Until_The_End
JF-Expert Member
- Nov 21, 2020
- 1,456
- 2,202
Tatizo ni pale unapotaka kuishi ili uheshimiwe.Binadamu kuna mambo usipomuonyesha hato kuheshimu.
Pole sana ndugu
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Tatizo ni pale unapotaka kuishi ili uheshimiwe.Binadamu kuna mambo usipomuonyesha hato kuheshimu.
Kwa kuwa umetoa suluhisho ni sawa, nakubali kuwa mimi ni mchafu na yeye ni msafi,Siamini kama kuna mwanaume ataweka condition ya kupasha kiporo ili ahudumie wanae.
Nachojua akitaka kupasha kiporo ataanza kuhudumia na kulipa bili zote plus zako binafsi e.g kununua nguo na zawadi za mara kwa mara bila kuombwa, na mwisho kiporo unakipeleja mwenyewe.
Maelezo yako umejiweka wewe ni safi sana jambo ambalo inaonesha wewe ndio mchafu zaidi.
Pole dada, uzuri maisha hayawezi kusimama iwe kwako au kwa huyo adui yako. Kwahiyo Take it easy.
Labda nimefupisha sana kiasi watu mmehisi nimeleta malalamiko, haikuwa lengo kama ulivyotafsiri. AsanteNimesoma uzi wako kwa umakini,
Ila nitakua mbaya kusikiliza upande mmoja,
Ila kuna namna pia wewe una tatizo sehem...
Hakuna mkamilifu, mwanaume alikukosea na hauwezi badilisha huo ndio ukweli...
Ameomba nafasi ya kulea wanae na una mkatalia..je unadhani umefanya hekima?
Angalau ungepata unafuu wa maisha,je unamkomoa nani?
Baba,watoto ama wewe mwenyewe?
Utajitesa kuwalea mwenyewe ila mwisho wa siku watoto wakikua watamtafuta baba yao, kama kuna todauti watazimaliza.
Lengo la kuandika huu uzi hapa ni nini ikiwa unakataa msaada wa mzazi mwenzio...je lengo tukuchangie watu baki angali baba wa watoto yupo?
Mpe mzazi mwenzio haki yake,
Hao ni watoto wake pia.
Lengo ni nini?Labda nimefupisha sana kiasi watu mmehisi nimeleta malalamiko, haikuwa lengo kama ulivyotafsiri. Asante
We usiniletee hayo maandiko wakoloni waliyatumia kutawala babu zetu, ukimsamehe adui yako unapata faida gani?Asipomsamehe anapata faida gani?
Kutokusamehe mwisho wake ni kutaka kulipa kisasi, je kisasi kinamazuri ndani yake?
Wapendeni adui zenu, waombeeni wanaowaudhi.
Lazima uishi kuheshimiwa, kuna faida katika kuheshimiwa au we unataka kuishi udharaulike?Tatizo ni pale unapotaka kuishi ili uheshimiwe.
Pole sana ndugu
Faida gani?Kuna faida katika kulipa kisasi
Oh kumbe hujaelewa nilichoandika?Oh kumbe kasema hakuheshimu ndoa yake?
Indeed this is a very good ideaJamiiforum wangeweka utaratibu wa wao kudhibitisha identify ya mtu, kisha wanaoguswa wakaweza kumsaport mtu kwa account ya jamiiforum, wengi wanapitia magumu ambayo kwa kidogo mtu alichonacho kingeleta relief.
All in all pole sana dada angu.
Ye kipindi ananifanyia ubaya hakujua itaniumiza na watu wanaonitegemea?Faida gani?
Kisasi kina hasara tu wala hakina faida, utaumiza mtu bure na inaweza kupelekea kuumiza wengine pia wasiohusika katika ugomvi.
Na kama ulitendewa ubaya huwezi kubadili yaliyopita.
Mbona ameshaeleza chanzo cha mwanaume kukimbia wazee?,amesema hakujua sababu ya mwanaume kuondoka lakin baadae alikuja kuambiwa na ndugu wa mwanaume kuwa mume wake ameatumia ndugu wa pande zote ujumbe kuwa huyu mtoto wa pili si wake,ina maana mwanamke alichepuka,hicho ndio chanzo kwa maelezo yake lakin hizo tuhuma sio kweliHuko nimefika ili kujaribu kufumua mafaili lakini unakataa kua sio kisa au chanzo cha mgogoro wenu, Sasa wewe unahisi chanzo cha yeye kukukimbia ni nini ikiwa kwamba unaamini yeye sio kichaa na ni mtu ulimchagua mpaka ukifika uamuzi wa kumzalia watoto Ina maana yupo timamu sio chizi, chanzo cha yeye kukuacha na kukukimbia ni nini, kiburi, majivuno, kujiona, majisifu, kutokumsikiliza au nini ?
Hapo upo sahihi kabisaKuwasaidia watoto ni mpaka akutane na mimi faragha? Mwenye nia ya kuwasaidia watoto angewasaidia tu, ndio maana nikikataa analeta maneno kama nilyosema kuwa nina jeuri, kiburi, nitakuwa na mwanaume ambaye ananipa kiburi, na kusema hatawasaidia kwa kuwa nakataa.
Nadhani hamjaelewa, lengo la msaada wake ni mpaka akumbushie na mimi maana yake apashe kiporo, nimeandika bila kufunguka nikajua mnaweza kuelewa.
Mimi na yeye tulishamaliza safari, siwezi kuruhusu hicho kitu kitokee abadani asilani eti ili watoto wapate matunzo.