Nilifuma SMS za mapenzi kwenye simu ya mke siku yetu ya ndoa, bado nikamuoa lakini sasa nahisi kuchanganyikiwa sielewi nifanyeje?

Ushauri wangu inabidi hapo ulieee sana machozi yakitoka ukinyamza hutafanya tena upuuzi kama huo.
 
ahsante kaka
 
Mwamba hapo umepigwa 100%, jiandae kwa maumivu makali zaidi ndani ya ndoa. Hizo mbanga huwa sio za kukimbilia kuzioa, hizo waachie wazee waliofiwa na wake zao, watu wazima waliochana na wake zao nk.

Ulikubali vipi kizembe hivyo kuingia kichwa kichwa na kuoa?
Ulilogwa?
 
Na bado..
Ila huyo mkewako ana nyota ya ndoa sana ..
Inaonekana kakudanganya mengi sana
.
Haya na wewe muache akaolewe kwingine
Upuuzi mtupu ..
 
Mungu aliamua kukusaidia kwa kukuonyesha kitu kikubwa kibaya kabla ya kumuoa, sasa ikawaje tena ukapuuzia?

Hiyo issue ya Sms ulipoipata siku ile, ilipaswa kwanza uhairishe suala la kuoa, ungepiga break na kusikilizia kwa muda zaidi.
 
Narudia tena kuwaonya vijana, ukishaona cheche, chenga chenga au Red light kwenye njia ya kuelekea kuoa, unapaswa mara mara kupiga break, vuta kabisa na hand break, subiri zaidi na tafakari upya. Huenda mtu anayetaka kumuoa/kukuoa sio sahihi au wakati wa kuoa sio sahihi.
 
sure ndugu yangu
 
Ushauri wangu wa kukusaidia tu kwa sasa ni huu, please zingatia zaidi.
Mosi, kaa kwa tahadhari kubwa, ishi kwa hekima, kuwa mwerevu zaidi na makini. Fanya hivi kwa at least miaka mitatu.
Pili, muombe sana Mungu kuhusu hatma yako na hatma ya ndoa yako.
Mwisho, endelea kuishi na mkeo wa amani na furaha, subiri muda na nature iamue.
 
ahsante sana kaka
 
ahsante sana kaka
Wewe ni mwanaume, hii issue nina uhakika utatoboa tu, kujua tatizo na kuomba ushauri hiyo ni hatua kubwa umeweza kuifikia, the rest ni muda, umakini na uvumilivu.
Mwanaume kukosea katika maamuzi ya ndoa sio jambo la ajabu, wanaume waliofanikiwa kwenye ndoa ni wale walioweza kupambana kurekebisha makosa waliyoyafanya.
 
Nashkuru sana kaka maana umenipa nguvu na moyo naamini nikijipa muda kwa umakini,busara na uvumilivu nitatoboa inshaallah maana MUNGU yuko pamoja na wenye SUBRA.Nashkuru sana ndugu yangu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…