Nilijikuta naishi maisha ambayo sikuyategemea ila sina jinsi

Nilijikuta naishi maisha ambayo sikuyategemea ila sina jinsi

Mbona ameshaeleza chanzo cha mwanaume kukimbia wazee?,amesema hakujua sababu ya mwanaume kuondoka lakin baadae alikuja kuambiwa na ndugu wa mwanaume kuwa mume wake ameatumia ndugu wa pande zote ujumbe kuwa huyu mtoto wa pili si wake,ina maana mwanamke alichepuka,hicho ndio chanzo kwa maelezo yake lakin hizo tuhuma sio kweli
Hapana hicho sio chanzo hio ni hearsay akisikia kwa watu wakisema nataka aseme chanzo na anakijua Ila hataki kusema ukweli na ukisoma huko juu amesema hatoniambia au hatotuambia chanzo au source ya huyo Mwanaume kumkimbia ukiondoa hio hearsay aliyoisikia kwa watu wakisema, yeye chanzo halisi anakijua
 
Mbona watu wa kataa ndoa hawaji[emoji1787][emoji1787]
Mwanamke hatakiwi kukataa ndoa haijalishi anapitia masaibu kiasi gani mkuu, maana ameumbwa na moyo wa chuma wa kuvumilia makosa ya mumewe, ila mwanaume ni haki yake kukataa ndoa sababu yeye kaumbwa delicate hatakiwi kuvumilia makosa ya mwanamke
 
Baba yao kama walivyo wababa wengine wapuuzi, alikua anatafuta njia ya kujirudi Kwa mwanamke aendelee kupasha viporo.

Lkn pia inawezekana mpaka akataka kujirudi nisababu alipokuja mambo yalibadilika.

Ni chaguzi sahihi sana ALOFANYA mtoa Mada hata kama ana shida ya Uchumi.

Kuhusu wababa kutulia kwenye Ndoa zao, hapa suala ni Akili ya Mwanaume mwenyewe , Kuna hao wanachepuka na kusahau familia, alafu Kuna Mimi, nachepuka lkn Huniambii kitu Kwa Wife na wanangu na wanangu wengine.
Same same to me[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
 
Mwanamke hatakiwi kukataa ndoa haijalishi anapitia masaibu kiasi gani mkuu, maana ameumbwa na moyo wa chuma wa kuvumilia makosa ya mumewe, ila mwanaume ni haki yake kukataa ndoa sababu yeye kaumbwa delicate hatakiwi kuvumilia makosa ya mwanamke
Eeeeeh, kazi tunayo wanawake loh
 
Same same to me[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
Si umeona Binadamubwana amefurahi au umefumba macho, mwambie aelezee chanzo au source ya jamaa kumkimbia ondoa hio nilisikia ndugu zake wakisema amewaambia no no sio hio kuna ile deep yenyewe hata yeye anajua ndio chanzo Cha mvurugano, anajua na kusema hataki
 
Umesoma Uzi wake wote? Kuna mabaya mumewe aloyafanya na hataki kuyaandika hapa.

Ukweli nikwamba amekua jasiri kiasi Cha kuandika hapa na pengine ameandika huku analia.

Kama Kuna sababu za kwake, ninkwann Mumewe baadae aanze kujirudi??.
Watu wengine wanasoma bila kuelewa mkuu
 
Si umeona Binadamubwana amefurahi au umefumba macho, mwambie aelezee chanzo au source ya jamaa kumkimbia ondoa hio nilisikia ndugu zake wakisema amewaambia no no sio hio kuna ile deep yenyewe hata yeye anajua ndio chanzo Cha mvurugano, anajua na kusema hataki
Yawezekana wewe unakijua kiseme, nilishasema nina mengi ila siwezi eleza naona mmekazania
 
Hapana Mimi nasimama upande wa mumewe mpaka akisema chanzo Cha yeye kukimbiwa ni nini ? Kwanini anaficha chanzo we hutatoaje hukumu bila kujua chanzo Cha tukio lenyewe husika, huyu anajua alichokosea tho kwenye mgogoro kila mtu anakua na % zake za ukosefu yeye hawezi akayaanika mabaya yake hapa kuelezea kua alimkosea nini hadi akamkimbia sababu hataki kuusema ukweli usipolijua hilo ni ngumu kung'amua ukweli, Ila nimebaini hasemi ukweli km anaficha chanzo Cha tatizo,
Mbona unakua sio mwelewa aisee,ameshasema mwanaume alisema mtoto wao wa pili si wa kwake,huko kichwani umebeba nin aisee
 
Niliachana na aliyekuwa mume wangu miaka 5 imepita, kuachana kwetu kulikuwa kubaya sana kwa mambo mabaya yaliyopita katikati yetu. Sipendi kuyaeleza maana ni mabaya ila nilishayasahau na kuyaacha yapite.

Baada ya kuachana (aliondoka bila kuniaga na kodi ikiwa tunadaiwa miezi 5 bila kulipa) nilibaki na watoto huku nikiwa sina pa kuishi kwani mwezi 1 baadaye mwenye nyumba alinitaka kumuachia vyumba vyake, sina kazi, sina hata kitu kimoja kwa kuwa aliondoka na kila kitu hadi nguo zangu na za watoto na kwenda kusikojulikana alihama nikiwa sipo.

Kabla ya yeye kuondoka nilikuwa sijui kama tunadaiwa kodi, kwa kuwa kodi ya mwanzo ilipoisha alinambia kuwa kodi imeisha na yeye hana pesa kwa kuwa kazini kwake wamepata hasara analipwa nusu ya mshahara ambao ndio tunatumia kujikimu nyumbani.

Tukashauriana nikope pesa kwa ndugu yangu ambaye amekuwa akitusaidia kutukopesha pale tunapokwama na tunamlipa kidogokidogo, nikamtafuta na akatukopesha, nikamkabidhi 1,200,000 ambayo ndio ilikuwa kodi ya miezi 6 nikajua kalipa kumbe kampa mwenye nyumba kodi ya mwezi 1 tu na nyingine sijui alikopeleka hadi leo.

Sasa alipoondoka ndio mwenye nyumba kunitafuta kuwa nadaiwa miezi 5 hadi siku ile na nimeshaanza mwezi wa 6 ivyo ananipa wiki 1 nimuachie nyumba yake, kumbuka hapo nalala chini mimi na watoto kwa kuwa kila kitu kilishaondoka na yeye. Na nafanya kazi ndogondogo kupata chakula cha watoto.

Nikawaza kurudi nyumbani, Kilichonishangaza ni kuona ndugu zangu wote hawapokei simu zangu na wakipokea wananilaumu tu kuwa nimeyatafuta mwenyewe na nisiwasumbue na wanakata simu. Nikawaza nimeyataka yapi? Nimekosea nini? Mbona changamoto zangu pande zote wanazijua kulikoni nalaumiwa leo, nikajaribu upande wa aliyekuwa mume wangu ndio balaa zito.

Mtu 1 akaniambia unajua kuwa Unatuhumiwa kuzaa nje ya ndoa? Nikahamaki, akaendelea kusema baba fulani amewaambia ndugu zako na zake kuwa mtoto huyo mdogo sio wa kwake na ndio maana kaondoka. Nikamwambia hapana haiwezi kuwa kweli kwa kuwa sijawahi kutoka nje ya ndoa hata siku moja. Na kama kasema hayo basi ana lake jambo huenda kaamua kuficha mambo yake kwa kunitwisha mzigo maana tayari alikuwa hana pa kukwepea kutokana na mambo yake.

Basi nikatuma ujumbe mfupi kwa ndugu zangu kuwa, nashukuru kwa kuwa nimejua sababu ya nyie kunichukia ila nawaambia siyo kweli na sijawahi kufanya uchafu huo ila nipo tayari wakapime DNA nchi yoyote na ikibainika ni kweli basi wanihukumu nikazima simu ili nipate muda wa kuwa peke yangu kuwaza nini cha kufanya, nikaanza kuwaza cha kufanya nalia peke yangu.

Nikaanza safari ya kutafuta chumba japo sijui nalipa nini, nikapata mama mmoja nikamweleza hali yangu akanambia nakupa chumba ila utakuwa unanilipa mwezi mmoja mmoja sh. 60000 na mwezi huu nakupa ukae bure utaanza kunilipa mwezi ujao, nikaona chumba ni gharama ila kwangu ilikuwa ahueni maana nina mwezi mmoja wa kuanza maisha kutafuta kodi ya watu.

Nikahamia hapo, na wanangu tukaanza maisha, mwezi mmoja baadae nikapata kazi japo haina mshahara mzuri ila inaniwezesha kupata chakula na kulipa kodi ya 60000 kila mwezi, nikaanza kujibana na kununua vyombo, godoro, kitanda, nguo za watoto nk.

Miezi 7 baadaye nikaja kujua alikokwenda yule mwanaume, na kwamba alipohama alihama na mwanamke mmoja ambaye alikuwa mchepuko wake wa siku nyingi wakaanza maisha yao, nilikutana na ndugu wa huyo mwanamke ndiye aliyenipa taarifa hizo.

Baada ya miaka 2, mwanaume huyo alinipigia simu, akidai anataka kuniona kanikumbuka, nikamwambia huwezi kuniona na wala hutakaa ujue naishi wapi, kwa kuwa sikutaka hata waliokuwa wanatufahamu wajue naishi wapi pia, baada ya kumjibu ivyo akasema kwa kuwa hutaki nikuone basi nilichotaka kusema sitasema, japo nilikuwa na lengo la kuonana na wewe ili nianze kukupa hela ya matumizi ya watoto kwa kuwa umekataa na mimi sihudumii hao watoto, nikamwambia kama wameishi miaka 2 bila huduma yako, basi wataishi tu.

Akawa anaendelea kunitafuta kwa namba mbalimbali huku akifoka na kuniita nina kiburi, jeuri, sina adabu kwake, nitakuwa nimepata mwanaume ananipa kiburi nk, mara aseme nitakuwa nimewalisha watoto sumu kuwa yeye mbaya ila yeye sio mbaya anataka kuwatunza ila mimi ndio nazuia. Mwisho alikata tamaa na sasa imepita miaka 5 nikiwa naishi na wanangu.

Inaniuma sana kuishi na wanangu wakubwa sasa ndani ya chumba 1 kikiwa ndio chumba na ndio sebule kwa kuwa sina uwezo wa kulipia zaidi ya chumba 1 ukizingatia ni wa kiume ila sina jinsi najipa moyo kuna siku nitapata nafasi ya kupata walau vyumba 2 wanangu wakalala tofauti na mimi mama yao.

Nimejitahidi kuandika matukio machache kwa kuyakata sana ili nisiwacoshe
dah pole dada
 
Yawezekana wewe unakijua kiseme, nilishasema nina mengi ila siwezi eleza naona mmekazania
Ndio ueleze chanzo Sasa Cha jamaa kukukimbia ni nini ? Maelezo mengine sawa tumeyapokea okay turudi nyuma chanzo ni nini hadi akafikia maamuzi ya kukukimbia ? Huwezi ukasema hujui maana najua unajua Ila hupendi kusema ukweli, na hautaki ukweli ujulikane Ila picha mbaya ya wanaume kukimbiwa wanawake na watoto ndio unayotaka ionekane, Jambo ambalo sio sahahi kwa kuangalia kwa upana na kwa kina
 
Yote 9 Ila 10 mwambie aelezee chanzo Cha tatizo hadi akakimbiwa na mwanaume wake, km hasemi chanzo hii kesi inatupwa mbali haina mashiko maana yeye ni muongo haelezei mabaya yake anaelezea mabaya ya Mwanaume wake tu
Isitoshe kusema hujitambui [emoji706][emoji706][emoji706]
 
Mbona unakua sio mwelewa aisee,ameshasema mwanaume alisema mtoto wao wa pili si wa kwake,huko kichwani umebeba nin aisee
Umeshikiwa akili nini ? Hio ni hearsay huelewi maana ya hearsay, hearsay evidence is not admissible (tho there are some exceptions) unaelewa maana yake ?
 
Wanawake huwa mnachekesha sana...yaani ugombane na mzazi mwenzako then ugomvi uuhamishie kwa watoto!! Kwanini umzuie baba watoto wako haki ya kuonana na kuhudumia wanawe??

Ni wazi ushawalisha sumu za kutosha hao watoto kuwa baba yao ni mbwa tu. Unawanyima watoto wako haki ya kumjua hata baba yao. Wanawake mnahukumu mambo kwa mihemko pasi na kutumia hekima na busara.

Kwanini usingemruhusu huyo aliyekuwa mumeo awahudumie watoro wake?
 
Yani wanaume bana story akileta mwanamke inayohusu ujinga wa mwanaume mnasema hamtaki kuhukumu bila kusikiliza upande wa pili, ila story akileta mwanaume inayohusu ujinga wa mwanamke wala hutasikia hayo mambo ya upande wa pili ni matusi na dharau tu kwa wanawake, seems ni either wanaume wanajiona innocent sana au wanajijua wana makosa ila wanaona kama makosa yao ni madogo na yanavumilika
 
Isitoshe kusema hujitambui [emoji706][emoji706][emoji706]
Wewe unajitambua nini hapo ulipo ? Nini unachojitambua kulishwa maneno ya uongo na yenye kupandikiza chuki kwa wanaume bila kueleza ukweli kwa kina ndio unaona umejitambua ?
 
Yani wanaume bana story akileta mwanamke inayohusu ujinga wa mwanaume mnasema hamtaki kuhukumu bila kusikiliza upande wa pili, ila story akileta mwanaume inayohusu ujinga wa mwanamke wala hutasikia hayo mambo ya upande wa pili ni matusi na dharau tu kwa wanawake, seems ni either wanaume wanajiona innocent sana au wanajijua wana makosa ila wanaona kama makosa yao ni madogo na yanavumilika
Issue sio kusikiliza upande wa Pili, issue ni source ya mgogoro wao ni nini ? Story yake ipo vizuri Ila kwenye source kaficha code na hataki ujue we unamwelewaje amelenga nini hapo sasa km sio kutaka wanaume waonekane wote wanakimbia wanawake bila sababu, aeleze chanzo ni nini na hicho chanzo hajakieleza na kasema wazi hatokieleza sasa ndio nini ? Ina maana gani ?
 
Duh huna bahati kwahyo miaka 5 yote hujapata jamaa lenye utindio wa ubongo ukakaa nalo au nyie ndio mnajiita wanawake jeshi kubwa. Tafuta msaidizi utalala na watoto mpka waote mavuzi ohoooo endelea kujidai umeumizwa hutaki tena wanaume fungua macho ona mbele kitembeze kitwga uchumi ww kikalie kioze
 
Pale mwanamke anapomshauri mwanamke mwenzie, hongera kwa ushauri
 
Wanawake huwa mnachekesha sana...yaani ugombane na mzazi mwenzako then ugomvi uuhamishie kwa watoto!! Kwanini umzuie baba watoto wako haki ya kuonana na kuhudumia wanawe??

Ni wazi ushawalisha sumu za kutosha hao watoto kuwa baba yao ni mbwa tu. Unawanyima watoto wako haki ya kumjua hata baba yao. Wanawake mnahukumu mambo kwa mihemko pasi na kutumia hekima na busara.

Kwanini usingemruhusu huyo aliyekuwa mumeo awahudumie watoro wake?
Khaa yani kuna watu vitu mnaandika hadi unajiuliza huyu mtu anatumia kiungo gani kufikiri, kwahiyo huyo mume alipokuwa anawakimbia hao watoto na kusema kuwa mmoja siyo wake alitegemea nini, kwanini wanaume mnakuwa ni watu wa kutaka kufanya makosa, halafu wanawake wachukulie poa tu kana kwamba hakuna kilichotokea, hivi ushenzi wenu huwa mnaona ni mdogo siyo
 
Back
Top Bottom