Nilijinunulia Pete, Nikagharamia harusi mwenyewe, Ndoa ikafa baada ya miezi minne

Nilijinunulia Pete, Nikagharamia harusi mwenyewe, Ndoa ikafa baada ya miezi minne

Tukasameheana

Sema Ukamsamehe.

Hayupo mwanaume timamu atakusamehe ukishamsaliti huyo sio mwanaume.

Wadada,mwanaume kamili hasamehi usaliti moja kwa moja.Akikusamehe usaliti ujue huna thamani km mwanzo,Ujue una mwanaume dhaifu sana,ujue atalipiza kwa namna nyingine.

Mwenye kusikia na asikie.Huo ndo udhaifu wa mwanaume.Tupo hivyo

Kama ambavyo mwanamke hawezi kutoa hela yake kwa mwanaume bila masimango.Wapo hivyo

Dada zangu ukisaliti ukastukiwa km upo kwenye mahusiano jua kbs ule upendo kwetu sisi haupo.Jua kbs 70% ya wanaume wanakuwa na chuki ambayo hata ukipata ajali kubwa au ukifa leo wanaweza sherekea kimoyomoyo.Huyo ndo mwanaume


Ila maendeleo yamekuja na wanaume dhaifu hili wadada litawasaidiA
Hii post ungeandika kwa herufi kubwa.
 
KWELI mkuu,
Mimi kupitia uandishi wake unaweza kujua alikua Ni mwanamke anayekera Kama bernad morison.

Mwanamke flani hivi,
Wa Mashindano na kupenda ligi.

Mwanamke flani hivi alikupa Ela yake lazima imuume Sana, na atakusimanga nayo.

Mwanamke flani hivi tulisoma shule ya msingi wanaitwa MWANAMKE SHUPAVU[emoji4]
Hahahaha
 
Kwani wewe unaruhusiwa kumnyanyasa mtu kihisia???

Unadhani kupiga kunakuja hivi hivi.

Embu tuwe wa kweli kuna kitu kinaumiza kuliko kunyanyaswa kihisia???hamjiulizi kwanini kila kabila saivi wanapiga wanawake maana hapo mwanzo mlimuwa mnasema wakurya wanapiga saivi kila kabila wanapiga.

Ndo tuseme wanaume wote wamejifunza upigaji kupitia wakurya?unyanyasi wa kijinsia hautaisha mpk siku tutakapokaa chini na kuulizanA maswali ya msingi.Kwanini wanaume wamekuwa wapigaji?kwanini wanawake wamekuwa na mdomo?halafu tujue tunatatuaje tatizo moja kwa moja na sio kufunika kombe.

Mnataka kuulaumu ukimwi na kuwaacha wafanya ngono?mkisema ukimwi unaenea tukubaliane ni kwa sababu tunafanya ngono.Haujienezi wenyewe.
Pumzika

Sent from my SM-G960U using JamiiForums mobile app
 
Hamna mwanaume alokamilka anaweza itaka ela ya mwanamke,

Uyo mume wa mtoa mada ni mitihini tu ya dunia ilimkuta akawa ana jinsi,

na kwa maelezo ya mtoa mada, jamaa hakua marioo kabisa ndo Mana alikua na uthubutu was kusimamia heshima yake isivunjwe kwasababu TU mwanamke anavijisenti.
(Makofi, waliachana na wakarudiana)
Nakuelewa saana mkuu
 
Hamna mwanaume alokamilka anaweza itaka ela ya mwanamke,

Uyo mume wa mtoa mada ni mitihini tu ya dunia ilimkuta akawa ana jinsi,

na kwa maelezo ya mtoa mada, jamaa hakua marioo kabisa ndo Mana alikua na uthubutu was kusimamia heshima yake isivunjwe kwasababu TU mwanamke anavijisenti.
(Makofi, waliachana na wakarudiana)
Sielewi hata unatetea nn
Sasa insecurity za mwanaume ndo ajihami? Tukubaliane hapakua na Mapenzi hapa. Kila mru abaki na chake

Sent from my SM-G960U using JamiiForums mobile app
 
Hapo ndipo mnapojua wanaume tuna moyo wa kipekee uliojaa upendo. Mwanaume ana uwezo wa kuishi na mwanamke hasiye na kazi na akamtunza kuanzia mke pamoja na familia yake.

Ila mwanamke kumvumilia mwanaume anayepitia changamoto za kiuchumi hamuwezi.

Ndio maana mwanamme akipitia misukosuko ya kiuchumi kuna 90% ya ndoa kivunjika, kwani ndoa imeshikiliwa na sentensi mbili.

1 Shida na raha.
2.ugonjwa na uzima

Dada zangu wanaingia kwenye ndoa na kufurahia kuvaa shela na show off ukumbini huku akiwa hajui hizo sensensi mbili zina maanisha nini.
Hayo si maandiko yameagiza hivyo? Mnapenda sana kulelewa mkuu?

Sent from my SM-G960U using JamiiForums mobile app
 
Hayo si maandiko yameagiza hivyo? Mnapenda sana kulelewa mkuu?

Sent from my SM-G960U using JamiiForums mobile app
Tufanye mimi sijui haya,niambie ww viapo vya ndoa vinasemaje?

Nani anapenda kulelewa........? hivi partner wako umeanza mahusiano yupo vizuri kiuchumi na huduma anatoa vizuri....... ila kuna vipindi (vinaweza kuwa virefu au vifupi) anapitia changamoto za kiuchumi.... hivi huyu utasema anapenda kulelewa?

Ila si shangai kwenye swala 50/50 mnalolipigania hali include kipato chenu bali cha mwanaume.
 
Kosa ulilofanya hapo ni moja tu, KUKUBALI KUWA ULIMSALITI. Hakuna mwanaume anaweza kuvumilia mwanamke hususan mke wake kumsaliti.Hata akikusamehe bado maumivu ya kumbukumbu yataitafuna ndoa yenu directly au indirectly
 
Mume wangu tulikutana chuo, mimi nikiwa na miaka 20, yeye 21. Tukaanza kuishi pamoja kama mke na mume.

Tulikuwa tukiandika majarida mitandaoni ndo tunapata pesa ya kujitunza wenyewe, na ndo pesa nilimsomeshea mdogo wangu kwani mama alikuwa mgonjwa na tuliishi maisha duni sana. Mimi na mume wangu tulilelewa na mama pekee.

Ikatokea kozi aliyokuwa anasoma mwenzangu kuwa na shida, wote waliokuwa wanaisoma wakasimamishwa masomo kwa muda, na kulikuwa na kesi mahakamani. Lakini baadae ilirudishwa na wenzake walirudi shule lakini yeye hakurudi, kwahiyo hakumaliza chuo. Nafikiri pia pesa aliyokuwa akipata wakati huo ilimfanya asirudi chuo.

Me nilisoma nikamaliza. Sikukaa muda mrefu nikapata kazi. Huku mwenzangu kazi ya uandishi ilianza kusuasua, mara asiandike, kwahiyo me nikawa ndo nalipia matumizi yote nyumbani.

Nikasema itakuwa wakati muafaka kuzaa, labda tukipata mtoto atapata moyo wa kutafuta kwa bidii. Tukapata mtoto, lakini mambo yalikuwa yaleyale. Mimi huku nako niliendelea kuchakarika, kuanzisha biashara n.k.

Nilichogundua, mwanaume akiwa hana kitu chake/pesa yake anakuwa hajiamini kabisa.

Basi hapo akaanza ku cheat. Me mwenyewe kusema ukweli nili cheat pia, maana unaenda kazini unakutana na wanaume wachapakazi unarudi nyumbani unamuona mwenzako kakaa tu unawaza huyu vipi! Tukaenda hivyo baadae baada ya kugunduana tukakaa kuongea, tukasameheana tukakubaliana tuanze upya.

Lakini mambo yalikuja kuwa mabaya zaidi, alininyanyasa kihisia na mwishowe alikuwa akinipiga.

Tukaamua tuachane, hiyo ni baada ya miaka tisa ya kuwa pamoja. Akaondoka nyumbani. Kwakweli nilivurugwa sana. Nilihisi amenipotezea muda mwingi, kanikuchua Nina miaka 20 kaniacha nina 29.

Nikawa mtu wa pombe. Narudi nyumbani saa nane usiku na asubuhi naenda kazini yani sijui niliwezaje kufanya kazi. Nikawa na mahusiano kadhaa, mmoja hadi aliniingiza kwenye utumiaji wa madawa.

Baada ya miaka miwili ya hayo maisha nikasema huku nje sio! Bora kurudi kwa shetani ninayemjua. Na hilo lilikuwa kosa kubwa sana nililofanya. Basi tukarudiana na huyo mume wangu, ambaye bado alikuwa Hana kazi.

Hapo mimi nikawa nimeokoka. Nikasema haya mahusiano tusirudishe yalivyokuwa, tuanze upya kama Mungu anavyotaka. Basi tukajiunga kwenye darasa la wanaotarajia kuingia ndoani.

Tukapanga siku ya harusi. Nikawa nampa pesa alipie vitu hadi mahari, maana huwa tunaambiwa kumfichia mwanaume aibu unampa yeye hela ndo atoe.

Nilijinunulia Pete nikampa, siku mmoja tulienda mgahawani akanivalisha. Kwahiyo mitandaoni mtu anaona tu nimevalishwa Pete hajui story.

Nilikuwa very desperate kwakweli, na nilifanya hivyo kwasababu kwanza niliona maisha huko nje sio, na pili nilitaka mwanangu awe na familia iliyokamilika. Harusi ilinimalizia akiba yangu yote.

Basi tukafanya harusi, tukaanza kugombana huko huko honeymoon! Kurudi nyumbani tena manyanyaso yalizidi.

Nikiri kuwa wote na mume wangu tuna tatizo la hasira, tena me wananiitaga mdomo pistol maana maneno yanayonitoka nikikasirika ni kama pistol.

Alikuwa akininyanyasa kihisia kwa kunikumbusha makosa yangu ya zamani kila mara. Vipigo vilizidi hadi mama yangu ambaye alikuwa amekuja kuishi na sisi akasema hataki kuishi hapo arudishwe kwao.

Tulijaribu counseling, pastor wetu alijitahidi sana kusaidia ndoa yetu. Unakuta baada ya misa anatuita, ananiambia ukirudi nyumbani wewe fanya hivi na hivi lakini tukifika nyumbani unaibuka ugomvi, ananipiga hadi majirani wanaamka.

Mtoto naye niliitwa shuleni nikaambiwa anaongea sana kuhusu kupigana, kwamba anaogopa anataka kumlinda mama yake lakini hajui amlindeje. Wakamuanzishia therapy shule. Na kazini kwangu pia kuna huduma ya counseling nilimpeleka.

Alipata therapy kwa miezi kadhaa na alianza kupona maana aliacha kuuliza kama nitarudiana na baba na siku moja therapist wake alimwmbia achore picha ya familia yake, akajichora yeye na mimi tu.

Sasa hivi tunaweza kuangalia picha za baba yake tukamuongelea vizuri. Kabla ilikuwa akiona picha ya baba anaanza kulia. Inauma sana kuona mwanao anaumia, bora ingekuwa kaumia mwilini ungesema ngoja nimpake hiki, lakini kihisia hujui ufanye nini!

Baba yake niliachana naye baada ya kujua kuna mwanamke mwingine, ex wake.

Ndo nikasema haiwezekani juhudi zote nazofanya, nimejitahidi kubadilika, kuomba msaada kanisani, nikawa mtu wa sala asubuhi mchana jioni ni kuomba tu Mungu aiponye ndoa yangu, nalipia bills zote, yeye kutwa kunikumbushia makosa yangu ya nyuma, halafu kumbe ana mwanamke mwingine!!! Nisingejua kuhusu huyo mwanamke nafikiri bado ningekuwa naye. Nikamwambia aondoke. Hiyo ni miezi minne tu baada ya harusi.

Wakati tunafunga harusi binafsi nilikuwa na furaha. Lakini niliwahisha mambo, hatukukaa kufikuria kwanini mahusiano yalishindikana mara ya kwanza. Kwakweli kufanya harusi haiondoi matatizo kwenye ndoa au mahusiano yenu.

Niliumia sana kuachana naye, hasa baada ya kufanya harusi kubwa miezi minne tu iliyopita. Nilikuwa silali. Nilikuwa na mawazo ya kujiua. Nikaanza kupata anxiety attacks.

Nikaenda hospitali nikaanza kupewa dawa na kufanya therapy kwa miezi kadhaa. Mawazo ya kujiua yamepotea. Nimekubali kuwa nimejitahidi kadri ya uwezo wangu kuokoa ndoa yangu.

Nikajiunga na divorce classes, yanasaidia kukabiliana na hisia zinazokuja na talaka kama Uoga, hasira, Upweke. Ni ngumu kujifunga huko tena baada ya miezi minne tu ya ndoa, unawaza utaambiwa na watu Mungu hapendi talaka. Sawa hapendi talaka lakini anampenda yule mtaliki.

Najihisi nimekuwa mtu bora zaidi, Najua nilipokosea, Najua ninachotaka kwenye mahusiano.

Sisemi kwamba ikitokea shida udai talaka. Pigania ndoa yako. Ipiganie mpaka hata Mungu akishuka aseme kweli ulifanya hiki na hiki na hiki. Ukiona imefika mwisho, achana nayo. Talaka sio mwisho wa maisha.

Mimi naona mume mzuri ni mwanaume anayemjua na anayeongozwa na Mungu kwasababu huyo atajua jinsi ya ku behave. Awe mchapakazi na Anayechukulia maagano ya ndoa kwa uzito.



Wajinga hivyo vikazi vyenu ndo hua vinawatia kiburi na jeuri. Wewe huwezi kuona ila amini nakwambia huyo mume wako ndio alikua mvumilivu kuishi na wewe na wewe haukua na uvumilivu wowote.
 
Back
Top Bottom