwa akinisulubia na huu mkia...loh maumivu makali sijawahi kuona...mkia ulinichanachana
Hatimaye baada ya kujitetea na kuona hawanielewi niliwaambia basi niueni hapo nikiwa nimekata tamaa na kumlilia sana Mungu kwa uchungu
Baada ya watu kumbana mzee nimemwibia nini na hakuwa na majibu ...kwa aibu alipiga simu kuuliza kama kuna gari ya polisi ilikuwa Doris maeneo ya Temboni ije kunichukua...ndio nikajua huyu kumbe alikuwa Afisa Mkubwa wa Jeshi la Polisi...baadae akaamua na yule mzee nikafungwa kamba kama mbuzi nikatupwa nyuma kwenye gari yake mpaka Gogoni Police Station...alivyonishusha nilimmshambulia kwa maneno makali sana huku akiwapa oda askari waliokuja kunichukua kuendelea kunipiga...sikusikia maumivu tena
..nilimtamkia maneno yote ya laana
Asubuhi yake niliulizwa na mkuu wa kituo unashtakiwa kwanini na nani nikamjibu simjui muulize askari alienipeleka...nikaandikiwa natuhumiwa kwa uhalifu bila kuutaja uhalifu wenyewe...nilipandishwa mahakamani...asante Mungu nilipata dhamana na hakimu nilivyorudi mara ya pili akafuta kesi
Swali...Hivi vetting ya polisi lazima uwe na roho mbaya ya kishetani au ni kozi mnasoma huko huko?
Tunafundishwa kusamehe...sasa kuamua kumpotezea mtu kama yule ndio kusamehe au kuna kwenda mbali zaidi?
Kabisa nikilegea katika ya Mungu nae akabadilika na kutenda ya haki huo ndio ukweliMungu wa Rehema na Neema usishangae yule mzee anaenda mbinguni harafu wewe ukaenda Motoni.
Hii imani ni complex sana
Wewe utakua polisi au hujanielewa?rudia story yanguMkuu chai yako ni mbichi. Kwamba polisi wakataka wakuchome moto ila barmaids wakawaombea.Polisi hayo mamlaka wanayotoa wapi ya kukuchoma moto!!!
Huu ni ongo..!! 😃😂
Siwezi kusamehe upumbavu. Ningekula nae sahani Moja kwa namna ya pekee sana.Tunafundishwa kusamehe...sasa
Nilikua na muonekano wa kawaida ...sijawahi kuwa na muonekano wa kihuni na siwapendi wahuniMuonekano wako ulikuwaje, nywele, nguo, utembeaji?
Sema kiukweli polisi ni watu wabaya sana. 2016 pale external nilikamatwa na askari wa barabarani, haha yule jamaa tuliwashana hadi kwa mkuu wa kituo, mkuu wa kituo akanyoosha mikono juu...
Dingi huyo ana roho mbaya tu. Anakaa anafikiria nitamuumizaje mtu. "Aha! Ngoja nipate mkia wa taa." Anaanza process za kuutafuta, anaupata na kuutunza ili siku moja aje amgawie binadamu mwenzake mau
Kaka huwa nafikiria neno kusamehe naishia kusema namuachia MunguSiwezi kusamehe upumbavu. Ningekula nae sahani Moja kwa namna ya pekee sana.
Sifichi kitu...usikutane polisi mkuu kwenye anga zao ...hujasikia polisi kwenye tuhuma za utekaji....uuaji kupora mali za watu...uepushiwe yasikukuteKunakitu unaficha